Kwa taarifa yako mbadala wa Zito ni zaidi ya zito, huyo ndiyo mwalimu wa zito katika siasa, anaitwa yaredi fubusa, huyo ni zaidi ya tundu lisu, kwa wale waliosoma milambo sec 1994 wanamkumbuka alikuwa mwenyekiti wa shule akapingana na walimu kwa msimamu dhabiti wakamtoa, akiwa shule aliwahi kumtikisa Dr Warid Kabour wakati huo upinzania ulikuwa Kigoma tu Tanzania nzima, Arusha wamejifunza siasa za upinzani kutoka kigoma, ni mkoa uliotoa mbunge kutoka chadema aka upinzani nchi nzima yaani Dr. Warid Kabour 1993 mwaka mmoja tu baada ya kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Arusha wanapata machungu ya polisi sasa wakati sisi hata makovu yanafutika, kwenye uchaguzi wa 1994 train mbili zikiwa na askali polisi zilitua kuzima upinzania lakini walishindwa. hivyo kaskazini ni wajukuu wa siasa za upinzani kwetu. Sisi hatuandamani wala kupigana tunafanya kweli kwenye sanduku la kupiga kura, ukisema tuandamane tunakuacha tunaenda zetu shambani au kazini lakini letu moja. Hata hatuhitaji kuhamasishwa tunajua wajibu wetu kwaani tumekomaa kisiasa kama wapiga kura. Na hatuchagui majina bali tunachagua wachapa kazi mfano: ZITO KABWE, MOSES MACHALI, MKOSAMALI, DAVID KAFULILA nani asiyejua michango yao bungeni? na kama si hila za CCM kuiba kura kwenye majimbo ya kigoma mjini peter serukamba na obama kasulu magharibi CCM ingekuwa hoi, kidogo Mheshimiwa waziri eng Christopher Chiza kwa sababu hana siasa za maji taka tunamheshimu japo yupo CCM.
Watanzania njooni mjifunze siasa Kigoma.