CCM kwa haya tumewadharau sana Walimu

CCM kwa haya tumewadharau sana Walimu

Awsom

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
1,085
Reaction score
307
Habarini Wadau,

CCM tumeiongoza nchi hii kwa muda mrefu zaidi ya miaka 50, na kwakweli yapo mengi mazuri tuliyoyafanya (watanzania ni mashahidi) LAKINI niweke wazi kuwa Tumewanyanyasa sana Waalimu wa Tanzania kwa miaka mingi kwa kutoyatimiza ahadi zifuatazo:-

-Tumeshindwa kuwapandishia mishahara yao ingawa bidhaa zinaongezeka thamani,na hawana Marupurupu.

-Tumewaahidi sana kuwapandisha madaraja yao kikazi bila kutimiza hilo katika asilimia kubwa ya waalimu.

-Tumeshawadharau sana mpaka kuwaita Mbayuwayu (aina ya ndege) na Pia kuwachapa.

-Tumekuwa tukiwatumia katika sensa,kuhesabu kura na katika shuhuli mbalimbali bila kuhesabu kama overtime na kuwalipa.

-Tumewapa ahadi ya laptop pekee badala ya kushuhulikia kero zao za msingi mfano umeme na hayo yaliyotajwa hapo juu.

Ni wakati wa kutafakari namna ya kufanya kama tutashinda uchaguzi hapo October.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
Ccm ni sawa na sikio la kufa hata uwachome mikundu hawasikii tena,ndio kifo chao kimefika,waache manake ndio saa na dk zao zimefika
 
Duu na MAWAA yote hayo mliofanyiwa lakini bado kidumu chama cha mapinduzi...!!
Kazi ipo.
 
Una moyo wa chuma me moyo wa nyama ningepasuka ila kupenda ni upofu
 
Unaona walimu tu,kuna polisi,magereza na ukiangalia wanaonufaika na Tanzania ni wale top layer tu,ss ni piga chini sisimu tu
 
Hapa dawa ni kubadilika Walimu,ile dhana ya Umbayuwayu,uchanganye za zako kufanya maamuzi sahihi october 25
 
Walimu, polisi, madaktari na manesi, magereza wote wameonewa na CCM ila bado wanaendekea kuwachagua.
 
Tatizo Mwaka Wa Uchaguzi Watanzania Tunadanganyika Kirahisi Sana, Sijui Tunarogwa!?
 
Back
Top Bottom