Ukweli uwe mtamu kusema japo ni mchungu sana, kwa sasa CCM inabebwa na dola kama Chama Tawala ila kwa ndani imeshajifia

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
320
899
Wakuu habari?

Ni matumaini yangu kuwa mko poa sana katika harakati zetu za watu weusi kutafuta rizki ya kila siku.Wanasema hatuwezi kuacha kujihusisha na Siasa sababu Siasa ndiyo ina mstakabali wa maisha yetu,kwa siku za hivi karibuni yaani kuanzia 17.3.2021 hadi sasa nimekuwa nikifatilia vyama vya Siasa kwa ukaribu zaidi juu ya mipango na malengo waliyonayo ya kuisaidia Taifa kupiga hatua na kuleta mabadiliko ya Maisha na Miundombinu ukizingatia rasiliamali zote tunazo na nguvu kazi zipo.

Kwanza uhitaji wa kwanza wa Nchi yetu kwasasa kabla ya yote ni Katiba Mpya na pia kupata viongozi wenye maono na walio tayari kujitoa kwajili ya Taifa letu lakini kwa Bahati Mbaya sijaona chama chochote cha siasa wala kiongozi mkubwa wa kisiasa hapa nchini anayeweza kukata kiu hiyo kubwa ya Taifa letu na hapa inawapa CCM faida ya kukamata tena dola 2025-30 upande wa Urais kwa masikitiko makubwa niliyoyaona na kuyashuhudia katika hizi chaguzi za ndani ya CCM ilivyojaa rushwa na upendeleo hakika CCM imeshajifia inasubiri kuzikwa ila cha kusikitisha ni kwamba Watanzania walio wengi bado wana Imani na Matumaini kuwa ccm hii itawafikusha katika nchi ya ahadi. Aaaaah subutu!

Viongozi wa CCM ni waongo na wametawaliwa na uroho wa mali na madaraka kiasi kwamba wapo tayari kutoana kafara hata wao kwa wao ili kulinda maslahi yao binafsi kuliko Taifa kwa bahati mbaya hakuna wa kumpa changamoto ccm kwani act wazalendo ni mtoto wa kuzaliwa na ccm kama ilivyo nccr mageuzi,tlp na sasa CUF.

CHADEMA wao walikwishajizika wenyewe kutokana na mfumo wao wa chama wa kuwa na mwenyekiti wa milele hivyo inaonesha wanaopikwa pale hawatoshi kuongoza nchi kama ndani ya chama tu hawaaminiki na kukabidhiwa uenyekiti nankuonekana kuwa Mbowe pekee ndiyo mwenye maono ya kuongoza chama ina maana hao wengine hawawezi kuongoza CHADEMA iweje watu waliokosa imani ya kuongoza chama chao tu tuwape dhamana ya kuongoza nchi?

Sasa nikirudi kwenye mada tunaelekea 2025 bila chama cha siasa imara itakayoivusha katika nchi ya ahadi. CCM imeshajifia inasubiri kuzikwa wengine walikwishaoza siku nyingi japo hawataki kutuambia ukweli.

Sauti ya Mzalendo wa kawaida Tunaipenda Nchi yetu kwa moyo wetu wote kwani ndiyo sehemu tuliyopewa na Mungu kuwa urithi wetu.

Karibuni tuchangie
 
Back
Top Bottom