CCM kuwakaanga wabunge ‘watoro’ wa BMK

CCM kuwakaanga wabunge ‘watoro’ wa BMK

Wenye uwezo huo ni cuf,nccr wakiongozwa na chadema(ukawa) hawa wakisema tunafukuza wanafukuza kweli but not hao wasanii wa sanaa za kuchonga

Kuwafukuza wabunge ambao misimamo yao inatofautiana na chama hata kama msimamo wa chama siyo sahihi kwako wewe unaona huo ndio UJANJA! Nadhani CCM itakuwa imeonesha ukomavu wa kisiasa na demokrasia ndani ya chama tofauti na vyama vinavyohubiri demokrasia kwa maneno huku nyuma wameficha mapanga.

Demokrasia gani ambayo mbunge/mwanachama akienda tofauti na msimamo wa chama hata kama anaona hauko sahihi anaitwa msaliti na kufukuzwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wakuu

salaam kwenu

leo ccm wametangaza kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwa wamewaandikia barua wabunge 25 wa ccm waliogoma kuhudhuria vikao vya bunge (waliojiunga na ukawa)
kujieleza ni kwanini hawaudhurii vikao vya bunge hilo la katiba na ikithibitika hawana sababu za msingi watawatimua

my take ccm iache kuwanyanyasa wazalendo wa kweli wa taifa hili

Mkuu tusaidie majina ya hao wabunge maana nao wafikiria nawaona bungeni
 
Nawaunga mkono hao wabunge 25 natamani wangeongezeka zaidi kwani kuna ambao bado wako ndani wanatamani kutoka! CCM kukataa Rasimu ya Katiba ni dharau kubwa sana kwa wananchi. Kwa vile wao ni viongozi wanafikiri sisi hatuna haki ya kusimamia tukionacho kinafaa kwa nchi yetu?

Huyo Sita, Wassira na Lukuvi na Werema kuna siku watajuta kuzaliwa na kama si hapa duniani huko watakapokwenda wakishaaga dunia. VIVA wabunge 25 wa CCM mliotoka nje kwani usanii wa Sita na wenzake ni dhuluma kubwa sana kwa wananchi.

Leo unawaunga mkono wabunge wa CCM kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama chao mbona wabunge wa CHADEMA waliokwenda kinyume na msimamo wa chama chao wanaitwa wasaliti?

Je, unaanza kupata picha kuwa kuna wakati viongozi wa vyama au wabunge wanatakiwa kuwa na misimamo yao na siyo kufuata tu msimamo wa chama hata kama hauko sahihi?
 
Kuwafukuza wabunge ambao misimamo yao inatofautiana na chama hata kama msimamo wa chama siyo sahihi kwako wewe unaona huo ndio UJANJA! Nadhani CCM itakuwa imeonesha ukomavu wa kisiasa na demokrasia ndani ya chama tofauti na vyama vinavyohubiri demokrasia kwa maneno huku nyuma wameficha mapanga.

Demokrasia gani ambayo mbunge/mwanachama akienda tofauti na msimamo wa chama hata kama anaona hauko sahihi anaitwa msaliti na kufukuzwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Naongelea swala la kutishia tishia hizo tabia ziko ccm tu kwa wapinzani hakuna kutishia kama mtu kakeuka utaratibu wa chama anafukuzwa tu,kiongozi wa vijana wa ANC hakutishiwa na chama chake bali alifukuzwa nakuanzisha chama chake na leo ana wabunge wa3,sasa nyie ccm kila siku mnatishia tishia tu wakati ndiyo chama kongwe nchini fanyeni maamuzi

Wapeni uhuru wanachama wenu bs na kama wakikosea msiwafukuze kama mlivyofanya kule zenji,leo wanaoitaka Tanganyika ndani ya ccm wako wengi iwaje mfukuze mbunge mmoja tu tena toka zanzibar?

Kifupi hatuna la kujifunza toka kwenu ila nyie ndiyo mnayo mengi sana ya kujifunza toka upinzani pamoja nakutumia pesa na nguvu nyingi kutaka kuupoteza upinzani nchini japo its too late
 
ccm hawana ubavu wa kufukuza mtu, yule mbunge wa ZNZ anawatoa kamasi hadi leo wameamua kumbambikizia kesi
 
Tangu watoto wa kidato cha nne waingie hili jukwaa imekuwa shida kweli tarifa haijakamilika ni nyepesi halafu mtu anatuletea kajiamini kabisa,hayo majina ya wabunge yako wapi,lini wameandikiwa barua.
 
tangu watoto wa kidato cha nne waingie hili jukwaa imekuwa shida kweli tarifa haijakamilika ni nyepesi halafu mtu anatuletea kajiamini kabisa,hayo majina ya wabunge yako wapi,lini wameandikiwa barua.

izuie usitapike haraka...
 
Wakuu

salaam kwenu

leo ccm wametangaza kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwa wamewaandikia barua wabunge 25 wa ccm waliogoma kuhudhuria vikao vya bunge (waliojiunga na ukawa)
kujieleza ni kwanini hawaudhurii vikao vya bunge hilo la katiba na ikithibitika hawana sababu za msingi watawatimua

my take ccm iache kuwanyanyasa wazalendo wa kweli wa taifa hili

Weka barua hapa usiwekilaza kama jina lako
 
ni Chadema tu,ndio wana ubavu wa kufukuza mtu asiyefaa kwenye uongozi wa chama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom