CCM kutoka magamba hadi mizigo

CCM kutoka magamba hadi mizigo

Sigam

Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
81
Reaction score
27
Nimeshangazwa na mdogo wangu Nape kuja na msamiati mpya wa 'Mawaziri mzigo' baada ya ule wa Magamba.
Wajemeni Magamba na mizigo naona ni kitu hicho hicho. Hivyo kabla ya mizigo alipaswa kutueleza magamba yameishia wapi? Kama walishindwa kuvua magamba mizigo ndio wataiweza? Vinginevyo inatupasa tuamini kuwa CCM yenyewe ndio GAMBA na MZIGO hapa TZ. aidha tujiulize baada ya magamba na mizigo, watakuja na msamiati gani mwingine? Nazani watasema kuna viongozi MIZOGA!
 
Ni utamaduni wao na wanatekeleza sera yao ya ulaghai na udanganyifu kupitia misamiati

Kilimo ni uhai, mkukuta, mkurabita, kilimo kwanza, matokea makubwa, magamba nasasa mizigo sijui ccm wanaelekea wapi...?
 
Kulikuwepo na thread humu JF juu ya maandalizi kabambe ya mkutano wa wazee wa kimasai ulikuwa ukiandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, Edward Lowasa na Ole Medee. Leo ndiyo mkutano huo ulifanyika kwenye uwanja wa Technical College na kuhudhuliwa na wazee wa kimasai na Ole Medee mwenyewe. na haya ndiyo maazimio ya mkutano huo:
-kamwe kuanzia sasa balozi, wenyeviti wa vitogoji,mbunge,meya na nafasi zote za juu hapa mkoani Arusha kamwe wasipewe Wachaga au kabila lolote.
-kutokuwauzia viwanja/machamba wachaga.
-Wachaga waondoke warudi kwao Moshi.

yaliyofanyika leo hatupaswi kuyafumbia macho kama kweli watanzania tunalipenda taifa hili kwaani baada ya waziri, mkuu wa mkoa na pacha wa Kikwete(Lowasa) kuratibu mambo maovu kiasi hiki kwenye taifa letu, Leo wachaga wanaambiwa watoke Arusha waende moshi na waziri, je nao wamasai watoke moshi na kote tanzania warudi Arusha!? Kweli CCM mnaliangamiza taifa hili..
Nukuu za baadhi ya wasemaji waliokuwa wameandaliwa na Lowasa, Medee na Mulongo
" HUYU MWENYE LUBEGA NYEKUNDU ANASEMA KWAMBA HAIWEZEKANI TENA TUKAONGOZWA NA WACHAGA NDANI YA JIJI LETU LA ARUSHA NA HATA SIKU MOJA MEYA WA MJI WOWOTE NI LAZIMA AWE NI MZAWA NA WATAHAKIKISHA TUNA WEKA MTU TUNAYEMTAKA SISI.
HATUTAKI TENA MAMBO YA UONGOZI WA KICHAGA KUANZIA UONGOZI KIJIJI KATA NA HATA MKOA TOFAUTI.
TANGU LINI UONGOZI WA MEYA AKAPEWA MTU WA KUJA?????
JINA LA KIMANDOLU, NGARENARO LEO UKIMWULIZA HUYU MBUNGE ANAJUA MAANA YAKE???
HATUKUBALI TENA KUONGOZWA NA MAKABILA TOFAUTI KABISA.
HUYU MBUNGE HATUMTAKI NA NDANI YA SIKU 25 NA WAPATE MAJIBU YA KWAMBA ATATOKA AMA HATOKI."


MKUTANO MWINGINE UTAITISHWA ITAKAYOTOA MAAMUZI NA KAMA HAWEZI KUONDOAKA TUTAMUONDOA NA NA WACHAGA WENZA WAENDE MOSHI.."

HATUOGOPI VITA TUTAPIGA MPAKA TUHAKIKISHE TUNA BAKI NA ARUSHA KAMA WALIVYO PIGANIA BABU ZETU NA WALIBAKI ARUSHA,TUTAPIGANIA NCHI YETU HATA KAMA NI KUFA TUFE, LAZIMA TUTAKAPOITA KIKAO TUWAITE VIJANA WETU NA TUWALISHE YAAMINI YA KUTUNZA SIRI...KIPASULIWE CHUNGU KWAAJIRI YA WANAO VUJISHA SIRI - HERI WAFE, HATUTAKI WACHAGA KWENYE UONGOZI KWENYE MKOA HUU.....View attachment 102027

Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania...
====================


Angalia yalivyo makabila
 
Last edited by a moderator:
Poor ccm! Poor Nape! Baada ya M/kiti wake kusema kwamba wajiandae kuachia dola, atimae ameibuka na single ya mizigo!
 
ccm= chama cha mizigo.teh teh hii kali ya kufungia mwaka huu 2013 na kuanza nao 2014
 
Nimeshangazwa na mdogo wangu Nape kuja na msamiati mpya wa 'Mawaziri mzigo' baada ya ule wa Magamba.
Wajemeni Magamba na mizigo naona ni kitu hicho hicho. Hivyo kabla ya mizigo alipaswa kutueleza magamba yameishia wapi? Kama walishindwa kuvua magamba mizigo ndio wataiweza? Vinginevyo inatupasa tuamini kuwa CCM yenyewe ndio GAMBA na MZIGO hapa TZ. aidha tujiulize baada ya magamba na mizigo, watakuja na msamiati gani mwingine? Nazani watasema kuna viongozi MIZOGA!
Ndugu yangu QUOTE lakuvunda halina ubani
 
Ninachowaza ni kwa vipi tutautua huu mzigo!
 
Kiukweli ccm yenyewe ndio mzigo kwa Taifa,tushirikiane kwa pamoja tuutue mzigo huu salama kwani waonekana unaganda kama kupe na unataka kufa na taifa.
 
nimeshangazwa na mdogo wangu nape kuja na msamiati mpya wa 'mawaziri mzigo' baada ya ule wa magamba.
Wajemeni magamba na mizigo naona ni kitu hicho hicho. Hivyo kabla ya mizigo alipaswa kutueleza magamba yameishia wapi? Kama walishindwa kuvua magamba mizigo ndio wataiweza? Vinginevyo inatupasa tuamini kuwa ccm yenyewe ndio gamba na mzigo hapa tz. Aidha tujiulize baada ya magamba na mizigo, watakuja na msamiati gani mwingine? Nazani watasema kuna viongozi mizoga!
walianza na kujivua gamba wakachemsha sasa wametuletea singo ya mizigo hakika ccm ni mzigo
 
watashindwa kuiondoa hiyo mizigo kwa kuhofia kama kile kilichotokea huko sudan Kusin
 
Ccm chali,hawana sera tena kila siku wanashindwa kuchukua maamuzi magumu kwa sera yao ya kubebana,tunawasubiri 2015 tuone watakuja na usanii upi, chadema hoyeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
CCM wanaendeleza ulaghai na usanii hakuna cha mizigo wala nini,

Kama walishindwa kuwaondoa madiwani wa Kagera wataweza mawaziri?
 
mambo ambayo ccm wameifanyia nchi hii yanatisha kuliko yale ambayo MWOVU SHETANI ameifanyia dunia yote !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom