Ndugu Wanajamvi....!
Kutokana na kauli aliyoitoa katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (ccm) leo wilayani Nyamagana,Nape Nnauye ametoa kauli ya vitisho kwa watendaji wa serikali kwamba ni lazima wahudhurie vikao na mikutano ya chama ili kueleza wamewafanyia nini wananchi.
Nadhani Nape Nnauye ametumia nguvu nyingi akili kidogo kufikia maamuzi hayo. Hivi viongozi wa ccm hawawezi kuelezea utekelezaji wa ilani hadi watendaji kama mkurugenzi wa TANROADS,Mkurugenzi wa halmashauri,Afisa mtendaji wa kata au kijiji waache shughuli zao zinazowapa mwanya wa ujira waje kujieleza kwa maslahi ya ccm?
Mwajiri wa watendaji wa serikali ni nani? Je,kila mtendaji wa serikali lazima aitumikie ccm na tafsiri yake hakuna atakayepata kazi serikalini nje ya ccm? Mhe.Nape umekurupuka mno,katika kumbukumbu...uliwahi kuitisha kikao na walimu mjini Mafinga,ulifanya hivyo kama nani?
WANAJF:
Naomba kueleweshwa kama tunaongozwa na katiba ya CCM au TANZANIA?