CCM kutimua wabunge wanaohusishwa na CCJ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kutimua wabunge wanaohusishwa na CCJ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijafulia, Mar 27, 2010.

 1. s

  sijafulia Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na Martin Malera

  VIGOGO kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwamo wabunge machachari wanakabiliwa na hatari ya kufukuzwa uanachama kwa tuhuma za kujihusisha na Chama Cha Jamii (CCJ) ambacho kina usajili wa muda.

  Habari zinasema baadhi yao wamekuwa wanachunguzwa kwa muda sasa, na Rais Jakaya Kikwete anataka kuwatoa kafara kama njia ya kuwatisha wenzao wanaodaiwa kuhujumu CCM katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

  Mmoja wa wabunge wanaotajwa tajwa sana kuhusiana na ukaribu wake na viongozi wa CCJ, amekuwa mwiba mkali kwa CCM katika miezi kadhaa ya hivi karibuni; na amekuwa anadaiwa kuwahamasisha wana CCM kujiunga na CCJ.

  Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata zinasema kuwa baadhi ya vigogo walio hatarini kufukuzwa ni wabunge ambao wamejipambanua kuwa ni wapambanaji wa ufisadi, na wamekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wenzao kujiunga na CCJ.

  Hatua hiyo inatarajiwa kufikiwa katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Rais Kikwete ambaye kwa siku nne mfululizo zilizopita ametumia muda mrefu katika ofisi yake ya chama iliyopo katika ofisi ndogo ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

  Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM vinasema kuwa Rais Kikwete aliweza kubaini nia ya vigogo wa CCM kujiunga na CCJ na ameamua kuitisha kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM, (NEC); na anataka kukitumia kutisha wabunge wanaojihusisha na CCJ.

  Hata hivyo, habari hizo zinasema baadhi ya vigogo wanaolengwa na hasira hizo za Kikwete ni wale wasioweza kuleta madhara makubwa au kukigawa chama.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, ili kurejesha hali ya utulivu na amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, Rais Kikwete ameamua kuitisha kikao cha NEC cha dharura ili kuwashughulikia wanachama hao, wakiwemo wabunge na viongozi wengine mbalimbali ndani ya chama.

  Habari hizo zinasema kikao hicho kitafanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mliman City, na ajenda ya mkutano huo anayo Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete.

  "Jana na leo, Kikwete aliongoza vikao vya sekretarieti na kesho ataongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huku NEC, ikitarajiwa kukutana Aprili nane hadi tisa," kilisema chanzo chetu cha habari.

  Hiki ni kikao cha kwanza cha dharura kuitishwa na Rais Kikwete tangu aliposhika nafasi ya mwenyekiti wa CCM taifa.

  Kutokana na hali hiyo, wadadisi wa masuala ya siasa ndani ya CCM wanasema kwamba huenda kuna mambo mazito ambayo Rais Kikwete anataka kuyafanya, achilia mbali suala la kufukuzwa uanachama kwa baadhi ya wabunge, viongozi na wengine.

  Tanzania Daima Jumapili, imepata taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, ikibainisha ajenda zitakazojadiliwa na kikao hicho kilichobainishwa kuwa ni cha kawaida.

  Ajenda zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni maandalizi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, mapendekezo ya wanachama watakaogombea nafasi ya Katibu Mwenezi wa mkoa wa Dar es Salam na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

  Kikao hicho ambacho wajumbe wake tayari wameshafika jijini Dar es Salaam, kitapata fursa ya kupokea na kujadili taarifa mbalimbali zihusuzo masuala ya ndani ya chama.

  Tangu kuanzishwa kwa CCJ, baadhi ya vigogo ndani ya CCM, wamekuwa wakihusishwa nacho. Hali hiyo ilimfanya Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kutoa waraka nchi nzima kuwaonya makada wake wanaojihusisha na chama hicho ambacho kimejipatia umaarufu mkubwa kabla ya hata ya kupata usajili wa kudumu.

  Baadhi ya vigogo waliotajwa kuhusika na CCJ na ambao mara kadhaa wamejitokeza hadharani kukanusha ni pamoja na Spika wa Bunge Samuel Sitta na wabunge wengine waliokuwa wanajipambanua kama wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi.

  Hata hivyo, CCJ kilizinduliwa wiki iliyopita bila kuwepo kwa vigogo hao waliotarajiwa.

  Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa inawezekana kuna wabunge wa CCM wanataka kujiunga na CCJ lakini katika mazingira ya sasa hawawezi kufanya hivyo kwa kuhofia kupoteza viinua mgongo vyao. Fedha wanazopata wabunge kama kiinua mgongo ni zaidi ya sh mil. 40 ambazo zinawafanya wasite kuhama CCM, hasa katika mazingira haya ambapo CCJ bado hakijapata usajili wa kudumu.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  Mimi sielewi.. chama ambachho tumeambiwa ni hoax, hakiwatishi, ni geresha n.k kinawasumbua watu hivi..

  Jamani kipeni tu usajili wa kudumu halafu kiacheni. Si hakina mpango?

  I hope CCM hawatapoteza muda na hiki "kichama" wakati vyama vigogo vya upinzani vipo kwa miaka mingi sasa.

  Leave it alone!!!
   
 3. s

  sijafulia Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Awalali na watoto zao kwa ajili ya

  ccj...kikipata usajili rasmi si balaa!!!
   
 4. M

  Msee Lekasio Member

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki chama cha CCJ kimewaweka CCM matumbo moto. Maedheso yote wanayotoa yanaonyesha hawajiamini na hawajui ngufu sa adui yao. Fiongosi wa nji sasa wanatumia muda mwingyi kuunda mikakati ya kupambana na CCJ badadha ya kutatua kero sa wananchi.
  Ni mimi

  Msee Lekasio Makusare
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,319
  Likes Received: 1,076
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Kulwa Karedia

  LEO tunakutana tena katika safu hii nikiamini msomaji hujambo na unaendelea na majukumu yako kama kawaida.

  Tunakutana wakati taifa likiwa limetangaziwa mgomo wa wafanyakazi na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).

  Jambo hili linaonekana kuwa kama mzaha hivi, lakini naamini kama serikali haitachukua hatua madhubuti za kukaa chini na kusuluhisha hali hiyo, kwa mara ya kwanza tutashuhudia wafanyakazi wakigoma taifa zima.

  Leo sitaki kujiingiza huko zaidi kwa sababu masuala hayo naamini yako mikononi mwa vyombo vinavyohusika.

  Leo mada kuu ni uzinduzi wa Chama Cha Jamii (CCJ) uliyofanyika Jumapili iliyopita mjini Dar es Salaam na kushuhudiwa na watu kadhaa.
  Hivi sasa Tanzania imeendeleza utaratibu wake wa kusajili vyama vya siasa kila kukicha kama vile uyoga unavyoota wakati wa mvua, hiyo ni haki ya msingi kwa wale wanaoanzisha vyama hivyo kwa malengo yao fulani.

  Wiki iliyopita, CCJ ilifanya uzinduzi huo ambao kila sikio na jicho la mfuatiliaji wa masuala ya siasa alilielekeza kwenye chama hicho kusikia nani atatua kwenye chama hicho kinachoonekana kuanza kwa mbwembwe za aina yake.

  Moja ya jambo kubwa ambalo CCJ wamekuwa wakilisisitiza siku zote ni lile la kuzoa vigogo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Hakuna ubishi sentesi hiyo iliwafanya Watanzania kukosa usingizi ili kuona ni kigogo gani ambaye ataingia CCJ na kuandika historia mpya katika medani za siasa za taifa hili.

  Viongozi wa kitaifa wa chama hicho, wamekuwa mstari wa mbele kuwahakikishia Watanzania kuwa kuna rundo la vigogo kutoka CCM watatua kwenye chama chao, hali ambayo baadaye imegeuka na kuwa sawa na mchezo wa kuigiza.

  Bahati mbaya siku ya uzinduzi huo, nilibanwa na majukumu ya ofisi sikuweza kwenda katika eneo la tukio, lakini kupitia vyombo vya habari nilisoma na kushuhudia uzinduzi usiokuwa na vigogo wala vijiti.

  Nasema hakuna ‘vijiti’ kwa sababu niliamini kama vigogo wamekosa basi hata wale wanasiasa wachanga ambao hawana majina makubwa wangeweza kujiunga.

  Kinyume chake tulibaki tunashuhudia vijana wakicheza ngoma na kuvalia sare za CCJ tu, je, hawa ndio walikuwa aina ya vigogo wapya?

  Kuanzia siku hiyo, nilianza kuamini kuwa vigogo wa CCJ walikuwa na nia ya kuwahadaa Watanzania ama kujitafutia umaarufu mkubwa kupitia vyombo vya habari ili habari zao ziandikwe kwa uzito.

  Na kweli siku hiyo tulishuhudia vyombo vya habari vikiandika habari hizo kwa uzito wa aina yake, lakini kati ya hizo viliandika ‘uzinduzi CCJ wadoda’, ‘uzinduzi CCJ wapwaya,’ ‘vigogo CCJ wayeyuka.’

  Utaona namna ambavyo viongozi wa kitaifa wa chama hiki walivyobuni njia ya kutaka habari zao ziandikwe kwa kina ili ziwafikie Watanzania haraka.

  Sikatai kuwa vyombo vya habari vina wajibu wa kuandika, lakini si kuandika habari kubwa ambayo siku ya mwisho matokeo yake yanakuwa ziro.

  Nasema ziro kwa sababu hakuna hata kigogo aliyeonekana siku ile, sasa tutawaamini vipi tena viongozi wa CCJ siku wakisema kuna vigogo? Tutaamini kuna ‘vijiti’ tu ambavyo ni vyepesi kubebwa.

  Siku chache kabla ya uzinduzi huu, itakumbukwa viongozi hawa walisafiri hadi Kijiji cha Butiama, mkoani Mara na kuzuru kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

  Kupitia vyombo vya habari tulishuhudia wakiwa wameliangukia kaburi la Mwalimu Nyerere na kulia kwa uchungu. Sasa swali linakuja, kilio hiki ndiyo ilikuwa njia ya kumuenzi Mwalimu kwa kumtafutia vigogo?

  Niliamini wazi baada ya safari ndefu ya Butiama na kutoa heshima za mwisho pale Mwitongo, CCJ ingekuja na rundo la vigogo ambao siku za usoni ndio wangekuwa mabalozi wazuri wa kunadi sera za Nyerere.

  Kwa nini CCJ inawadanganya Watanzania kuhusu vigogo? Ni wazi kuwa hao vigogo waliokuwa wakidaiwa kuwamo ndani ya chama hicho ni hewa ambayo si rahisi kuonekana.

  Nasema hivyo kwa sababu sidhani kama kuna mbunge wa CCM ambaye anaweza kukiacha chama chake na kukosa mamilioni ya kifuta jasho ambacho ni zaidi ya sh milioni 45 kwa ajili ya kujiunga na CCJ kabla ya kuvunjwa kwa Bunge.

  Kila mmoja anafahamu fika kuwa macho, mikono na masikio ya Bunge yamekaa tayari kupokea vitita hivyo ili wavitumie katika kusaka nafasi ya kurejea bungeni ambako hivi sasa kumekuwa na ushindani mkali hasa baada ya siasa kuonekana ndiyo eneo zuri la kuvuma mamilioni ya walalahoi.

  Mbali ya wabunge, hata wale viongozi wastaafu kwa mfano John Samuel Malecela, Dk. Salim Ahmed Salim, David Cleopa Msuya, hawa bado ni vigogo wa CCM ambao wanalishwa na serikali siku zote za maisha yao kutokana na kushika nyadhi kubwa za uwaziri mkuu katika serikali ya Tanzania, je, watakubali kumwaga mboga?

  Napenda kuwasihi wanasiasa wa taifa hili kuacha kutanguliza au kutoa ahadi kubwa wasizoweza kuzitimiza.

  Ni wazi baada ya uzinduzi ule, CCJ watakuwa wameanza kujikaanga kwa mafuta yao kwa kushindwa kuwaweka vigogo mbele ya hadhira.
  Kama kweli ahadi hii ingetimia ningesema CCJ imekuwa na mkakati madhubuti ambao ungesaidia kuondoa dosari ya utitiri wa vyama vya siasa ambavyo vipo na baadhi yao havijawahi kuvuka hata Chalinze.

  Kuna zaidi ya vyama vya siasa 17 vilivyopata usajili wa kudumu, lakini vizuri mtandao wao unafikia wapi… utasikia majibu sisi ni watoto wa mjini bwana!

  Baadhi ya vyama vimekuwa miradi tu ya watu kutaka kuendesha maisha mjini na si kukomboa Watanzania zaidi ya milioni 35 walioko kwenye hali ngumu ya maisha.

  Umefika wakati sasa wa kuwa na vyama vya siasa vyenye lengo la kusaidia Watanzania, kwenda mbali katika mikoa kama Mtwara, Lindi, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Mara na kwingineko ambako huko ndipo Watanzania wanabanwa zaidi na chama kimoja tu.

  Kama viongozi wa CCJ watatumia busara ni vema wakawaomba radhi Watanzania kutokana na hadaa ya kuwa chama hicho kina vigogo wa CCM ambao tulitarajia wangetangazwa siku ile ya uzinduzi.

  Pili, CCJ warudi na kukaa chini ili kuangalia ni njia gani nzuri ya kueneza sera zao ili kupata umaarufu, badala ya kutwambia kila kukicha kuwa wamejipanga kuonyesha mabadiliko makubwa.

  Tatu, ningefurahi kama safari ya CCJ ya Butiama itaonyesha matunda, kwa sababu pale ni kama mlikwenda ‘kuhiji’, hivyo tumieni maombi yenu na baraka mlizopata Butiama kuwasaidia Watanzania.

  Nne, nawaambia jengeni mtandao wa kutosha msije kuwa kama vyama fulani vya kukaa mjini na kusubiri kuitisha mikutano ya waandishi wa habari, katika siku za karibuni tumewashuhudia viongozi wa baadhi ya vyama hivyo wakigeuka kuwa wasemaji wa kambi fulani.

  Tano, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmelisaidia taifa na chama tawala (CCM) kukiamsha katika lindi la usingizi na kuanza kutekeleza baadhi ya mambo ambayo yamesahaulika.

  Napenda kumalizia kwa kusema, CCJ ahadi yenu ya vigogo itawahukumu kama mkishindwa kuitekeleza kwa dhamira ya dhati, mzimu wa ‘Muhunda’ utawashukia.

  Watanzania hivi sasa wasingependa mambo ya kubahatisha au yasiyo na utekelezaji, wanataka vitendo, si brabra za wanasiasa wetu ambazo zimewachosha.

  Umakini wa kauli ni mzuri kuliko kujitafutia umaarufu tu, kiongozi anayejitafutia umaarufu kwa mgongo wa watu Fulani, kamwe hafai kuongoza nchi.

  Mapambano daima.
   
 6. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chanzo cha taarifa: Tanzania Daima. Ilinichanganya kidogo, nilidhani Martin Malera, Sayari.
   
 7. m

  miner Member

  #7
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hafukuzwi mtu wala kumvua uanachama mtu wakati haupo nao hawawezi kufanya kosa la kukigawa chama chao sasa uchaguzi keshokutwa itawagharimu, wataridhiana na kutoka wamoja kutetea ufisadi kwamba serekali ya ccm imeisha anza kuchukua hatua na watanzania watawashangilia. Tusubiri
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  hehehehe hehehehe
  hwa hwa hwa

  naongeza biwi la mahindi ya kuchoma na bilauri kadhaa za maji nikiwatch muvie
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 60,105
  Likes Received: 38,405
  Trophy Points: 280
  Wasanii tu hawa CCM hawakuwatimua Wabunge mafisadi akina Chenge, Karamagi, Yona, Mramba, Rostam na wengineo sasa ndiyo wataweza kuwafukuza chamani Wabunge wanaojihusisha na CCJ!? USANII MTUPU! Waanze kwanza kuwafukuza Wabunge mapapa wa ufisadi.
   
 10. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM haina mwenyewe.

  Kama wabunge watafukuzwa kwa kujihusisha na CCJ na Basi wabunge wanaojiusisha na CCJ wawafukuze wenzao kwa kuwa mafisadi tuone kama kuna atakayebaki.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  CCM ya sasa haina ubavu wa kumtimua mwanachama yeyote mwandamizi
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,070
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  leave alone kufukuza uanachana!!! hivi mwenyekiti mwenyewe wa kufukuza watu CCM nani?labda sio JK otherwise ni vikao vya kukutana tu na kunywa kahawa na kuchekacheka basi ,,,nothing substantial
   
 13. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine inasikitisha kuona jinsi ambavyo Watanzania tumefika mahali tunadhani kwamba hakuna chama cha siasa kinachoweza kuanzishwa na kushamiri bila kuwapo 'vigogo'. Tanzania ni ya wananchi wote maskini na tajiri, 'vigogo' na 'vijiti' na wote hao wana haki sawa katika kila jambo kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Naliunga mkono jibu lililotolewa na CCJ kwamba kwao wao 'vigogo' ni wananchi wa kawaida, wapiga kura wenye uwezo wa kuwaweka madarakani ama kuwanyima kura hao wanaoitwa 'vigogo.' Kwa maana hiyo uzinduzi wa CCJ ulihudhuriwa na 'vigogo' halisi wa nchi hii - wananchi wa kawaida.

  Tufike mahali tuache tabia ya kuwatukuza bila sababu hao tunaowaita 'vigogo' kana kwamba hakuna binadamu wengine wenye akili na mawazo ya kimaendeleo kuwashinda. Waasisi wa taifa hili hawakuwa vigogo walipoanzisha TANU, walikuwa ni wananchi wa kawaida kabisa na waliweza kufanya makuu ya kuwashinda Wakoloni Wazungu waliotumia kila aina ya mbinu chafu lakini 'vijiti' wa TANU walifanikiwa kulikomboa taifa letu. Naamini kama CCJ kina dhati ya kweli ya kutaka kuleta mabadiliko kinaweza kufanikiwa bila kuwa na 'kigogo' (kwa tafsiri ya Kulwa) hata mmoja!

  Mzimu wa Muhunda siku zote unasimamia haki, hausimamii kuwepo kwa vigogo!
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Mar 28, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,604
  Likes Received: 3,609
  Trophy Points: 280
  CCM nadhani sasa hawatilii maanani maslahi ya Taifa,yaani wameamua kuwa wachafu kweli kweli na wamechagua jalala kuwa makao yao
   
 15. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #15
  Apr 9, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inachekesha hii thread!!!!

  Hivi hao CCM watatoa wapi ubavu wa kufukuzana??
   
 16. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #16
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  jamani huu usanii wa CCM hautaisha!
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,523
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hawa CCM hawanapointi wala nini, wathubutu kuwatimua jamaa iwe kama kuongeza msumari kwenye jeneza lao!
   
 18. k

  kosamfe Member

  #18
  Apr 9, 2010
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili haliwezekani
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hilo ndo tunalo ombea walio wengi wameguke vipande pengine yaweza kuwa pona yetu!
   
 20. T

  Tristan Member

  #20
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hamna lolote usanii tu
   
Loading...