babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,221
- 3,167
Ndio, Mrema alikuwa ni kati ya wabunge walioshinda kwa kura nyingi wakati huo. Kupewa uwaziri ni kutoka na umachachari wake jimboni Moshi Vijijini -kabla haijagawanywa kuwa Vunjo na Moshi Vijijini- ambao ulimfanya kuandikwa sana kwenye magazeti kipindi hicho..
io
Asante kwa sahihisho, hii Moshi Vijijini na Vunjo bado inanichanganya sana. Namkumbuka Mbatia aliwahi kulitwaa, akaja Jesse Makundi ndipo akaingia Kimaro, hivi Mrema naq aliwahi, enzi zake akiwa CCM.
Alianza ubunge kwa nguvu ya hali ya juu. Mapolisi kipindi hicho walikuwa wananuka rushwa na unyanyasaji kutoka kwa wafanya biashara wadogo wa boda,mpakani mwa Kenya na Tanzania na kuwaacha wafanya biashara wakubwa ambao walikuwa wadili na maboss zao.
Umaarufu wa Mrema ulikuja kwa kuwatetea awa wafanya biashara wadogo hasusani wakinamama. Kama sijakosea alimpiga Polisi mmoja vibao kwa kukimbizana na wakina mama wanaofanya biashara ndogo ndogo na hii kama sijakosea tena ndiyo iliyompa uwaziri.
Kwa hiyo sitashangaa wanavunjo kuchagua Mrema kwa mazuri aliyowatendendea. Mimi binafsi ninaamini Mrema wa sasa hivi sio yule wamiaka ishirini iliyopita.