CCM Kupoteza Moshi Vijijini-Lyatonga Mrema Kuibuka Kidedea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kupoteza Moshi Vijijini-Lyatonga Mrema Kuibuka Kidedea!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 13, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Katika mapumziko ya long week-end hii, nilipata kajinafasi, nikaamua kubadili upepo, this time, nikaenda mitaa ya Moshi Vijijini,

  Nilianzia Njia Panda, nikapandisha Marangu, nikasimama kidogo Marangu Mtoni, Mamba na kupanda juu mpaka kule Marangu National Park. Kesho yake nikateremkia Kilema, kupitia bara bara ya Kawawa, nikaanzia Legho Kilema, nikaja Legho, Iwa Mission, nikaremkia Nduoni, nikashuka Tella, nikapita Sumi, nikaja Uparo na kuchomokea Kawawa Rd inapoungana na barabara ya Moshi Dar.

  Nilifanya hojaji isiyo rasmi kuhusu watanchagua nani, huwezi amini, asilimia klubwa chaguo lao ni Mrema, CCM hawana kitu kabisa. Mtu wa pili kwa kukubalika ni mgombea wa Chadema akifuatiwa na NCCR -Mageuzi.

  Imani kubwa waliyonayo ndugu zangu hawa kwa Lyatonga, bado wanaamini anaweza kufanya mambo. Hawajaamini kuwa amechoka, hana sera wala hana jipya ukilinganisha na yule wa Chadema. Wachagga wanachagua mtu, siyo chama, siyo sera, siyo uwezo, bali jina, na kwa Moshi Vijijini, mtu wao ni Mrema, Hawaoni hawaskii wala mtu hawaambii kitu!, kama ilivyo kwa Ndesa na jimbo la Moshi Mjini.

  Cha ajabu anachokifanya Mrema huyu, sio tuu anajipigia debe kuchaguliwa, bali anampigia chapuo la kiaina JK, kwamba ubunge mnichague mimi, ila kura za urais, mchagueni Kikwete!.

  Licha ya chama chake kuweka mgombea urais, na kuzinduliwa kwa kampeni zao jijini, Mrema kama Mwenyekiti wa chama, alipaswa kuwepo, lakini yeye alikacha, akiendelea na kampeni zake kule Kiraracha!.

  Angalizo, TLP, CHADEMA na NCCR, wasijeishia kugawana kura kama vita vya panzi, na furaha ikawa ni kwa kunguru!
   
 2. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lyatonga Mrema gani unayemzungumzia?
  Agustino Lyatonga Mrema? kweli usipo staajabu ya Musa utaona ya Firauni, all the best bwana A.L.Mrema katika kuibuka kidedea.
   
 3. p

  pierre JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hajui atendalo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Pasco, asante kwa information lakini sahihisho dogo tu ni kwamba nchi hii haina MARANGU national park bali ina Kilimanjaro National Park katika muktadha huu hapa.....

  Na labda kwa kucomment hili la wachagga kuchagua 'mtu'...inategemea na uwezo wa mtu, nadhani wako after maendeleo, kwa hiyo kama kuna mtu ana uwezo wa kuwaletea maendelea anachaguliwa bila kujali yupo chama gani, ndo kisa cha Ndesa pesa kuchaguliwa Moshi mjini, na Mramba atakavyopeta tena Rombo mwaka huu notwithstanding tuhuma zake za ufisadi na kesi mahakamani.
   
 5. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  sahihisho jingine , jimbo ulilotembelea ni Vunjo na sio Moshi vijijini, Moshi Vijijini ni Oldmoshi, Uru hadi Kibosho
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Pasco,

  Mkuu nakubaliana na wewe 100 %,Vunjo Mrema A L atapita kwa kishindo kikubwa.

  Nilikuwa huko maeneo ya Mkolowonyi Rawiya kwenye msiba wa mfanyakazi mwenzetu nilishangaa jinsi wananchi wa huko wanavyomkubali. Nilijifunza kitu kimoja kwa wapiga kura wa Vunjo wanajali sana mtu hawana habari za sera au chama.Vunjo sioni dalili za wapinzania kugawana kura hata kidogo Mrema A L ataongoza kwa kura nyingi sana labda uchakachuaji wa kura utokee.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  .
  Asante kwa Sahihisho, hakuna ubishi Wachagga hupenda maendeleo, hivyo watamchagua mtu atakayeleta maendeleo. Mrema alileta maendeleo na polisi posti zale kibao nchi nzima.

  Kwa maoni yangu, kati ya maeneo ya Kilimanjaro niliyatembelea ukiondoa Upareni, Vunjo ndio aneo linaloonekana limechoka, specifically Kirua Vunjo, barabara ni vumbi la kutupwa, na baadhi ya maeneo hakuna umeme, safari hii ndio nimeona angalau nyumba moja ya ghorofa pale Mandangeni, nikaelezwa ya Mzungu.

  Kwa uchovu alionao Lyatonga huyu kwa sasa, ni maendeleo gani anayokwenda kuwaletea watu wa Vunjo?. Nmehudhuria kampeni yake moja, hana sera, hana hoja zaidi ya kusisitiza "nichagueni mimi Agustino Lyatonga Mrema ndio nitawaletea maendeleo", hasemi ni maendeleo yapi, kwa resources zipi, na mikakati gani, yet atachaguliwa as populist leader with no agenda, no strategies, ila pia nakubali, akiingia bungeni, ataichachafya serikali.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  .

  Asante kwa sahihisho, hii Moshi Vijijini na Vunjo bado inanichanganya sana. Namkumbuka Mbatia aliwahi kulitwaa, akaja Jesse Makundi ndipo akaingia Kimaro, hivi Mrema naq aliwahi, enzi zake akiwa CCM.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Hapo ndo penye tatizo Pasco....Mrema ni tofauti sana na wengine kama kina Mramba na Ndesamburo, in that case wanamchagua sio kwa vile eti anaweza/ataweza kuwaletea maendeleo ila ni kwa vile, kama ulivyoisema, wanadhani mrema wa leo ni yule yule wa 1995. Kitu ambacho sio kweli kabisa.....Who knows, anavyompigia JK debe, anajua pia atampendelea kwenye bajeti so maendeleo yatakuja tu.... (lakini pia ukiongelea bara bara ongea pole pole manake maeneo mengine nchi hii ni balaa hata huko Vunjo wako better off)
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  .

  Kuna watu Kirua Vunjo, huwaelezi lolote kuhusu Mrema, mama mmoja mstaafu wa idara nyeti ya serikali, nimemsikia akisema wazi wazi, kura yangu ya urais ni kwa JK, akasema japo anamkubali sana Dr. Slaa, lakini anaogopo kuipoteza kura yake kwa mtu ambaye hatashinda, hivyo urais ni kwa JK ila mbunge wao ni Mrema tuu! cha ajabu, akasema diwani ni wa Chadema!.
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mrema Lyatonga atachaguliwa kwa sababu kubwa; wapiga kura wengi nchi hii ni wazee, tena wale wale wa miaka yote. Akiingia bungeni hataweza kuichachafya serikali, na sitashangaa kuwa hatapewa post yeyote katika kambi ya upinzani. Anyway, wa-Vunjo wanastahili kumuenzi huyu mzee wao 'aliyewatangaza' miaka ya nyuma. Kwa kweli Mrema ana hali mbaya kiuchumi na kiafya, hivyo angalau apewe tu hilo jimbo limsaidie kupata vijisenti vya kumkimu, la sivyo atatia huruma.

  On the other hand, huyu mzee alionekana kama shujaa wa upinzani Tanzania, lakini hali halisi imemfanya aukane upinzani walau apate vijisenti vichache vya kuendeshea kampeni zake kutoka kwa JK...
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280

  Ndo kusema yale ytaliyotokea kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Dodoma ndo yanatimia hapa...
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  I am watching!!...still watching|!
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Stop just watching and start acting...
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  how fit is he mentally. I mean Lyatonga!
   
 16. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ANGALIZO
  Kwenye Nyekundu hapo ...Hii barabara ya Moshi to Himo Pale njia panda ndio himo to Tanga sio Dar marekebisho kidogo. Asante kwa Info. Mimi ni Nimeoa Hapo Uchira
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kazi ipo Lyatonga nae yumo
   
 18. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kampeni za bwana mrema pale vunjo zinafadhiliwa na aliyekuwa mbunge bwana kimaro ili kumkomesha mwenyekiti wa ccm mkoa mama swai.
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280

  yeah kind of read this saga kwenye raia mwema, inaonekana kuna beef kali kati ya mama swai na kimaro......mama swai anatuhumiwa kuwa yeye ndiye anayeamua nani agombeeubunge kupitia CCM, of course it is ridiculous kumchagua Salakana aliyekuwa no 3 kwenye kura za maoini Moshi Mjini awe ndo mgombea..
   
 20. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... niwakumbushe pia kwamba kuna jamaa toka Vunjo ambao kila awamu ya uchaguzi wamekuwa vinara wa ku-organize mikutano ya kuchangisha mamilioni ili kuwangoa UPINZANI huko Vunjo kwenyewe. Kina Kida, Kilewo, Marealle na wengine wengi tu! Mamilioni yanayokusanywa hupelekwa kule kwa CCM Moshi - sina uhakika Vunjo kwenyewe au Mkoani.
  Michango hii hukusanywa na Wanavunjo wa Dar es Salaam. Mwaka 2000 zilipatikana milioni 200 na ushee. Nilichoshuhudia mie ni kwamba hawa jamaa hutoa hiyo MIPESA ili kujikomba kwa CCM (kitaifa) na sio mengine. Hata kama tayari wanazo, ukweli unabaki pale pale kuhusu KUGANGA njaa na kutafuta UMAARUFU, cheaply at that, in total DISREGARD ya interests za jamaa zao huko VUNJO.
  Analofanya MREMA sio tofauti na haya nloandika. Bahati mbaya, VUNJO imechoka kinoma. Hoi mno, wamebaki na tai zao! Si unamwona Mvunjo yule ambaye ni kamanda wa vijana Moshi. Style ile ile ya kujikomba. Watavuna laana tu. suluhu yao waache hayo na wamchague atakayewavusha kweli. Ni Chadema na Sera zake.
   
Loading...