CCM kumtosa Sitta? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kumtosa Sitta?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Mar 14, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  na Mwandishi Wetu

  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, ni mmoja wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye wakati mgumu katika harakati za kurejea bungeni, kutokana na mashambulizi yanayoelekezwa kwake kutoka ndani na nje ya CCM, Tanzania Daima Jumapili imebaini.

  Kwa takriban wiki mbili hivi sasa, Sitta amekabiliwa na upinzani mkali ambao wachambuzi wanadai ni jitihada za washindani wake kuzima tambo zake na dhamira yake ya kurejea bungeni au katika uspika, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

  Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata kutoka kwa makada wa CCM zinadai kuwa kiongozi huyo wa Bunge anaweza kutoswa katika mapendekezo ya chama chake kuwania nafasi hiyo kwa sababu ya msimamo wake wa kupambana na ufisadi, ambao nusura uiangushe serikali.

  Sitta anadaiwa kuwa amekuwa akishabikia mijadala ambayo ilikuwa ikizidisha chuki na makundi ndani ya CCM pamoja na kuruhusu serikali inayoongozwa na chama chake ishambuliwe na wapinzani pamoja na makada wenzake.

  Wakati kiongozi huyo akionekana kupata kukabiliana na upinzani ndani ya chama chake, limezuka kundi la viongozi wa upinzani likimshambulia Sitta kwa kubainisha kuwa hawezi kupambana na ufisadi.

  Juzi Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema Spika Sitta hawezi kuwa mpambanaji wa ufisadi wakati rekodi yake inaonyesha kuwa ni miongoni mwa kundi hilo ambalo limesababisha nchi kuwa maskini na maisha ya watu kuwa magumu kadiri siku zinavyosonga mbele.

  Mbatia alimtaka Sitta aondoke CCM kama anataka kupambana na ufisadi, vinginevyo watu wataanza kuamini tuhuma mbalimbali zinazohusishwa na Sitta, kama vile madai ya yeye kuhusishwa na uchotaji wa kiasi cha shilingi milioni 200 na kuzipeleka katika Jimbo lake la Urambo Mashariki, pamoja na kukubali kupangishiwa nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa mwezi.

  Kabla ya kuibuka kwa Mbatia, Mwenyekiti wa TLP, Agustine Mrema, naye alishamshutumu Spika Sitta kuwa hana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi kwa kuendelea kubakia ndani ya CCM.

  Hata hivyo shutuma hizo za Mrema zilijibiwa na Sitta, akisema Mrema amefilisika kisiasa na kifedha, na kwamba anapewa pesa kuipigia debe CCM, hasa Rais Jakaya Kikwete.

  Baadhi ya wachunguzi wa masuala ya siasa waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wamebainisha kuwa Sitta ataandamwa na kila aina ya tuhuma katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

  Walibainisha kuwa tabia hiyo ya kuanza kuzushiwa baadhi ya mambo iliyoanza kuibuka hivi sasa, ni sawa na ile ya mwaka 2005, ambapo makundi yaliyokuwa yakiwaunga mkono wagombea wa nafasi ya urais ndani ya CCM walikuwa wakiitumia dhidi ya wapinzani wao.

  Wameweka wazi kuwa mwaka huu nafasi za ubunge zitakuwa na upinzani mkali, hasa baada ya kutokea kwa kashfa mbalimbali zilizowahusisha wabunge na mawaziri ambao wengine wameshang'oka madarakani.

  Sababu kubwa waliyoielezea ni kuwa makundi ndani ya CCM yamejengeana chuki, licha ya juhudi mbalimbali za kuwasuluhisha kuendelea kila kukicha.

  Sitta amekuwa miongoni mwa vigogo wa CCM wanaosemekana kuwa na kundi kubwa la makada wanaotaka baadhi ya wanachama wenzao wang'olewe ndani ya chama kwa madai ya kushiriki katika vitendo vya ufisadi.

  Mara kadhaa kumekuwepo na taarifa za kuandaliwa kwa mikakati kabambe ya kumng'oa Sittta madarakani, likiwemo jaribio la baadhi ya wajumbe katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) uliofanyika mwaka jana kupendekeza anyang'anywe kadi ya uanachama.

  Taarifa za kiongozi huyo kutaka kuvuliwa unachama kwenye NEC, zilithibitishwa na yeye mwenyewe (Sitta) hivi karibuni alipokuwa akitoa risala kwenye harambee ya kidini, ambapo aliweka wazi kuwa ukweli wake wa kuwaumbua mafisadi ulihatarisha uanachama wake.

  Aidha Sitta, mara kadhaa amenukuliwa na vyombo vya habari akiwalalamikia baadhi ya makada wenzake kwa kutembeza fedha na kuwafadhili wapinzani wake jimboni kwake kwa lengo kutaka wananchi wasimchague.

  Zipo taarifa kuwa moja ya makundi ya CCM linahusishwa na jitihada za kumng'oa Sitta bungeni, na linatumia nguvu zote, wakiwamo ‘mamluki' kummaliza kisiasa.

  Swali kubwa linaloonekana kuwaumiza vichwa wachambuzi wa masuala ya siasa, ni kama Sitta ataweza kurejea katika kiti chake, hasa baada ya kutamba bungeni kwamba ana uhakika wa kukalia kiti hicho baada ya uchaguzi wa mwaka huu.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhh......
  how low can they go?????????
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndiyo CCM inayoongoza taifa la Tanzania lenye raslimali nyingi sana lakini ni maskini kuliko Rwanda iliyowahi kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya nusu ya muda wote wa uhuru wao. Bado watanzania tunaamini kuwa siku moja tutadondokewa na maendeleo kutoka kwa wafadhili chini ya uongozi wa hii CCM kama ambavyo waisraeli walivyodondoshewa manna kutoka mbinguni chini ya uongozi wa nabii Musa.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  blah... blah... blahaaaa.. blaaaaaablablablaaaaahhh!!! As usual, Magazeti yameshindwa ku-focus mambo yanayohusu watanzania, yameishia kuspeculate na kuandika hekaya mbaya kuliko za abuniwasi
  tulisikia richmond
  mpasuko
  mtaguso
  mmomonyoko
  ukware nk.

  Waandhishi please... change your style and change your focus, mnadumaza tu tathnia ya habari sasa!!!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  jipya ni lipi hapa?is this supposed to be newz? mi naona kama ni recap flani hivi au maoni ya mwandishi. au?
   
 6. I

  IMBOMBONGAFU Senior Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pumba tu,Tumeyasikia hayo uku Kyela lakini naona hayajafanya kazi...pumbaaaaaaaaaaaaaaaa.....sita
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndio nchi yetu hiyo... mhariri anaruhusu upuuzi kama huo umalize wino na kuweka gazeti mitaani!!! sijui hata mwenye gazeti anajisikiaje kuona gazeti lake limejaa shombo namna ile
   
 8. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,028
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Maana ya neno hilo ni MKUTANO, sijui wewe hapo umelitumiaje. Plz lete ufafanuzi mujarabu
   
 9. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hata mimi nashangaa. sioni kitu
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hawawezi kumtosa coz wakifanya hivyo itakula kwao...CCM sio wajinga kiasi hicho,wanajua upepo wa kisiasa na wanajua jinsi ya kusoma alama za nyakati wameshajifunza kutokana na makosa yao ya nyuma.
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu kama hicho hivyo kuna umuhimu wa Watanzania kuanza kujua kuwa ni lazima kuchagua wabunge wengi wa Upinzani ili kufanya na kufuta dhana ya CCM
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kama unakumbuka vizuri palikuwepo na ule wa butiama, tukategemea kila kitu we ended up seeing photos of NEC members wakila sambusa...

  Then Dododma, we ended up seeing Lowassa kusimikwa kama "mwanaume haswaa"

  Need i say more?
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hii ndio serikali ya CCM inayosubiri mvua ya maendeleo inyeshe toka kwa wafadhili na wahsani wa Magharibi! Kikubwa walichokifanya kwa miaka 5 iliyopita ni ku distract wale wenye mapenzi mema na nchi hii, kuwanyamazisha kwa gharama yeyote na kuombaomba sana while kile wanachokifanya hakionekani!
   
 14. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Kuna nini kwa wahariri wa habari kuzifanyia editing taarifa za zamani kuwa news? It's doubious!! Change U're attitude p/se.
   
 15. I

  Irizar JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CCM hawawezi kumtosa nani hapo ana ubavu wa kumtosa mtu, weeeeee wizziiiiiiii mtupuuuuuuuuuuu
   
Loading...