Kushirikiana na Mhalifu ni Sawa na Kuwa Mhalifu

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,564
41,080
Sheria zetu zinatamka wazi kuwa mtu anayesaidia uhalifu kutendeka, ni mhalifu.

Sasa tuna chama ambacho uovu wake dhidi ya wananchi hauelezeki, na kuna watu ama wanakiunga mkono kwa kuwa wanachama wake au hata viongozi wake. Hawa wote, kiuhalisia ndio wanaokifanya chama hiki kiendelee kutekeleza uovu wake.

Wewe unayeiunga mkono CCM maana yake ni mhalifu kama CCM yenyewe. Kwa kuounga mkono CCM kwa namna yoyote ile ujue kuwa:

1) Unashiriki kwenye uporwaji wa rasilimali za Taifa ikiwemo bandari zetu, mbuga zetu za wanyama na misitu yetu.

2) Unashiriki kwenye kugandamizaji haki za raia unaofanywa na CCM na serikali yake, ikiwemo kuwanyang'anya wamasai haki yao ya kuishi kwenye maeneo yao halisia.

3)Unashiriki kuligeuza jeshi la polisi kuwa kikundi cha wahalifu dhidi ya raia kama CCM inavyofanya.

4) Unakuwa mshirika wa wizi unaofanywa na CCM, rejea EPA, Kagoda (Mkapa kabla ya kufa kwame alikiri wizi wa pesa ya umma inavyoibwa na CCM, na kisha kutumika kwenye uchaguzi).

5) Unakuwa mshirikina na mchawi kama ilivyo CCM (rejea uchaguzi wa 2015, mganga wa kienyeji mshirikina alikutana na wajumbe wa Serikali za mitaa usiku saa nne kwenye ukumbi wa jiji la Mwanza akiwa na madawa ya kishirikina, na kisha kuwapa wajumbe hao waliopewa kazi ya kuwanga kwenye vituo vya kupigia kura eti kura za wizi zitakapoletwa, waletaji hawataonekana!! Mjumbe mmojawapo aliyeshiriki kwenye matukio hayo aliwahi kuniomba ushauri wa kiroho maana anaamini alitenda kinyume cha imani yake ya kikristo)

6) Unakuwa umeshiriki kwenye ulaghai na uwongo (CCM huwa wanadanganya wananchi na kusema kuwa wao ni watumishi wa wananchi, wananchi ndio waajiri wao na kuwa daima watawasikiliza. Lakini jaribu kukosoa ndipo utajua walivyo malaghai)

CCM NI
CHAMA CHA MAJIZI (ushahidi upo)

CHAMA CHA WAGANDAMIZAJI WA HAKI (ushahidi upo)

NI CHAMA CHA KISHETANI KINACHOAMINI KATIKA USHIRIKINA (ushahidi upo)

NI CHAMA CHA KUGAWA RASILIMALI KWA WAGENI KWA MALIPO YA RUSHWA (ushahidi upo).

NI CHAMA CHA WALAGHAI NA WAONGO (ushahidi upo)

WITO
Mwananchi jitenge na uovu, jitenge na CCM. Ondokana na chochote cha CCM kinachokufanya kuwa mshirika wa uovu. Tupa kadi zao, tupa bendera zao, tupa kofia na mavazi yao ili kukataa kuwa mshirika wa shetani aliyefungamanishwa na Chama hiki kilichogeuka kuwa kongwa la utumwa, kongwa la ukoloni, kongwa la umaskini na kongwa la unyonge kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom