CCM kuichukia Yanga na kuifanya kuwa moja Ya miradi yake ya kuipatia mapato, wanachama na Wapenzi wameshirikishwa? Na Vipi Wafanyabiashara waovu?

CCM kuichukia Yanga na kuifanya kuwa moja Ya miradi yake ya kuipatia mapato, wanachama na Wapenzi wameshirikishwa? Na Vipi Wafanyabiashara waovu?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,098
Heading Isomeke ..Kuichukua, na siyo kuichukia


Vyanzo vikuu vya mapato vya CCM, kwa kiasi kikubwa, siku zote imekuwa ni uovu na ukosefu wa maadili. Kwa CCM, uovu huipatia mapato makubwa, ila hili la Yanga kuifanya chanzo kimojawapo cha mapato yake, linashamgaza sana.

Siku za nyuma, CCM ilijaribu kuwa na miradi mbalimbali na kampuni, kama ile kamouni ya SUKITA, lakini kwa sababu ndani ya CCM karibia wote ni mafisadi, miradi na kampuni ya SUKITA, haikufika popote..

Kwa kutamua kuwa watanzania ni walevi wa timu za Yanga na Simba, CCM kila mara imetaka kuichukua Yanga kuwa timu yako na kuwa chanzo kimojawapo cha mapato yake, kama ambavyo baadhi ya makada wake, kama Yule wa Singida ameamua kuwa na mradi wa club ya mpita.

CCM kwa kutumia watu wake waliotumbukizwa ndani ya Yanga, imekuwa ikitaka kuitambulisha Yanga kama timu ya CCM, kiasi cha hata kuitaka Yanga kutumia jezi zenye rangi za chama. Baada ya kuona wamekwishafanikiwa kwa kiasi kikubwa, jana wameiambulidha rasmi timu ya Yanga kama mradi wa CCM. SWALI LA KUJIULIZA:

Je wale wanachama wa Yanga wasio wanaCCM watalazimishwa kuwa wanaCCm, watafukuzwa au watabakizwa humu na kuonekana ni mamluki?UOVU NA UKOSEFU WA MAADILI KAMA CHANXO KIXURI CHA MAPATO KWA CCM:

Tunaposema CCM hutegemea uovu kama chanzo kikuu kimojawapo cha mapato, kuna ushahidi mwingi:

1. EPA
Mwishoni mwa mwaka 2008, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, CCM kwa kupitia makada wake na wafanyabiashara waovu, walipora shilingi bilioni 133 toka BOT kufadhili kampeni za uchaguzi. Kwa kulikamilisha hilo, wafanyabiashara hao waovu na makada wa chama, nao walipewa mgao mzuri wa pesa.

UUZWAJI WA MGODI WA DHAHABU
Mwaka 2009, Mkanada James Sinclair aliombwa pesa na kile kilichoitwa Presidential Trust Fund, dola milion 1 kwa ahafi ya kupewa mgodi wa dhahabu wa Buckreef. Mfanyabiashara huyo baada ya kutoa dola milioni 1 alipewa mgodi ambao awali ulikiwa wa Serikali, halafu ukafanyiwa utafiti na kampuni ya Canada ya IAM Gold kwa gharama ya dola milioni 37, kisha mradi kurudishwa Serikalini, halafu akapewa James Sinclair baada ya kutoa dola milioni 1 kugharamia kampeni za uchaguzi za mgombea wa Urais wa CCM. Mfanyabiashara James Sinclair ni mtu asiye na maadili na aliwahi kupatikana na hatia huko kwao na akazuiwa kufanya biashara, lakini mtu kama huyu ni lulu kwa CCM (A businessman has been found guilty of fraudulent trading from an office in Knutsford.

James Sinclair, 54, an employee at North West Surveys Ltd formerly based in Brook Street, was given a six-month suspended sentence at Knutsford Crown Court on Monday.
He was also banned from being a director, liquidator or manager of a company or property for five years).

WAFANYABIASHARA WAOVU NI MTAJI MKUBWA MZURI WA MPATO YA CCM

Kuna mfanyabiashara wa Morogoro wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia, alikuwa anaingiza mafuta ambayo ni tayari, bila ya kodi, yakipitishwa kama malighafi za kutengenezea mafuta, wakati tayari ni mafuta. Hayo yalikuwa yakifanyika huku mamlaka zote zikiwa zinajua, lakini wakamwacha. Ilipofika kipindi cha uchaguzi akaambiwa aichangie CCM kiasi kizuri cha pesa, la sivyo atatakiwa kulipa kodi yote aliyokuwa akiikwepa ambayo wanaijua. Akakubali kuchanga kiasi kikubwa cha pesa, na kosa la ukwepaji kodi ukaishia pale. Lakini pia wapo wafanyabiashara ambao huwa wanalazimishwa kuichangia CCM kwa ahadi kuwa watafikiriwa kwenye kodi au kuoewa upendeleo kwenye tenda za Serikali.

Hivi karibuni, wiki moja kabla a Harambee ya CCM, kuna jamaa, ni miongoni mwa wawekezaji na wafanyabiashara waliopewa mwaliko wa kwenda kuichangia CCM, kwa masikitiko aliniambia kuwa amefuatwa na Roster kuwa anatakiwa kuichangia CCM siyo chini ya bilioni 1 ili shughuli zake za uwekezaji ziende vizuri. Akasema hana namna, inabidi achangie maana la sivyo anahofia hawa bwana watamkomoa kwenye uwekezaji wake.

KWA UJUMLA
CCM wakishajua mfanyabiashara huyu ni mkwepaji wa kodi au mhalifu wa biashara, kwao tayari huo ni mradi mzuri wa chanzi cha mapato.

Kwa hiyo ukitaka kuwajua wafanyabiashara waovu au wasio waadilifu, au wanaosubiria uoendeleo, subiria siku ya kuichangia CCM. Siku za nyuma ilikuwa ikifanyika kwa siri, walikuwa wakifuatwa mmoja mmoja na ama kulewa ahadi za mbalimbali au vitisho, lakini kwa sasa CCM haina hofu tena, imeamua kuwaanika wote hadharani.
 
Back
Top Bottom