CCM kuanzisha makampuni ya biashara

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?
 
hahaa CCM bana wanahangaika kweli..yaani wao wanajua bila hela hawawezi kushinda uchaguzi wowote ule...hahaaa poleni sana CCM
 
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?

Msendekwa, ulishawahi kuona mfugaji wa fisi (ipo hapo shy) anaamua kufuga na mbuzi?

kuna ofisi moja ya kata pale A town, UVchichiem wamesepa na faranga za chama halafu hawajulikani walipo miezi miwili. viongozi wao wanahisi machalii wamesepea CDM. inawezekana vijana wenye damu ya CDM wameamua kumfuata kamanda Millya.
waanzishe tu kampuni na biashara. wenye meno mbona wapo wengi tu!
 
Hivi mali za SUKITA zilienda wapi? Mabanda ya kuku, kiti moto, ushonaji, nk.

Huwa naona magofu ya ghorofa pale Kimara Stover vijana wananiambia ni ya mtu mmoja alikuwa akiitwa Kapinga. Ujenzi wa hilo ghorofa refu kwenda kulia ulisita baada ya SUKITA kisuasua. Nasikia Kapinga ndiye alikiwa akiiongoza SUKITA.
 
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?

Hizo coy zina tija gani kwa mwanchi wa nanjilinji?
 
uhenda wakazitumia hizo kampuni kuibia pesa hazina kwa kuzitupia pesa nyingi za miradi kama kiini macho huku wakizichukua upande wa pili kumbuka kagoda. CCM haina uwezo wa kuendesha mradi wa kuuza maembe leo ghafla wanataka kufungua kampuni.
 
Wanachofanya ni kusafisha pesa chafu walizotuibia.Si siku nyingi zijazo tutazirejesha hela zetu.
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?
 
Hili jambo ni la kuangalia kwa makini sana. Kuruhusu vyama vya siasa vifanye biashara yoyote wanayotaka linaweza kuleta balaa. Tuliona sekeseke la mgomo wa mafuta. Ni lazima itungwe sheria inayotoa mwongozi aina ya uwekezaji unaoruhusiwa na vyama vya siasa. Tusiliache hili kiholela. Wafanyabiashara watateka nchi.
 
Kwani ile kampuni yao(Ikulu) imepatwa na nini? wameona waongeze zingne coz they know hawatakuwa na biashara pale by 2015!!!!!?
 
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?

wezi watupu.
 
Nalikumbuka tangazo lao la
"... SUKITA supermarket. Bingwa wa mabingwa katika biashara ya supermarket jijini Dar es Salaam.
Wakiwa mtaa wa Lumumba, wanatoa huduma nzuri kwa wateja. Na bei zao, zimepangwa ili kukupa unafuu wewe mnunuzi..."
Na bidhaa zao za Shang shang, Flying Pigeon(Basikeli), Butterfly(Cherehani), n.k.
Labda wataifufua!
 
Sidhani kama Tendwa ataruhusu hili,kutakua na conflict of Interest!!!kwa sasa tuu mohammed enterprises anawapa vijipesa basi wanampa kila kitu,misamaha ya kodi na kaiwekaserikali mfukoni!CHAMA CHA SIASA SIO SACCOS!maeneo yaliyokua ya wananchi chini ya ccm wamempa oil com kujenga vituo vya mafuta jee mapato yake yapo wapi?
 
kwa hiyo wanataka waendelee kufanya biashara bila kulipa kodi!kwani vodacom,uhuru,mzalendo,jamba leo,itv,channel 10,star tv,radio uhuru,azam etc haziwatoshi?
 
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?

Hawa ccm hawawezi kufanya biashara yeyote wakati huu kwani walishindwa enzi za SUKITA wakati huo wanapata mikopo ya bure toka NBC sembuse leo!! Leo hii hakuna pesa za bure pengine waanzishe EPA nyingine kwani huyu gavana wa BOT ni kiazi, ameshimndwa kabisa kuthibiti mfumuko wa bei hapa nchini amebakia kutoa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu!!!!
 
mie napita tu. mawazo ya akina kisumo tuliwahi kuyasikia enzi za mzee ruksa. sijui zile kampuni ziliishia wapi? tutasikia mengi mwaka huu.
 
Ili kukabiliana na pesa chafu, CCM inakusudia kuanzisha makampuni au kununua hisa kwenye makampuni ya biashara.
Hii ni kwa mujibu wa Peter Kisumo(mwenyekiti wa baraza la wadhamini).

My take:
Watuambie kwanza nani aliiua SUKITA na kachukuliwa hatua gani?

SUKITA ilijifia yenyewe kwani ilikuwa ni moja ya vichaka vilivyoanzishwa na CCM kuwaibia watanzania
 
Back
Top Bottom