CCM Kuanguka Kwa CHADEMA is not our Party Interest we should Help Them!!

CCM Kuanguka Kwa CHADEMA is not our Party Interest we should Help Them!!

- Ni muda mrefu sasa kumekuwa na mtafaruku mzito ndani ya Chadema ambao umekuwa ukikitafuna sana chama hicho, na pia kuna utabiri mzito sana ulitolewa na Waziri Wassira kwamba Chadema ipo katika siku zake za mwisho. Ninasema hivi kufa kwa Chadema kama dalili zinavyoonyesha sasa hivi sio the best Interest ya chama chetu CCM. Tunahitaji kuwasaidia sana waendelee kuwepo kwa sababu they have proven time and time kwamba ni paper tiger tu, wazuri kwenye makaratasi lakini hawana nguvu yoyote kisiasa.

- Kupitishwa kwa musawada wa Katiba mpya juzi bungeni ni mfano mzito sana ulio hai wa jinsi wasivyo na nguvu kabisa za kisasa za opposed na makelele yao ya kila siku na lile gazeti lao lenye makao makuu yake kwenye Club ya Disco ya Mwenyekiti wao. Ninawaomba sana CCM tunahitaji kuwa makini sana na matatizo ya chama hicho sasa hivi, tutumie nafasi hii kuwasaidia wasiambaratike maana Chadema ikisambaratika tutaanza kufukuzana na adui tusiyemjua, ni bora kushindana na huyu huyu adui tunayemjua, anayelia posho za wabunge ni kubwa na huku anazipokea, anayelia lia kwamba magari ya wabunge ni ya gharama sana na huku anayapokea hayo hayo. Anayelia lia safari za Rais huku wabunge wake wanasafiri kila siku nje kwa visingizo vya kamati za bunge.

- AGAIN KWA WANA-CCM WOTE NI KWAMBA TUNAWAHITAJI SANA CHADEMA HII INAYOONGOZWA NA AKILI NDOGO, MAANA OTHERWISE TUTAKUTANA NA WAPINZANI WENYE AKILI KUBWA WATATUSUMBUA, TUWASAIDIE WASISMBATRATIKE!! ha! ha! ha!

- KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!

LE Mutuz Big Shoow!!

wewe ushukulu baba yako alikuwa waziri lakini leo hii ungekuwa ombaomba DODOMA TU KWA AKILI ZAKO FUPI SHUKULU KWA HILO
 
Ccm hawana chao kimebaki ni chama kama cha kifalme yani kama baba ni kiongozi mkubwa pale basi atataka mkewe,watoto wake,wajukuu,vitukuu,vilembwe ili mradi waendelee kuiba hii inchi.msahau chadema ni chama cha kikombozi,mtu mnafiki kamwe hawezi achwa akitaka kuharibu chama kwa maslahi ya tumbo lake,kama zito anataka hayo mambo basi aende ccm.pili m4c ni chama cha watu walioenda shule na wanaojua kujenga hoja kama hujui hilo chukua kiongozi wako yoyote yule unayemjua mweke na wachadema then utajua utofauti wao ulivyo,tatu huyo wassira unayemzungumza hana jipya kwani huu ni mwaka wa ngapi yupo kwenye madaraka na amefanya nn mpaka asimame kwa watanzania aanze kutuambia alichokifanya.ccm ni chama kilichokosa dira wala wmelekeo.r.i.p kolimba
 
Wewe le Mutuz ni kimbelembele. Wewe si msemaji wa CCM na wala si mwanachama wa CHADEMA kinachokuwasha ni nini pale CHADEMA?
 
Kama miaka 59 ya uhai wa chama hamjaimarika basi hamtaimarika. Ukomavu wa chama huonekana pale viongozi wa chama wanapoweza kufanya maamuzi magumu na mazito ambayo wengi walidhani hayatawezekana. Kwa busara na hekima zao Viongozi wa juu wa CHADEMA wameamua kufanya maamuzi hayo bila kuogopa athari za maamuzi hayo. Siyo nyie MACCM Mwenyeki wenu akatangaza mnalivua gamba kwa kuwafukuza wale wote wanaokichafua chama. Wakamweka kiti moto na kumuuliza hivi wewe ni msafi!? Usafi huo umeanza lini!? Unakumbuka uchafu uliofanya 2005 kwa kuununua urais kwa mabilioni ya shilingi!? Unataka nasi tuanike uchafu wako hadharani!? DHAIFU akagwaya na kuanza kuikimbia kauli yake ya kulivua gamba kwa kuwafukuza mafisadi akina Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo.

Hatujaimarika tunaongoza nchi, Jee, tukiimarika?
 
Nashukuru ila hujasema kwanini mna hofu? na mtaendelea kutawala namna gani wakati umesema unamhofia Zitto?

Hofu yetu kubwa ni hawa wenye akili wakiamuwa kujiunga na vyama vingine vya upinzani au wakiamuwa kuunda chama chao chao upinzani, nna uhakika chama hicho ndiyo kitakuwa cha upinzani wa kikweli na tishio kwa CCM.

Kwa uongozi wa chadema kwa sasa, tunaafuraha kubwa sana. Fikiri mtu kama DJ asimame kulumbana hoja na Handsome Kikwete. Si kama kusimamisha Mlima kilimanjaro ushindane na kichuguu!
 
Wewe Malecela wa bandia,hawa watu wote wameitwa na wamekiri yale yote waliyofanya,si maccm ss kwamba hatuchukui maamuzi,CDM ni mpango wa mungu.Wasira alihusika kumshawishi zito ktk mahotel ili asaliti chama.CCM mmeumia,CDM ni zaidi ya mtu binafsi.MUNGU TUSAIDIE
 
CDM wakiamua kung'oa miti na mizizi yake wanaweza. Sio CCM ambao gamba liliwakwama na halijang'oka hadi leo! Big up CHADEMA.
 
Kwanza unakosea. Kazi iliyoko CHADEMA ni kukiimarisha chama kwa kujali maslahi ya chama na siyo kulinda mtu au kiongozi. Kwa hiyo kile kilichoishinda CCM kiitwacho "lindana" huku CHADEMA hakipo. CHADEMA imara itatokana na maamuzi imara.

M4C idumu!

Idumuu!
 
nakipongeza chama kwa maamuzi ya busara na ndiyo itakayofanya chama kibaki salama hatuktaki unafikihata vitani ukimuona mwenzenu anawageuka kumuua ruksa teena mnampiga risasi nyingi ili kama akipona harudii tena akifa akaadithie kuzimu
 
Akili zako zinakutuma bila hao hakuna CHADEMA? subirini muone kazi itakayofanyika wanafki wote wakishaondoka, mmemsikia mmoja aliyeitabiria CHADEMA itakufa lkn hamjasikia maelfu ya watabiri wanaotabiria kifo cha CCM 2015.

Uko sawa kabisa,hao waliojiudhuru ni watu na wala sio chama kilichojiudhuru.
 
Le Mutuz nimekuwako nikaona Nccr ilivyosambaratishwa, kisha Tlp na baadaye hujuma dhidi ya Cuf hatuhitaji mtabiri. Ushahidi wa mkakati anaofanyiwa Chadema unaonyesha mchawi ni yule yule. Kwa hiyo hapa wa kulaumiwa ni mchawi wa mageuzi anayeua juhudi za kuleta demokrasia kwa kutumia raslimali zetu. Wazalendo wote hatua hii itAwaongezea uchungu na Mori wa vita. I for one navaa kombati niingie kwenye active war!!!!!
 
Wewe Malecela wa bandia,hawa watu wote wameitwa na wamekiri yale yote waliyofanya,si maccm ss kwamba hatuchukui maamuzi,CDM ni mpango wa mungu.Wasira alihusika kumshawishi zito ktk mahotel ili asaliti chama.CCM mmeumia,CDM ni zaidi ya mtu binafsi.MUNGU TUSAIDIE

Alichokosea Wassira ni kuanza kutamba kabla ya mpango kukamilika kuwa ...." Kabla ya mwaka 2015 upinzani nchini utakwishaa"

Mimi kwa maoni yangu naona mtu yeyote anayetaka kurudisha Nchi Hii kwenye upinzani dhaifu Hana nia njema na ustawi wa Taifa letu ....pengine atakuwa anataka CCM iendelee kujisahau....na wanaanchi WAWE hawana wa kuwasemea..especially wenye mawazo mbadala...Hali itakayozaaa upinzani wa KIMYA KIMYA ambao Ndio Mbaya kabisa..

Chadema ni muhimj kwa ustawi wa CCM ...imemsaidia ku shape CCM ...iachwe iendelee kuwepo.....
 
Hofu yetu kubwa ni hawa wenye akili wakiamuwa kujiunga na vyama vingine vya upinzani au wakiamuwa kuunda chama chao chao upinzani, nna uhakika chama hicho ndiyo kitakuwa cha upinzani wa kikweli na tishio kwa CCM.

Kwa uongozi wa chadema kwa sasa, tunaafuraha kubwa sana. Fikiri mtu kama DJ asimame kulumbana hoja na Handsome Kikwete. Si kama kusimamisha Mlima kilimanjaro ushindane na kichuguu!

kwanini uwe na hofu?
 
Kwanza unakosea. Kazi iliyoko CHADEMA ni kukiimarisha chama kwa kujali maslahi ya chama na siyo kulinda mtu au kiongozi. Kwa hiyo kile kilichoishinda CCM kiitwacho "lindana" huku CHADEMA hakipo. CHADEMA imara itatokana na maamuzi imara.

M4C idumu!

Mkuu Arushaone
Haya unayoongea ndio zile akili ndogo tunazozijadili hivi unapotumia neno kulindana unalijua maana yake au ni kukosa maneno muafaka ya kutumia? Zitto amepigwa zengwe muda mrefu sana kwasababu ya kulindana; kama unakumbuka wakati Zitto anatangaza kugombea uenyekiti alipigwa zengwe ili kumlinda Mbowe; alipotangaza nia yake kugombea uraisi alipigwa zengwe ili kumlinda Dr.W.Slaa; 2015 CCM kiulaini kama kusukuma mlevi!
 
Last edited by a moderator:
Hasira za Mkizi...

Waswahili hawana shida ya kumalizia msemo huo.

Ni furaha kubwa sana kwa wale ambao siku zote humu JF tumeshambuliwa kwa kuitwa wadini eti kwa kuwa tu tunaanika ukweli na hatukusita kukemea udini na ukanda wa dhahiri unaooneshwa na viongozi, wanachama, mashabiki, wanazi na bila kuwasahau misukule wa magwanda.

Furaha ilioje kubainika ukweli kuwa chadema ni chama kinachoongozwa kibaguzi. Ubaguzi wa ukabila na udini umejionesha wazi wazi kwa yanayojiri sasa hivi.

Dhambi hiyo ndiyo inawakaanga leo chadema.

Si mimi, waliotangaza kuachia ngazi bila kufukuzwa wamesema hayo.

Poleni sana wale walioipenda chadema kwa dhati na kufikiri kuwa ingewaletea mabadiliko. Leo naona simanzi na huzuni imewashika, hamtaki kuamini ukweli, lakini huo ndio ukweli.

Jee, M2 siyo Mohamedi Mtoi?

...Furaha ya mvuvi.
 
Alichokosea Wassira ni kuanza kutamba kabla ya mpango kukamilika kuwa ...." Kabla ya mwaka 2015 upinzani nchini utakwishaa"

Mimi kwa maoni yangu naona mtu yeyote anayetaka kurudisha Nchi Hii kwenye upinzani dhaifu Hana nia njema na ustawi wa Taifa letu ....pengine atakuwa anataka CCM iendelee kujisahau....na wanaanchi WAWE hawana wa kuwasemea..especially wenye mawazo mbadala...Hali itakayozaaa upinzani wa KIMYA KIMYA ambao Ndio Mbaya kabisa..

Chadema ni muhimj kwa ustawi wa CCM ...imemsaidia ku shape CCM ...iachwe iendelee kuwepo.....

- Naunga mkono hoja hii, jana nilikuwa Serena nikajionea mkutano live sikusikia anything serious ninawashukuru sana Zitto na Kitila, kwa kuwa waangalifu sana kutoibomoa Chadema kwa maneno yasiyo kuwa na tija, walisema maneno ya kawaida sana, halafu ukisoma kwa makini maoni ya wana Chadema huku JF ndio unajionea wafuata upepo, wanafiki na wasiojitambua kabisa kwenye hii ishu mazumbukuku ni wengi sana wasiojua kitu,

- Zitto ni CCM, lakini ameenda Uswiss kutuabisha CCM zaidi, Kitila ni CCM, lakini si ndiye anayewatungiaga hoja za kumdhalilisha Rais wa CCM kama ile ya Mnyika kuwa ni dhaifu, sasa anakuwaje CCM na this kind of politics, Chadema ninaamini kuna matatizo mawili makubwa la kwanza ni Zitto kutaka mahesabu ya chama na pili ni Zitto kuutaka uenyekiti ambayo ni halali yake,

- Chadema kwenye haya matatizo yenu mnajonyesha wazi kwamba hamko serious na mnachokidai toka CCM yaani Demokrasia ya kweli, this is very damaging hasa kwa wafadhili wenu kutoka nje maana hapa mmewahakikishia kwamba ni wajanja wajanja tu lakini sio a serious oppostion party, lakini still ninasema hivi kuvunjika kwenu sio in CCM interest so ninawaomba tena wale wote wahusika ndani ya CCM tuwasaidia hawa ndugu zetu wavuke hiki kipindi kigumu kwao salama bado nasema ni afadhali hawa Chadema adui tunayemjua kuliko adui mpya ambaye hamtumjui.

Le Mutuz
 
Hasira za Mkizi...

Waswahili hawana shida ya kumalizia msemo huo.

Ni furaha kubwa sana kwa wale ambao siku zote humu JF tumeshambuliwa kwa kuitwa wadini eti kwa kuwa tu tunaanika ukweli na hatukusita kukemea udini na ukanda wa dhahiri unaooneshwa na viongozi, wanachama, mashabiki, wanazi na bila kuwasahau misukule wa magwanda.

Furaha ilioje kubainika ukweli kuwa chadema ni chama kinachoongozwa kibaguzi. Ubaguzi wa ukabila na udini umejionesha wazi wazi kwa yanayojiri sasa hivi.

Dhambi hiyo ndiyo inawakaanga leo chadema.

Si mimi, waliotangaza kuachia ngazi bila kufukuzwa wamesema hayo.

Poleni sana wale walioipenda chadema kwa dhati na kufikiri kuwa ingewaletea mabadiliko. Leo naona simanzi na huzuni imewashika, hamtaki kuamini ukweli, lakini huo ndio ukweli.

Jee, M2 siyo Mohamedi Mtoi?

...Furaha ya mvuvi.
Mkuu elezea sera za CCM badala ya kupambana na vyama unavyoviita vya kidini
 
Back
Top Bottom