Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,858
Wayahudi walipokuwa wanamsulubisha Yesu walikuwa wanafurahia sana wakidhani wanamkomoa lakini ukweli ni kwamba walikuwa hawajui walitendalo na ndio maana Yesu kabla hajakata Roho pale msalabani alisema: "Baba wasamehe hawa kwakuwa hawajui walitendalo".
CCM nao,kwa waliyoyafanya Dodoma siku mbili zilizopita kwa kuwasulubu wanachama wao huku wakishangilia wakiamini wanawakomoa, hakika ni wazi nao hawajui walitendalo kama ilivyokuwa kwa Wayahudi na bahati mbaya wao hawawezi kusamehewa mbinguni na duniani maana hakuna wa kuwaombea msamaha.
Hawajui walitendalo kwasababu wanayoyafanya yatakuja kuwagharimu huko mbeleni kama tulivyoona mwaka 2015 baada ya Lowassa na makada wengine kuamua kujitoa katika chama hicho na kutimkia upinzani na matokeo yake leo hii kila mtu ni shahidi.
Nina hakika kiongozi yoyote yule wa CCM au mwana-CCM mwingine yoyoye yule leo hii ukimuuliza ni uchaguzi gani ulikuwa tishio kubwa kwao bila kufikiria mara mbili atakujibu ni Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Dodoma kwa sasa naitazama kama Yerusalem mji aliosulubiwa Yesu Kristo ili kuwakomboa wanadamu kwani wanaosubiliwa Dodoma kwa sasa wanasulubiwa ili watanzania wakombolewa.
Dodoma, Jerusalem ya Tanzania.