CCM, JamiiForums ni watu siyo Mashine!!

CCM, JamiiForums ni watu siyo Mashine!!

Kila wakati CCM wakizidiwa kwenye mijadala humu JF hukimbilia kusema kuwa "CCM haipendwi JF tu lakini mitaani inapendwa"

Niwafahamishe CCM kwamba sisi tunaochangia humu tunaishi mitaani na siyo mashine (Robot) bali ni watu halisi.

Sisi tumo mitaani na wakati mwingine maoni tunayoyatoa ni ya watu wengi walioko "mitaani" CCM inakosema inaungwa mkono!

Kama mnaungwa mkono mitaani na mnapingwa kwenye mitandao ya kijamii, ni kwa nini basi msiruhusu huko mitaani CHADEMA nao wafanye siasa ili ionekane wanavyokataliwa na watu wa mitaani?
Paragraph ya mwisho imebeba ujumbe mzito sana
 
Uliokuwa nao ccm wakiona comment zako wanaangalia kiwiziwizi kama huyu jamaaa gilikipa!View attachment 969801
Ute unanidondoka
downloadfile-6.jpg
 
Sawa, pole ndugu. Set keyboard kuwa kiswahili badala ya English kwenye simu janja(smartphone) yako.
Naona nijaribu kutumia kiswahili kiasi ni nafuu psych
Jaribu kusoma ulichoandika apa,ukiwa umetulia uone kama umeandika kitu kinachoeleweka.
Ni kweli baadhi wameshindwa kuelewa. Teknolojia ni changamoto
 
Haya mambo ya kusema kuwa watu wa JF ndiyo wanasema hali ya maisha ni Ngumu lakini mitaani hali ni shwari, yanakera sana. Kwani sisi watu wa JF hatufanyi manunuzi ama hatuishi kwenye jamii zaidi ya nyie watu wa CCM mlioko JF?
 
Kama mnaungwa mkono mitaani na mnapingwa kwenye mitandao ya kijamii, ni kwa nini basi msiruhusu huko mitaani CHADEMA nao wafanye siasa ili ionekane wanavyokataliwa na watu wa mitaani?

Hapa ndipo penye tatizo Allen.

"----basi ni kwa nini msiruhusu-----"

Kama huko vijijini CHADEMA wanasubiri 'waruhusiwe', watasubiri sana na kusema kweli ndilo kosa kubwa sana wanalolifanya.
Na haitatokea hata siku moja chama chochote kushinda aina 'yoyote ya uchaguzi', hata uwe uchaguzi HURU kabisa, bila ya vyama hivi vya siasa kuwafikia wananchi walioko huko vijijini.

Sote matokeo ya juhudi zao mitaani mijini tumekwishayaona, na hii ni juhudi zilizofanyika huko. Sasa sijui matokeo kama hayo yatapatikana vipi huko vijijini bila ya juhudi kama zile zilizofanyika mitaani! Kuna miujiza gani inayotegemewa huko?

Mh Lissu alizungumzia "Mafuriko", lakini haya pia huhitaji maandalizi maalum ili yapatikane.
Hii dhana ya kufikiri tu kwamba "watu wamechoshwa" na yanayofanywa na waliopo kwenye madaraka haiwezi kuwa ndilo tegemeo la tufani ijitokeze. Tufani inatakiwa itengenezwe na iandaliwe.

Unapoona wakati wa kupiga kura hata asili mia arobaini ya waliojiandikisha hawajitokezi kupiga kura ni lazima uelewe watu wanasema nini. Hii haina maana wanaipenda CCM na viongozi waowaendelee kuwanyanyasa!
 
Kalamu1 hoja yako ina mantiki. Lakini hoja yangu inatokana na mtazamo wa wana CCM wa JF wala si kwa maudhui ya hoja yako ambayo na mimi pia naiunga mkono.

Kwa sasa inafanyika juhudi kubwa sana nchi nzima kujenga mfumo wa CHADEMA ambao utasaidia kuifanya CHADEMA ifanye siasa bila ya kutegemea siasa za mikutano.
 
Kila wakati CCM wakizidiwa kwenye mijadala humu JF hukimbilia kusema kuwa "CCM haipendwi JF tu lakini mitaani inapendwa"

Niwafahamishe CCM kwamba sisi tunaochangia humu tunaishi mitaani na siyo mashine (Robot) bali ni watu halisi.

Sisi tumo mitaani na wakati mwingine maoni tunayoyatoa ni ya watu wengi walioko "mitaani" CCM inakosema inaungwa mkono!

Kama mnaungwa mkono mitaani na mnapingwa kwenye mitandao ya kijamii, ni kwa nini basi msiruhusu huko mitaani CHADEMA nao wafanye siasa ili ionekane wanavyokataliwa na watu wa mitaani?
Ufugaji wa wasiojulikana umedumaza akili zao!
 
Siku DJ makengeza akistaafu ndo tutawaelewa. Vinginevyo huu muda ni wa kuchapa kazi kuanzia level ya mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla. Sio kila time ni za kubishana na viroja vya JF badala ya hoja za msingi za kujenga taifa letu. Ishu ya CDM na UFIPA kwa ujumla kutumika na mabwanyenye kuifanya serikali ya awamu ya tano isitulie ktk kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi hasa wanyonge imeshashtukiwa kitambo sana. Wanasema hata dhahabu hupitia kwenye moto mkali sana ndipo ing'ae. Raisi MAGUFULI endelea kukamatilia hapohapo hadi wakora na manyang'au wasalimu amri
Tumechapa kazi wameiba korosho zetu.afu amenyuti kimya kama hausiki vile .lipeni tuandae mashamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna shida kubwa sana hapa. Kwahiyo hizi ndio hoja zinazoongelewa. Matusi!. Tunasubiri 2020 mtukane ili tuone kama mtashinda uchaguzi. Huo utakuwa ubunifu wa kipekee kutoka Tanzania.
Waoga !mnaogopa hata vikao vya ndani.pamoja na kumiliki taasisi zote usalama+sungusungu +mgambo.pia NEC hata mahakama majaji mnateua.afu eti upinzani unakufa.sio kwa uoga huo.mmebakia kidogo tu kutangaza uchaguzi mwiko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila wakati CCM wakizidiwa kwenye mijadala humu JF hukimbilia kusema kuwa "CCM haipendwi JF tu lakini mitaani inapendwa"

Niwafahamishe CCM kwamba sisi tunaochangia humu tunaishi mitaani na siyo mashine (Robot) bali ni watu halisi.

Sisi tumo mitaani na wakati mwingine maoni tunayoyatoa ni ya watu wengi walioko "mitaani" CCM inakosema inaungwa mkono!

Kama mnaungwa mkono mitaani na mnapingwa kwenye mitandao ya kijamii, ni kwa nini basi msiruhusu huko mitaani CHADEMA nao wafanye siasa ili ionekane wanavyokataliwa na watu wa mitaani?
Maneno ya kawaida tu ata nyie munakimbilia kusema wanalipwa buku 7 wanawasema vibaya wapinzani
 
Back
Top Bottom