CCM itaangushwa kama vilivyoangushwa Vyama vya KANU, MCP na UNIP

Mtazamo wangu juu ya Benard Membe kujiunga upinzani.

Wapo wanaoshangilia na wapo wanaobedha,wapo wasiokuwa na msimamo juu ya Benard Membe Kuhamia Chama cha ACT-Wazalendo.

Jambo moja nataka kuwakumbusha,ni kuwa hakuna popote Afrika ambako Chama cha ukombozi(Chamaa kilichopigania uhuru) kiliangushwa bila kuwatumia makada wa chama hicho.

Nitatoa mifano mitatu tu

1. Chama cha KANU kiliangushwa na Mwai Kibaki mnamo mwaka 2002.

Kibaki alikuwa nani?

Mwai Kibaki ni miongoni mwa Makada waandamizi wa chama cha KANU kilichokuwa kikiongizwa na Jomo Kenyata.

Kibaki mwaka 1963 aligombea Ubunge kupitia Kanu na kushinda uchaguzi.

Kibaki mwaka 1969 aliteuliwa kuwa Waziri wa fedha wa Kenya.

Kibaki mwaka 1978-1988 alikuwa makamu wa Rais wa Serikali ya Kenya iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha KANU.

Kibaki hakufurahia udikteta na ukabila wa Rais Moi.

Kibaki akajiuzuru mwaka 1991.

Mwaka huohuo Kibaki akaanzisha Chama cha Democratic Party (DP)

Wakati Kibaki anaondoka ,Raila Odinga nae akaondoka KANU kuanzisha chama chake.

Kibaki akagombea Urais wa Kenya kwa chama chake cha DP mwaka 1992 akashindwa vibaya.

Kibaki akarudua tena Kugombea uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 1997 kwa chama chake ya DP akashindwa tena.

Kibaki akabadili Mbinu, akaona atafute vyama vingine ili waunganishe nguvu.

Kibaki akaungana na Raila Odinga, Charity Ngilu,Michael Kijana na Wamalwa wakaunda Coalition waliyoita.

NATIONAL RAINBOW COALITION(NARC)

Mgombea akawa Kibaki aliekuwa makamu wa Rais wa KANU kwa miaka 10(1978-1988) .

Uchaguzi wa mwaka 2002 Kibaki akawaongoza wenzake kupambana na Mgombea mpya wa KANU ambae ni Mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya aitwa Uhuru Kenyatta.

Kibaki akashinda uchaguzi kwa asilimia 62% Huku Uhuru akiambulia asilimia 31% tu.

Huo ukawa ndio mwisho wa chama cha KANU nchini Kenya.

Upinzani wenye nguvu ndani ya Kenya uliongozwa na Makada walioiasisi KANU na ndio waliamua kuiangusha KANU baada ya KANU kukiuka misingi ya uanzishwaji wake.

CCM haijakiuka misingi? Makada waliokuwa wa CCM hawawezi kushiriki kuiangusha CCM?

2. ZAMBIA Chama cha ukombozi cha Zambia ni UNIP (United National Independence Party)
Chama kilichoasisiwa na Rais Keneth Kaunda.

Kaunda aliongoza nchi kati ya mwaka 1964 hadi 1991.

Upinzani ukaanza kujitokeza ndani ya chama cha UNIP

Aliekuwa mfadhili na muungaji mkono wa UNIP akiwa ni kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa mashamba kiitwacho ZCTU ndugu Fedrick Chiluba akawa kila akimshauri Kaunda haelewi, Chiluba akakata misaada, na akabadili mwelekeo ZCTU kuiunga Mkono UNIP ya Kaunda.

Chiluba akaanzisha chama.

Chama kiliitwa MMD (Movement for Multparty Democracy)

Mwaka 1991 Chiluba akashinda uchaguzi na kuiongoza nchi ya Zambia, akamfunga Rais Kaunda.

Historia ya Zambia ni ndefu, baada ya Chiluba alikuja Levy Mwanawasa,na baadae Michael Satta.

Wote hao ni wapigania uhuru wa Zambia ambao awali wote walikuwa chama cha UNIP.

Tatizo la viongozi wa Afrika wakishapata madaraka wanadhani watu wengine hawana akili ndio maana makada wanapoona hawathaminiwi wanaanzisha vyama au kujiunga na vyama vingine.

Chiluba alianzisha Chama,lakini Mwanawasa hakuanzisha Chama, yeye alijiunga na chama cha Chiluba yaani MMD akitokea chama tawala mwaka 1990. Lakini kwakuwa alikuwa na mtazamo wa kuikomboa Zambia mwisho alishinda uchaguzi na kuingoza nchi.

3. Malawi na chama cha Ukombozi cha MCP chini ya Rais Kamuzu Banda.
Baada ya Rais Banda kuwa Mungu mtu wa chama cha MCP aliamua kujitangaza kuwa Rais wa Maisha wa Malawi.

Makada walipinga ndani ya chama,waliompinga wakapewa kesi za uchochezi na wengine walifungwa.

Mfano Henry Chipembere aliamua kujiuzuru kama alivyofanya Lazaro Nyarandu baada ya kuona Mwenyekiti wa MCP anavunja misingi ya chama na katiba ya nchi.

Bakili Muluzi yeye alikuwa Mpambe wa Banda na waziri ndani ya serikali ya Rais Kamuzu Banda.

Bakili Muluzi alikuwa Waziri asiekuwa na wizara maalum ndani ya serikali ya Banda. Lakini aliamua kujiuzuru baada ya kuchoshwa na maudhi ya Mwenyekiti wa MCP.

Bakili Muluzi alijiuzuru mwaka 1980 na kuanzisha chama upinzani cha UDF .

Bakili Muluzi alishinda uchaguzi na kuliangusha rasmi chama cha Ukombozi cha MCP akiwa aliwahi kuwa kada na waziri wa serikali ya MCP.

Nani anasema Membe hawezi kuiangusha CCM?

Bila kuwa na makada wanaojua hila na mbinu za CCM basi hiyo CCM itatawala milele.

Ndio maana wanaompinga Membe ukifuatilia ni makada wa CCM,ndio wanaandika makala mbalimbali kufananisha Membe na Lowassa ili Upinzani usimtumie katika mapambano ya 2020

Ujumbe wangu kwa Upinzani, msigawanyike CCM wanahofu kubwa, wanaamua kufanya Propaganda ya kuwa vunja moyo wapinzani.
Acha kukariri ccm sio kama vyama hivyo vingine ambavyo badala ya kuviita vya ukombozi ni vyama vilivyopigania uhuru kisiasa. Vyama vya ukombozi afrika ikiwemo ccm karibu vyote viko madarakani. Vyama hivyo ni pamoja na ccm ya tanzania, frelimo mozambique, mpla angola, zanu pf zimbabwe, swapo namibia na anc cha afrika kusini. Hivi ni vyama vyenye muelekeo wa kijamaa maarifa na malengo ya kuleta maendeleo kwa nchi zao. Vimeongoza vita vya ukombozi au kusaidia vita vya ukombozi kama ilivyofanya ccm. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kujitathmini na kujisahihisa hivyo kuendelea kuungwa mkono
 
Back
Top Bottom