CCM Isaidiwe Kujua Inachoumwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Isaidiwe Kujua Inachoumwa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Albedo, Apr 15, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]Kuna Imani kwamba Kadiri Mtu Unaponyoa Ndevu sana ndipo ndevu na Zenyewe zinaota sana na Ukiendelea Kunyoa sana Ndevu na Zenyewe zinazidi kuota hata kuweka alama Nyeusi isiyopendeza Kidevuni.[/FONT]

  [FONT=&quot]Nilikuwa natafakari dhana hii ya Ndevu kwenye Magamba, kila mtu anafahamu Gamba, hakuna mtu anayependwa kuitwa Gamba (Ila wenzetu CCM kumbe kuna Magamba yaliyokuwa yanaongoza chama na Juzi tumeona yakivuliwa). Nadhani hii dhana ya Kuvua Gamba na kuota Gamba lingine gumu imenza Kujidhihirisha kwa Ndugu zangu CCM (Chama Cha Magamba), na Kinachowasumbua hawa ndugu zangu ni ile hali ya wao kutotambua kwamba Tatizo lao siyo “Muonekano wa Nje” bali ni “Utendaji” katika Vyombo ambavyo wao wana Sauti kubwa. [/FONT]

  [FONT=&quot]Wameteua Consultants ili awaambie nini hasa kilichofanya Chama hicho kuchikiwa sana na Wananchi, wamemlipa pesa nyingi laki Consultant amekuja na Majibu kwamba Mchawi wa CCM ni Lowasa, Chenge, Makamba, Rostam, Chadema na Jamiiforums. Huyu anaitwa eti Consultant aliyelipwa Pesa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kuna Mtu mmoja amesema kwamba hii kazi ya Consultation hata Kingepewa Kichwa Kimoja cha hapa JF (Home of Great Thinkers) kingeweza kuifanya just over a night na kutoa Majibu Mazuri ambayo yangeweza kukisaidia Chama hicho dhidi ya Kifo kilicho dhahiri Mbele yake.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa Kifupi RIPOTI YA CCM CONSULTANT NDIYO IMEKUWA MSUMARI WA MWISHO KATIKA JENEZA LA CCM, CCM ILISHAKUFA NA SASA AMEPATIKANA WA KUGONGA MSUMARI WA MWISHO WATU TUKAZIKE.[/FONT]

  [FONT=&quot]Wanasema JF ni hatari kwa Chama Sababu inatoa habari za Kupotosha. Ina maana hata CCM ambao ni member hapa nao ni Hatari kwa CCM kwamba na wao wanamilikiwa na CDM kupitia JF! Nawashauri CCM wasijaribu kupamba na e-media hata siku moja kifupi ni kwamba HAWAWEZI ila wanachoweza kufanya na wao waanzishe Foruma yao ila wasije wakaikana kama daily news na Forum yao[/FONT]

  [FONT=&quot]Wanasema Rostam ni Hatari kwa Chama. Najiuliza ni Rostam Yupi? Ni Huyu Rostam Azizi aliyenyanyiliwa Mikono na Mwenyekiti wakati wa Kampeni au ni Rostam Yupi? Ni huyu Rostam aliyetajwa na Dr. Slaa halafu CCM yote ikaitisha Press Conference kumtetea au ni Yupi? Ni huyu Rostam mmiliki wa Dowans ambayo Mwanasheria Mkuu, NEC ya CCM, panda na wengine walitaka Ilipwe bilioni 94 haraka au Rostam yupi? Jamani nisaidieni ni huyu Rostam aliyeitwa kwamba ni Jembe na Mwenyekiti au ni yupi?[/FONT]

  [FONT=&quot]Wanasema Chenge ni Hatari. Ni change huyu huyu ambaye ndiye Mkuu wa Maadili ndani ya CCM au ni Chenge yupi? Ni huyu huyu Mzee wa Vijisenti au ni yupi?[/FONT]

  [FONT=&quot]Wanasema Lowasa, Ni Lowasa yupi huyu, ni Edward Ngoyayi Lowasa au ni yupi? Ni huyu huyu Lowasa ambaye Wabunge wa CCM walimchagua kwa Kishindo kuongoza kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge au Yupi?[/FONT]

  [FONT=&quot]Tatizo na CCM siyo Chenge, Siyo Lowasa, Rostam, Chadema wala Siyo JamiiForums ( The Home of Great thinker)[/FONT]

  Tatizo la CCM ni Magamba?
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  We wa wapi? Watu hadi wametafuta Consultant awaambie wanaumwa nini na yeye akaishia kuwaambia eti Tatizo lao ni Magamba
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,201
  Trophy Points: 280
  Wewe umeshatoa gamba au unatembea nalo, CCM LOL!! mijitu mizima kumbe mlikuwa hamjatoa magamba toka utotoni aibu.
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huyo Nadhani Gamba lake limeanza kuota
   
 5. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM inaumwa kweli na iko taabani, imekata tamaa hata kwenda kutafuta tiba kwa babu Loliondo. Inaishia kujivua gamba na kujichubu ngozi ikidai eti ndo tiba ya ugonjwa wake. Nani asubiri moto wa mgonjwa? CCM ndo inasubi kuzikwa tu na kusahaulika kabisa na ikifa hakutakuwa na matanga maana mkosi utaiandama nchi hii iwapo itafanya matanga ya CCM.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Bado Mnachochea Kuni tu?
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Gamba Limekuwa Gamba
   
Loading...