CCM is better than CHADEMA

Wewe acha hizo fikra za kifinyu.
Kunafaida zipi umezipata kuwepo CHADEMA?
Naomba uwe mkweli. na unijibu.

Fikra za kifinyu ndio zipi? Faida za kuwepo CHADEMA ni hizi (na baadhi tu na si kwa faida yangu binafsi tu bali kwa TAIFA zima):
  • Ufisadi haufanyiki bila uoga kama zamani
  • Mikataba si siri tena, watu tuna uwezo wa kuipitia
  • Sheria za kipuuzi zimelazimika kujadiliwa upya (rejea mchakato wa katiba mpya).
Hakuna hata moja kati ya hayo matatu ambayo yangetokea kama si kuwepo kwa CHADEMA hii ya sasa yenye nguvu na viongozi makini wanaowanyima usingizi nyie magamba.

Unalo jingine?
 
Annael mi nimekuelewa vizuri sana, umeona uweke sifa zao hasi na ukatumia kama sifa chanya, wakuu someni tena mkiwa mmetuliza akili, huyu jama ameamua kuwatukana kimtindo magamba!
 
Mimi sio dada ni Mwanaume. Unataka za nini? +255790567234
duh we kweli dada tena dada poa,mtu yeyote anyeshabikia CCM ANA UPUNGUFU WA AKILI,MMESHUHUDIA,HUYO ANNA HATA ALIYEMUITA HILO JINA ALIJUA NI JANGA LA KITAIFA,ETI ANAULIZA ZA NN?HALAFU ANATOA ILI IWEJE,HIZO NI TABIA ZA DADA ZETU ,OOH MI SITAKI,MI SITAKI ,OOH SIJAWAHI KULALA NA MMWANAUME,OOOH NAOGOPA HUKU ANAENDA MPAKA NDANI DUUUUUUUUUUH NI MTAZAMO TU.
 
duh we kweli dada tena dada poa,mtu yeyote anyeshabikia CCM ANA UPUNGUFU WA AKILI,MMESHUHUDIA,HUYO ANNA HATA ALIYEMUITA HILO JINA ALIJUA NI JANGA LA KITAIFA,ETI ANAULIZA ZA NN?HALAFU ANATOA ILI IWEJE,HIZO NI TABIA ZA DADA ZETU ,OOH MI SITAKI,MI SITAKI ,OOH SIJAWAHI KULALA NA MMWANAUME,OOOH NAOGOPA HUKU ANAENDA MPAKA NDANI DUUUUUUUUUUH NI MTAZAMO TU.
Hizo ni fikra zako na usidhani kila mtu atakusaport unacho waza.
Mimi nimechagua CCM na ninaiona ni nzuri na inafaa. Wewe umechagua CHADEMA so sio kwa sababu mimi napenda CCM ukadhani wewe unaakili kuliko mimi hapa tena hapana.
Kila mmoja anamtazamo wake. Wewe unaohuo ulio nao lakini mimi ni huu nilio nao.
Acha kunitukana na kunitolea matusi kuniambia mimi ni mwanamke na hapo juu nimekueleza mimi ni mwanaume wewe unataka shari au kheri?
Samahani mkuu matusi hayatakiwi.
 
Hizo ni fikra zako na usidhani kila mtu atakusaport unacho waza.
Mimi nimechagua CCM na ninaiona ni nzuri na inafaa. Wewe umechagua CHADEMA so sio kwa sababu mimi napenda CCM ukadhani wewe unaakili kuliko mimi hapa tena hapana.
Kila mmoja anamtazamo wake. Wewe unaohuo ulio nao lakini mimi ni huu nilio nao.
Acha kunitukana na kunitolea matusi kuniambia mimi ni mwanamke na hapo juu nimekueleza mimi ni mwanaume wewe unataka shari au kheri?
Samahani mkuu matusi hayatakiwi.

Hawa hutaezana nao ndugu yangu hawa kwao SLAA yao ni matusi hawana hoja na unakuta mtu mmoja wa pale UFIPA ana account kumi kwa hiyo kuwa makini ndugu yangu Annael hawa kiboko yao Mwema pekee yake
 
Aisee hili jukwaa linataka nidhamu, mtu kama huyu kama mnaongea live, unaweza mpa neno, milele akabaki kulitafakari bila kupata majibu!
 
Hawa hutaezana nao ndugu yangu hawa kwao SLAA yao ni matusi hawana hoja na unakuta mtu mmoja wa pale UFIPA ana account kumi kwa hiyo kuwa makini ndugu yangu Annael hawa kiboko yao Mwema pekee yake
Kweli bana kwenye mikutano ya wanatoa matusi makubwa makubwa
eti ee wazalendo. Hivi nyie CHADEMA mnadhani hii nchi yenu pekee?
This is our country.
 
Aisee hili jukwaa linataka nidhamu, mtu kama huyu kama mnaongea live, unaweza mpa neno, milele akabaki kulitafakari bila kupata majibu!
Samahani kidogo. Hivi unadhani maneno matupu huvunja mfupa? au kelele za vyura humzuia ng`ombe kunywa maji?
Mimi naipenda CCM wewe wapenda CHADEMA si kila upendacho wewe wote wapende
La hasha
I LOVE Tanzania I LOVE Africa I LOVE CCM.
 
Hii ni kweli:-
1. Ni chama sikivu
2. Wanajua jinsi ya kutatua matatizo
3. Wameiweka nchi katika hali ya utulivu.
Naunga mukono chalii yangu.
1. Chama sikivu - Kimewasikiliza IMF, WB na Walanguzi. Wameuza viwanda vyote, mabenki yote, migodi yote, ardhi yenye rutuba, na sasa wameanza biashara ya kuuza damu (a.k.a mumiani)
2. Wanajua jinsi ya kutatua matatizo - Kidiplomasia zaidi (a) acha upepo upite (b) Risasi na Mabomu (c)kuhama nchi baada ya kuficha fedha ughaibuni na kuanzisha vita.
3. Wameiweka nchi katika hali ya utulivu - Kwa kudhoofisha uchumi, kuua kiwango cha elimu, huduma duni za afya, kupunguza upatikanaji wa lishe bora (uliona wapi mgonjwa na mwenye njaa akapiga kelele)
Big up mtoa mada.
 
Hii ni kweli:-
1. Ni chama sikivu
2. Wanajua jinsi ya kutatua matatizo
3. Wameiweka nchi katika hali ya utulivu.

Kutatua matatizo kwao ni kuua tu kesi iishe. Ama kweli ni watu wa short Cut kama wewe na umasaburi wako
 
Hoja za kuanzia saa 4 usiku hizi, kichwani full viloba,gongo,wanzuki nk.


Mkuu only83, akili ya kuambiwa changanya na zako. Watu huwa hawamaanishi wanachosema na wanachosema hawamaanishi. Nadhani umemwelewa mtoa mada.
 
AHADI YA 'UWAZIRI MKUU' KWA MWANACHADEMA UTAUA WENGI HADI KUNAKOFKA 2015:
KIFO CHA DAUDI MWANGOSI KULE KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA NI KWAMBA KIJANA KANASA KWENYE MTEGO SI WAKE


Mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, afia msalaba si wake kwa kuchinjwa kinyama kwa kuwa tu moyo wake ulimtuma kutetea kile chenye maslahi kwa taifa dhidi ya maslahi ya CCM wilayani Mufindi.

Mauaji haya wenye ukatili mkubwa na kudhalilisha utu wa Mtanzania kule katika kijiji cha Nyololo wala hayakutokea tu kama ajali bali ukweli wa mambo ni kwamba dhamira hii ilifahamika masaa 48 kabla ya zoezi la CHADEMA kwenda kufungua mashina ya kichama wilayani hapo. Swala kwamba polisi wanafanya maandalizi kwenda kuua Mufindi ni jambo lililoenea kwingi kwa zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Mkoa wa Iringa isipokua undani wa akina nani wanaenda kuuaua na kwa mtindo gani pekee ndicho kilichobakia siri kuu kwa jeshi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa nyeti tulizonazo toka nyuma ya pazia, mhanga Daudi Mwangozi, kilichomuua ni kule kugundulika kuingiwa moyo wa upendo na kuamua kutahadharisha mapema na taarifa nyeti kuokoa MASLAHI YA UMMA mauaji ya kutisha yaliopangwa na nguvu zilizodhamiria kutetea CCM kwa gharama yoyote ile dhidi ya uongozi wa juu CHADEMA walioko mkoani hapo kwa ziara ya kikazi.

Ndugu yetu Mwangosi ambaye alifika mapema katika eneo la kazi pale kijiji cha Nyololo na kuonekana kubadilishana utani na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA, wala hakua hataa na chembe cha taarifa kwamba umati wote uliokusanyika mahali pale majuzi ulikua ni wa kumhudhurisha yeye katika harusi ( harusi nyinginezo katika maisha ni kule kuzaliwa na pili kuoa au kuolewa) yake ya mwisho katika maisha.

Siku zote wakati ukuta, wahenga husema, muda wa Malika Israeli kuchukua roho ya Mwangosi ulipowadia, mwenzetu alimaziza hatua zote za kutendewa haki kikatiba kwa maana ya kwamba ndani ya kitu kipindi cha wastani wa dakika kama 35 hivi kijana mwenzetu alishakutana na (1) polisi waliomnasa kwa kosa ambalo jamii ya Tanzania bado inasubiri kufahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na jeshi lake, (2) akaswekwa rumande ndani ya dakika 5 tangu akamatwe, (3) dakika ya 21 tayari Mkurugenzi wa Mashitaka nchini alikwishaandaa faili yake kule Dar es Salaam na kuirudisha Iringa kwa (4) hakimu Kamuhanda (mdogo wake Seth Kamuhanda wa Ikulu) tayari kwa kutoa hukumu juu ya hatima ya kijana Daudi sawasawa na mapenzi ya makao makuu nchini.

WaTanzania wenzangu, hukumu ya kifo kilopotolewa na Kamanda Kamuhanda kupitia kwenye radio call pale kwenye gari la umma lililokua limeegeshwa pembeni kidogo tu kutoka machinjioni Nyololo, kijana mmoja kati ya vijana watatu wa 'vikosi maalum' nchini waliopelekwa Iringa siku tatu tu kwa shughuli maalum ndiye aliyetekeleza agizo la Kamuhanda tena kwa ufundi wa hali ya juu iliowaduaza hata vijana chipukizi kwenye jeshi la FFU pale Iringa.

Ndio, ukweli wa mambo ni kwamba huyu kijana mwenzetu Daudi Mwangosi kamwe hakunyimwa haki ya kusikilizwa na jeshi makini chini ya mzalendo namba 6 kitaifa kwa viwango vya CCM Chamwino, Saed Mwema, kama katiba inavyoelekeza kwa mtuhumiwa wa kosa lolote lile, bwana huyu hakunyimwa muda wa kuita mwanasheria wake kuja kumtetea dhidi ya hii nguvu kubwa yenye maelekezo moja tu; maslahi ya CCM kwanza, maslahii ya taifa itategemea na hali itakavyoruhusu.

Naam, nasema kwamba si siri kwamba Mwangozi hakunyimwa haki ya kuwaaga marafiki zake hata Ken Simbaya analitambua hilo, hakunyimwaa haki ya kuwaaga wazazi na familia zima kwa maana kwamba mzazi wake wa Magogoni alionekana kumpenda zaidi kitaifa.

Ukweli wa mambo ni kwamba mwenzetu Daudi Mwangosi kimsingi aliruhusiwa na hakimu Kamuhanda kutekeleza mambo mengi sana tu ndani ya kipindi hicho cha dakika 35 isipokua tu ni kwamba ilimezwa na zile za jopo lililokua likimsafirisha toka hapa duniani kwenda ulimwengu mwingine huko ahera.

Hakika baadhi ya chipukizi hawa walionekana wazi kutokuamini macho yao jinsi gani kijana mwenzao Daudi Mwangosi waliomuona chini ya dakika 15 zilizopita akiwa amependeza ajabu na kitendea kazi yake begani (kamera) jinsi gani alivyogeuka rundo tu la nyama mahali pale.

Kwa taarifa tulizo nazo hadi hivi sasa, baadhi ya hawa vijana wanahali mbaya mno kisaikolojia tangu siku waaliporejea mjini Iringa wakitokea kwenye hiyo kazi nyeti Mafinga, mji mdogo nje kidogo ya Iringa lakini yote juu ya yote WaTanzania wengi bado wanaendelea kutanabahi juu ya nini hasa kilichomfikisha huyu mwenzetu mahali hapo.

Sote tunajua kwamba tangu CHADEMA kiamue kwamba utani wa kuwa chama cha uchaguzi au cha msimu ndio basi tena, ni ukweli kwamba viongozi wa CCM hawajakaa wapate kufahamu kitu amani moyoni wala kule kujistarehesha kitu kwa kiburi cha kobe kugoma kutembea pindi aguswapo isipokua mambo ni mchakamchaka ulimi nje afadhali ya siku jana kwao kisiasa nchini.

Katika hali ya kuonyesha hayo mafanikio makubwa na kuendelea kukubalika kwa chama cha upinzani nchini hakika linaonekana kuleta tabasamu na nuru ya maisha iliopotea miaka mingi tangu Mwalimu Nyerere, kiongozi pekee aliyewadekeza sana wananchi wa taifa hili, atutoke.

Licha ya msururu huo mrefu wa mafanikio kwa CHADEMA, mtazamo kwa upande wa pili ni huzuni kuu kuona CDM kuonyesha kukubalika kupindukia kila kukicha tayari kumesababisha songombingo si tu katika kundi la wanasiasa wa kambi ya chama tawala bali pia kwa theluthi ndogo ya wanasiasa chipukizi ndani ya CHADEMA yenyewe ambayo nayo inajitafsiri kuumizwa sana kisiasa na mafanikio haya ya tangu kuzaliwa mtoto 'Movement for Change (M4C)' ambayo kila siku wanaonekana kulipiga chenga kutokushiriki shughuli zake lakini bila mtu yeyote kuhisi utupu wowote wa uhiari wao huu kutokujipanga wazi wazi na jeshi la kisiasa la chama chao ambacho hivi sasa ni lulu kwa zaidi ya 70 % ya wapiga kura nchini.

Naam, ni siri ilio nje kabisa kwa Wana-CHADEMA walio wengi kwamba ni hili hili kundi dogo la baadhi ya wanasiasa chipukizi na wenye kuegemea udini wanaojihisi kwamba wao hawana chao katika mafanikio haya makubwa CHADEMA, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba kiota chao cha kutingishia kiberiti cha udini tayari kilishasambaratishwa na CDM mara baada kuingiza chamani jopo kubwa la wanachama mali zaidi, waaminifu zaidi na mahiri zaidi kwenye michepuo yao ya kitaaluma na kuheshimika sana kijamii, ambao ndio hivi sasa wameamua kuunda umoja na kundi mojawapo kati ya vikundi kibao ndani ya CCM kujaribu kutupa karata yao ya mwisho kabla ya kuinua rasmi mikono yao juu mbele ya nguvu ya umma wa Tanzania.

Kama mtu atakua anadhani kwamba usemi kwamba 'hofu kuu na kiwewe humgeuza hata simba kuwa paka' ulikosewa basi kwa taarifa yako utakua umekosea sana tena ajabu. Mbali na CDM kuonekana kuwa ni tishio la uhakika kuendelea kwa utawala wa CCM kwa zaidi ya miongo 4 hivi sasa, mafanikio yake makubwa ya kufungua utitiri wa matawi kila kona ya dunia, kukubalika zaidi huko na hata kupewa michango mikubwa mikubwa ki-hali na mali ndio kabisaaaa kimeingiza hofu kuu ndani ya CCM vikundi vyake vyote nchini na hata kuamuliwa kufanyika kwa msururu wa vikao ndni na nje ya nchi kutafakari kwa pamoja NINI KIFANYIKE KWA KIWANGO MITHILI YA BIG BANG / AU GAME CHANGER ili kuzuia CHADEMA kukamata dola kiulaini kiasi hiki.

Naam, ni hiyo hiyo hofu kuu na kiwewe cha ajabu kisiasa nchini kufuatia mabadiliko kisiasa kwa kasi mwangwi wa sauti inayofanywa na CHADEMA na washirika wake nchini na kiwewe chake ndio cha kile kilichowasukuma baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu CCM kufanya vikao vya siri kibao na kisha kuamua BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA inayokisubiri chama hiki kwenye sanduku la kura miaka michache ijayo.

Lengo la kumsambaratisha mwili mwandishi huyu ilikua ni KUTIA HOFU UMMA WA TANZANIA kwa kuwa hiyo SILAHA YA HOFU NA KUTOKUJIAMINI ni silaha iliokilea vema CCM kukalia madaraka kwa zaidi ya miongo 4 hivi sasa bila mtu yeyote kupaza sauti juu ya kitu haki lakini kwa programu ya elimu ya uraia inayoendeshwa kote nchini na asasi zisizo za kiserikali na pia CHADEMA tena kwa mafanikio makubwa hadi vijijini, wana-Chimwaga kwa tathmini yao hivi majuzi wakuja kubaini kwamba wananchi, kwa viwango vya juu sana kiminyanyaso wamefikia mahala hawana hofu tena na serikali ya CCM pamoja vyombo vya dola vinavyotumika kiitikadi zaidi.

Lengo la pili lililofanya NEC-CCM alioongoza rais Kikwete kwa notisi ya dharura Majuzi mjini Dodoma kuamua kufanya msururu wa mauaji kila CDM wanakofanyia mkutano wa kisiasa ni kule kutafuta kukishawishi chama hiki cha upinzani kukubali kuingia kwenye laini ya kufanya vurugu ili CCM kiweze kupata urahisi na kisingizio cha kuwadhibiti barabara na zaidi kuwaua baadhi ya viongozi tumainio na wenye msimamo usioyumba kwenye chama hicho.

Itakumbukwa kwamba CDM wamejitahidi sana kukinyima nafasi hiyo CCM hivyo chama tawala kushindwa pakuweza kufaidi kutumia nguvu za dola kwa faida yao kukidhibiti wahasimu wao. Ni kweli kwamba wengi wetu wahatambui jinsi gani silaha hii ya CDM kujichagulia KUTOKUKUMBATIA VURUGU, hata kichokozwe na kuchokonolewa vipi, ilivyochangia sana tena sana kukiimarisha chama hiki na kukidhoofisha maradufu CCM angali anazo na silaha za kivita zilizoagizwa toka Iran na bila kusajiliwa popote. Katika hili la silaha ni faraja kubwa kwamba tayari Jumuia ya Kimataifa inakaribia sana kufanya jambo humo.

Kwa kuahirisha tu taarifa hii juu ya kifo cha Mwangosi kwa msalaba wa wengine, ni muhimu kudokezea tu japo ki
dogo kwamba maandalizi kutekeleza mauaji ya kisiasa kule Mufindi wala ilifanyika kwa hisani ya Mwana-CDM aliyeinya uia kuona viongozi wake wa juu wakiuaua ili ndoto ya ahadi ya Uwaziri Mkuu uweze kutimia kwa uhakika zaidi mnamo 2015.

Kwa taarifa tulizo nazo hata hivi sasa kuna baadhi ya taarifa za chama na nyingine nyingi zikiwa ni za kupika zinaendelea kujadiliwa na kuwekewa mikakati hivi sasa nje. Haya yote ni sehemu ya maandalizi kambambe ikao vha siri vilichofanyikia mjini Dar es Salaam wiki moja Kamanda Lema alipokua Ulaya, baadaye kukafanyika nyingine Dodoma kabla ya kikao cha dharura cha NEC-CCM, na sasa sehemu nyingine ikiendelea kule Adis Abbaba Ethiopia.

Mungu aziweke roho za Ally (Morogoro) na Daudi (Iringa) mahala pema peponi huku tukiendelea kufunga kwa sala kwa ajili ya na wale wengine wengi ambao CCM tayari kinainuia kuwapunja haki ya kuishi na uhuru wa maoni kwa kutetea maslahi binafsi na mabilioni yaliofichwa Uswisi.

Wapenda mabadiliko wote, mapambano mbeeeeele kama tai mpaka CCM na mafisadi wake wote hata wale waliojificha ndani ya vyama vya upinzani wote kung'olewa madarakani kwa nguvu ya kura zetu kwa pamoja.

Hii ni kweli:-
1. Ni chama sikivu
2. Wanajua jinsi ya kutatua matatizo
3. Wameiweka nchi katika hali ya utulivu.
 
Wote wehu na waroho wa madaraka msajili futa ccm na cdm tuanze upya huu ni upuuzi wa simba na yanga
 
  • pia wanajua jinsi ya kula bila kunawa,
  • pia wanajua namna ya kuwatumia polisi.
  • pia wanajua namna ya kuchelewesha mishahara ya polisi
  • pia wanajua kulindana kwa wizi
  • pia wanajua kutoa visingizio visivyo na mashiko
 
Back
Top Bottom