Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa vijijini kupitia kwa Katibu wake Sure Mwasanguti wametoa onyo kali na la mwisho kwa baadhi ya watia Nia wa nafasi ya Udiwani na Ubunge wanaojipitisha katika Kata na Majimbo na kujitangaza na kuomba ushawishi kwa wajumbe kabla ya muda kutangazwa.
Mwasanguti ametoa onyo hili akiwa ukumbi wa Siasa ni kilimo uliopo Manispaa ya Iringa akiwa katika kikao maalumu na wajumbe wa jumuiya ya Wazazi pamoja jumuiya ya Wanawake wa chama hicho kutoka Jimbo la Kalenga na Jimbo la isimani.
Soma Pia: Iringa: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025
"Hata Yesu alihubiri Duniani na Kuzimu ili ujumbe ufike kote hivyo hili ni onyo la mwisho muda bado haujatangazwa waacheni viongozi wafanye kazi msiwape 'Presha' bado hawajamaliza muda wao hapa tuna wabunge wawili tu Williams Lukuvi wa Isimani na Jackson Kiswaga wa Kalenga basi hao wanaojipitisha waambieni tutawafyeka" Alisisitiza Mwasanguti