CCM Ipo Njia Panda - Haina Jinsi zaidi ya kuitumia Kete Ya Dr. Magufuli

Magufuli hawezi kuwa Rais na hafai hata kidogo. Ni mtu mwenye jazba, matusi. Kumbuka alipokuwa waziri wa mifugo na Uvuvi aliwanyang'anya Wafilipino meli yao na baadaye wameshinda kesi na hivyo Taifa hili linadaiwa zaidi ya Tshs.300bn. Hii ni sababu ya majivuno yake akijifanya anajua kila kitu. Pili, mauzo ya nyumba za Serikali yeye ndiye aliyemdanganya Mhe. Mkapa ili wauziane nyumba za Serikali. Mpaka leo suala hili limekuwa na dosari kubwa na nina imani UKAWA ukiingia madarakani kesho yake nyumba zitarudishwa. Hata Chato hawezi kupata tena ubunge na ndiyo tuseme KWAHERI POMBE MAGUFULI.

Kama kile kituo cha mafuta Barabara ya Makongoro alicholazimisha kivunjwe kinyume cha sheria na serikali ikashtakiwa na kushindwa kesi na kuibidi kulipa fidia ya zaidi ya shs 3 Bilioni. Ni ubabe usio na hekima ya kusikiliza wataalamu wanasema nini.
Hasara hiyo na nyingine alizoingizia hasara nchi alipaswa kuadhibiwa sio kusifiwa kwa propaganda zake za kitoto.
 
Hata Yule alibomolewa shell yake mwanza alishinda Kesi na serkali ikamlipa fidia kubwa. So sidhani kama magufuli anafaa kuwa centre half wa TANZANIA
 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekiacha Chama Cha Mapinduzi kikiwa na makovu makubwa yakiongozana na maumivu makali. Kimepigwa ngumi na mateke ya kutosha.

Tumepata taarifa toka sehemu mbalimbali za nchi kwamba UKAWA wamejinyakulia viti lukuki kulinganisha na matokea ya miaka mitano iliyopita. UKAWA kupitia mshirika wake mkuu, CHADEMA, wamefanikiwa kusimamisha wagombea maeneo mengi kuliko ambavyo CHADEMA ilifanya miaka mitano iliyopita. Tumeshuhudia wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa wakipungua sana. Kwa hali inavyoendelea, CCM inasubiri anguko lingine kabla ya uchaguzi Mkuu nalo ni kukataliwa kwa Katiba Pendekezwa!

Hii inaonyesha kwamba upinzani hapa nchini umeimarika na unazidi kuimarika kadri tunavyosogelea uchaguzi mkuu wa mwaka kesho. Kama UKAWA wataendelea kuwa pamoja na kuacha uroho ambao tumekuwa tukiushuhudia miaka kadhaa iliyopita, basi mwakani hali ni ya hatari kwa CCM. Kila kukicha watu wanapata confidence kwamba kumbe CCM inaweza kutoka na kisitokee chochote kama ambavyo waliaminishwa hapo zamani.

Kwa hiyo CCM inabidi ijipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu kama inataka kubaki madarakani. Hali ya sasa ya makundi ndani ya CCM itaendelea kuitafuna hadi inaondoka madarakani na kuitafuna hata kama itakuwa upinzani na matokeo yake tunaweza kushuhudia chama kingine kikongwe hapa Afrika kikipotea kwenye ramani ya vyama kongwe kama ilivyotokea kwa KANU, UNIP, UPC, n.k

Katika hali kama hii ya tishio kubwa kutoka UKAWA, kwa sasa CCM watake wasitake wana turufu moja tu nayo ni Dr. John Pombe Magufuli. Inajulikana kwamba wahafidhina wengi ndani ya serikali wanaiogopa misimamo ya Dr. John Pombe Magufuli lakini kwa hili wataona ni afadhali zimwi likujualo na hivyo wakamsimamisha kuwaokoa. Wanaweza wakaamua Rais asiwe Mwenyekiti wa Chama ili kupunguza nguvu zake ndani ya chama.

Huyu ndiye compromising candidate ndani ya CCM na anauzika kwa Watanzania walio wengi.

Najua watu watakuja na hoja ya uuzaji nyumba za serikali. Waliuziwa watanzania.
Sema waligawiwa watanzania, si kuuziwa.
 
Sema waligawiwa watanzania, si kuuziwa.

Ni moja ya aibu za CCM na Taifa zitakazo tolewa mfano na vizazi vyetu vijavyo hata kuliko EPA,Richmond,Escrow,nk. Ktk nchi zenye kufuata utawala bora na sheria Magufuli na wenzake wangekuwa jela na nyumba zetu zingekwisha rejeshwa Serikalini.

Wakati mwingine huwa namlaumu Mwl. Nyerere kuwapeleka shule jamii za ajabu ajabu kama aina ya Magufuli,Pinda,Ghasia,nk kama ndicho chanzo cha kukwama kwa Tanzania. Watu ambao akili zao zilikuwa bado ni kucheza ngoma,kulogana,kulima jembe la mkono,ghafla wakajikuta ni watawala wa taifa lenye maliasili nyingi ajabu wakati hawana uwezo hata wa kutawala kijiji!
 
I second you mkuu hasa kwa kuporomoka kwa CCM, ila kwa Magufuli ... Hapana, kwake Chato kakung'utwa saba na #teamukawa . Wasiomjua Pombe watamshangilia sana but this dude can't deliver good leadership!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Mwenye maamuzi sahihi na magumu ni Mwakyembe.Maamuzi yake huwa hayapingwi mahakamani kwa mafanikio.
Ni kweli Magufuli anakubalika kuliko viongozi wengi wa CCM.Lakini kwa maoni yangu hafai.
 
Magufuli hawezi kuwa Rais na hafai hata kidogo. Ni mtu mwenye jazba, matusi. Kumbuka alipokuwa waziri wa mifugo na Uvuvi aliwanyang'anya Wafilipino meli yao na baadaye wameshinda kesi na hivyo Taifa hili linadaiwa zaidi ya Tshs.300bn. Hii ni sababu ya majiv2uno yake akijifanya anajua kila kitu. Pili, mauzo ya nyumba za Serikali yeye ndiye aliyemdanganya Mhe. Mkapa ili wauziane nyumba za Serikali. Mpaka leo suala hili limekuwa na dosari kubwa na nina imani UKAWA ukiingia madarakani kesho yake nyumba zitarudishwa. Hata Chato hawezi kupata tena ubunge na ndiyo tuseme KWAHERI POMBE MAGUFULI.

mimi CCM wakimsimamisha mmoja kati ya hawa nawapigia kura. 1 magifuli. 2 Lowassa. Sihitaji kuelezwa kuhusu hawa watu binafsi nafahamu utendaji wao
 
Utakumbuka maneno yangu na wewe! Magufuli ndiye kimbilio la CCM kwa sasa


Porojo nyingi kumbe mwisho wa siku unampigia debe Magufuli aka Political Entrepreneur firs class... Arudishe kwanza Nyumba za Serikali alizojigaia Arejeshe Trillions zetu kweye deals zake za kuwalipa wakandarasi na kuwatimua kimaigaombwe bila ya kazi kufanyika... CCM haina mwingine Zaidi ya Lowassa ambaye mnaogopa kuwa atawalipizia kisasi kwa mabaya yote mliyomtendea...

Maghufuri hawezi kuteuliwa urais, utakumbuka maneno yangu. Hata hivyo si kiongozi bora, hajui atoe maamzi gani wakati gani.

Amesogea manake kuwa ndani ya tano bora si masikhara, kimya kimya anasonga mbele.
 
Kwa hii 5bora weng wanaopenda utendaji kazi najua watasema magufuli ndie...lakini kiuhalisia mfumo uliopo haupendi mtu anadai kua husimamia sheria bali mtu anelinda masrahi kwa mgongo wa sheria...nahisi wameamua kubadili chupa tu mvinyo ni ulele yaani membe
 
Magufuli hawezi kuwa Rais na hafai hata kidogo. Ni mtu mwenye jazba, matusi. Kumbuka alipokuwa waziri wa mifugo na Uvuvi aliwanyang'anya Wafilipino meli yao na baadaye wameshinda kesi na hivyo Taifa hili linadaiwa zaidi ya Tshs.300bn. Hii ni sababu ya majivuno yake akijifanya anajua kila kitu. Pili, mauzo ya nyumba za Serikali yeye ndiye aliyemdanganya Mhe. Mkapa ili wauziane nyumba za Serikali. Mpaka leo suala hili limekuwa na dosari kubwa na nina imani UKAWA ukiingia madarakani kesho yake nyumba zitarudishwa. Hata Chato hawezi kupata tena ubunge na ndiyo tuseme KWAHERI POMBE MAGUFULI.

Kushinda au kushindwa kesi ni udhaifu wa mahakama zenu na si maghufuli. Kwani we hujui hii nchi ni laini kiasi gani hasa unapoongelea kesi?
 
Kwa hii 5bora weng wanaopenda utendaji kazi najua watasema magufuli ndie...lakini kiuhalisia mfumo uliopo haupendi mtu anadai kua husimamia sheria bali mtu anelinda masrahi kwa mgongo wa sheria...nahisi wameamua kubadili chupa tu mvinyo ni ulele yaani membe

Hiyo tano yao sijaona bado .
 
Aliharibu kwa kugawa nyumba Za serikali. Hakuuza aligawa. Kuna maeneo nyumba ya billioni watu waligawiwa kwa millioni 20. Kwa kweli siamini kama atafaa. Pia kwenye samaki ametutia hasara sana. Barabara ya mtwara hadi sasa haijakamilika miaka yote huyo.

Barabara ya Mtwara imeisha, wacheni upotoshaji
 
Back
Top Bottom