CCM inawatakia Ramadhani njema, kila la kheri!

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, naomba kuwatakia Ramadhani Njema wale wote watakaoshiriki ibada hii muhimu!

Nasihi wafanya biashara wote nchini kutopandisha bei ya vitu muhimu hasa vyakula ili kuwezesha wanaofunga kukamilisha hili kwa amani na furaha!

Serikali ihakikishe inasimamia na kudhibiti wanaotaka kuchuma faida kubwa za duniani kwa kupandisha bei ya vyakula badala ya kutumia mwezi huu kuvuna baraka za mwenyezi Mungu kwa kutenda haki!

Wana CCM tuongoze kwa kuwa mfano bora kwa kutenda haki kwenye biashara zetu! Kwakuwa CCM ndio chama tawala, basi sisi tukiongoza kwa kutenda haki nchi yetu itapata baraka kubwa zinazotokana na mwezi huu mtukufu!

NAWATAKIA RAMADHANI NJEMA!

Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Taifa
 
...
Serikali ihakikishe inasimamia *na kudhibiti wanaotaka kuchuma faida kubwa za duniani kwa kupandisha bei ya vyakula badala ya kutumia mwezi huu kuvuna baraka za mwenyezi Mungu kwa kutenda haki!...
Serikali ya chama gani na wewe ni katibu mwenezi wa chama gani? Nilitegemea utawaambia huko huko!
 
asante sana nape. baada ya ramadhani tunaanza kusaka kifaa mnachofuatulia msg na kujitumia kisha kusingizia wapinzani wenu wa kisiasa ili kuwachafua kwa wananchi. Poleni sana.
 
Nape, nasikia ule mtambo wa kutuma sms ni wa Ridhiwani, je ni kweli?
 
huyu jamaa huwa ni jalala kichwa kumaji mtu utamtambua kwa umakini wake

Pole sana dogo naona hata elimu uliyonayo haikusadii
 
Wana CCM tuongoze kwa kuwa mfano bora kwa kutenda haki kwenye biashara zetu! Kwakuwa CCM ndio chama tawala, basi sisi tukiongoza kwa kutenda haki nchi yetu itapata baraka kubwa zinazotokana na mwezi huu mtukufu!
NAWATAKIA RAMADHANI NJEMA!

Ha ha ha,Nape mnawadanganya wanachama wenu wakati nyie mnafisadi nchi hampend wanachama wenu wananchi wa chini wafisadi kwa kupandisha bei ya chakula. ..au nyie ndo mmeandikiwa maisha mazuri tu?
 
waislam walioko ccm wakianza na kina kova, mwema, jakaya, na wengine wangetumia mwezi huu kukiri wanayofanya gizani ingekuwa heri zaidi kuliko kufikiria bei za vyakula tu.
 
Asante! Ujumbe umefika mh. Nape. Lakin watu vichwa ngumu, nenda sokon kuanzia jana vitu vimeanza kupanda bei. Nategemea mtafuatilia kwa vitendo na sio maneno. Halafu angalia hiyo heading yako "CCCM" rekebisha mkuu! Jpili njema kiongozi.
CPA(T)
 
Sababu kubwa ya inflation Tanzania hivi sasa ni economic mismanagement, vinginevyo kipindi cha ramadhan huambatana na a general increase in price levels kutokana na law za demand and supply na hii ni kwa nchi zote, even oil rich countries, sio Tanzania tu ambapo ni kawaida kwa bei za bidhaa za vyakula kuongezeka by 3 to 5 percent during this period. Tofauti na nyakati za kawaida, wakati wa mfungo wa ramadhan familia hununua stock kubwa za vyakula, familia hula chakula kingi zaidi na in a communal sense n.k. Kwahiyo wafanyabiashara wasilaumiwe kwa kupandisha bei katika nyakati hizi kwani hizi ni laws za demand and supply, tatizo linakuja pale ambapo tayari kuna inflation kutokana na mismanagement of the economy na taasisi husika hivyo tusishangane inflation ikaenda way beyond 20% katika kipindi hiki kwani an increase of 3% to 5% is constant na ni kawaida, so kama hii itaongezeka juu ya the current rate of inflation, tusishangae inflation kufikia 22% - 25% katika kipindi hiki.
 
hongera katibu mwenezi.
jipigie makofi kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuliongoza taifa hili kwa haki,kila mtu anapata haki yake,mafisadi wamefukuzwa ndani ya chama na wamepelekwa mahakamani,wapinzani wanaua watu wanawasingizia ninyi.
ukitaka kujua kesho ya mfugaji ngombe angalia banda lake,kwenye banda upo wewe,mwigulu,le mutuz,kinje,rizwani,shigela nk.

EE MUNGU BABA TUNUSURU.
 
Nape Jr usilete utani na mwezi mtukufu..........haya mauaji mnayofanya mnadhani Mwenyezi Mungu hana habari?

Mkuu OKW BOBAN SUNZU avatar yako haisomeki, ebu jaribu hii:

8.JPG
 
Ngoja nitoke kwenye huu uzi ..maana maandiko yanasema heri mtu yule asiyekwenda kwenye shauri la wasio haki wala hakuketi barazani pa wenye mizaha kama nape na CCM yake!
 
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, naomba kuwatakia Ramadhani Njema wale wote watakaoshiriki ibada hii muhimu!

Nasihi wafanya biashara wote nchini kutopandisha bei ya vitu muhimu hasa vyakula ili kuwezesha wanaofunga kukamilisha hili kwa amani na furaha!

Serikali ihakikishe inasimamia na kudhibiti wanaotaka kuchuma faida kubwa za duniani kwa kupandisha bei ya vyakula badala ya kutumia mwezi huu kuvuna baraka za mwenyezi Mungu kwa kutenda haki!

Wana CCM tuongoze kwa kuwa mfano bora kwa kutenda haki kwenye biashara zetu! Kwakuwa CCM ndio chama tawala, basi sisi tukiongoza kwa kutenda haki nchi yetu itapata baraka kubwa zinazotokana na mwezi huu mtukufu!

NAWATAKIA RAMADHANI NJEMA!

Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Taifa

Bwana Nape,
Nadhani unaweza kuwa kiongozi mzuri, lakini uhaharibiwa na huko uliko. Jana nimekusikia ukikanusha na kutetea chama chako CCM kuhusu tuhuma za Mabere Marando. Kwa mtu makini asingelikanusha bila kuwa na uhakika kama anachokisema Marando ni sahihi. Umechukua unazi wako na CCM. Suppose ushahidi usio na mashaka unatolewa kuhusiana na aliyoyasema, jamii ya wasomi/waelewa/wachambuzi wa mambo watakuweka kundi lipi/wapi. suppose unakuwa Rais kesho utakurupuka kutoa kauli bila ushahidi hivyo!! If it were me I will request Marando to provide evidence rather than rushing to acussations against Marando. Nakutakia kazi njema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom