CCM inawakosea sana Watanzania

Man from cuba

JF-Expert Member
May 2, 2021
557
1,365
Chama cha mapinduzi kimezindua chuo chao cha uongozi wiki hii kilichojengwa kwa kushirikiana na vyama rafiki barani Africa kwa ajili ya kuwapika au kuwafunda viongozi watarajiwa wa nyadhifa mbalimbali serikalini.

Kimsingi lengo au dhumuni lolote la kuanzishwa chama chochote cha siasa ni kushika madaraka lakini kwa CCM ilipofikia na ilivyojitanabaisha kama chama dola kukipa kipaumbele chuo hicho na kuacha mambo ya msingi ni matumizi mabaya ya rasilimali za watanzania.

Kuna mtu anaweza kuja na hoja kwamba CCM inatumia fedha zake sio za serikali kitu ambacho kihalisia ni uongo kutokana na nature ya CCM kuwa chama dola kuliko kuwa chama cha siasa pale 90% ya pesa zilizotumika ni kodi za watanzania maskini.

Badala ya kuwaza kuzalisha wanasiasa Hawa wa kutuibia ingekuwa jambo jema kwa CCM kuanzisha angalau chuo cha kilimo ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini hicho chuo kingekuwa msaada mkubwa kwa vijana wetu kuliko hicho chuo cha uongozi. Lakini sishangai na maamuzi ya CCM kwani ni chama ambacho kwao madaraka ni bora kuliko maisha ya mtanzania.

Ifike wakati wananchi tukatae na tuwapinge wanasiasa ambao wao kila wanachokiwaza ni kuongoza badala ya kutuwekea misingi imara kama nchi.

NI MUDA MUAFAKA KWA POLEPOLE KWENDA KWENYE CHUO CHAO NA KUFUNDISHA SHULE YA UONGOZI HUKO
 
Back
Top Bottom