CCM inatumika vizuri kuitangaza CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM inatumika vizuri kuitangaza CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, May 29, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia matamshi ya viongozi mbalimbali wa CCM pamoja na habari za gazeti la uhuru na Mzalendo na kugundua kwamba chama hichi kikongwe cha siasa wamekuwa madalali wazuri wa kukipandisha chati Chadema. Wakati CDM wakijikita kushambulia CCM kama chama kwa hoja zilizo wazi za matumizi mabaya ya fedha za umma, ugumu wa maisha, mapungufu ya mchakato wa kuandika katiba mpya n.k., CCM wamejikita kujadili watu ndani ya CHADEMA hasa Dr.Slaa na Mbowe kwa hoja zisizo na mashiko za ukanda, ukabila, udini n.k. huku wakisahau Watanzania wamefuguka haswa.

  CCM wameendekeza ukiritimba wa fikra za ujima katika dunia ya sasa ambayo ipo katika riadha, baadhi ya viongozi ndani ya CCM wanadhani bado wapo enzi za Mwalimu Nyerere au enzi za mwanzoni mwa miaka ya tisini wakati wa kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. Wamesahau kwamba wakati wa kuwahadaa wananchi umepitwa na wakati, minyororo ya kifikra imeanza kulegea na siku zinavyozidi kwenda ndio CCM kinakosa uhalali wa kuendelea kutawala. Kama CCM wanadhani wataendelea kuhonga wapiga kura wanajidanganya, watanzania wameanza kuapa CCM sio Mama yao. CCM inatumika vizuri kuitangaza CHADEMA hadi vijijini na CHADEMA imewaingia kwelikw
  eli.
   
Loading...