MKONGA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2015
- 667
- 453
Ni vizuri kukubaliana na mm kuwa msema kweli ni mpenzi wa mungu kama asemavyo Mh rais, leo naye Mh Lazaro Nyalandu kawa mpenzi wa mungu kwa kueleza umma wa watanzania namna ambavyo chama hichi kilivyopoteza mwelekeo wake. Hoja kubwa zaidi na niliyoilewa ni pale aliposema, namnukuu. 'Ccm imepoteza dira, na imesahau kazi yake ya kuisimamia serekali na kuishauri. Pia kuikosoa inapo bidii kukoselewa. Hapo haswa ndipo nilopo muelewa zaidi Mh Nyalandu. Nilikumbuka wakati ule wa akina Mh Tumtemeke Sanga na lile kundi la G8 namna walivyo kuwa wanaikosoa serekali kupitia chama chao, nikakumbuka namna serekali ilivyokuwa ina kumbushwa kufanya kazi na akina komredi Kinana na Mh Nape wakati ule wa utawala wa Mh Jakaya, na Kufanya mabadiliko serikalini mara kwa mara ili tu kurekebisha dosari zilizokuwa zinaibuliwa na wana ccm wenyewe iwe bungeni au nje ya bunge.
Kwa maana hiyo hoja yake hiyo Mh Nyalandu ya kuwa Serikali inaingilia kazi za chama, ina mashiko tosha kuweka bayana sababu Yy kuondoka na ni hoja nzito kwa serekali, chama cha mapinduzi, na jamii kwa ujumla. Ni hoja isiyo jibika kirahisi hata kama itatumika propaganda nyingi kuijibu.
Ni vyema sasa Ccm kutambua endapo haitochukuliwa kwa uzito hoja hiyo, ni dhahiri ifikapo 2020 wanaccm wengi wapenda demokrasia wataingia mitini na itakuwa ndilo anguko kubwa kuwahi kutokea kwenye vyama vya siasa vikongwe ktk Afrika, na inawezakana ikawa ndiyo mwanzo wa kufutika Ccm kama vile ilivyokuwa kwa KANU ya kenya. Ni vyema wajitafakari sasa kwa hilo. Mengine kama vile katiba mpya, ukandamizaji wa demokrasia, uhuru wa kutoa maoni, uonevu n.k yalishasemwa sana na wengi na yalikuwapo.
Nampongeza Mh Nyalandu kwa uamuzi wake wa kikatiba aliouchukuwa, pia nampongeza zaidi kwa kuimbia serekali ukweli na wana ccm ukweli ya kuwa wameshindwa kuisimamia serikali ya chama chao, kuingoza, na kuiokosoa. Heko zikufikie popote ulipo komredi Nyalando.