CCM inapoteza mwelekeo na dira yake kama ilivyozoeleka.

MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Ni vizuri kukubaliana na mm kuwa msema kweli ni mpenzi wa mungu kama asemavyo Mh rais, leo naye Mh Lazaro Nyalandu kawa mpenzi wa mungu kwa kueleza umma wa watanzania namna ambavyo chama hichi kilivyopoteza mwelekeo wake. Hoja kubwa zaidi na niliyoilewa ni pale aliposema, namnukuu. 'Ccm imepoteza dira, na imesahau kazi yake ya kuisimamia serekali na kuishauri. Pia kuikosoa inapo bidii kukoselewa. Hapo haswa ndipo nilopo muelewa zaidi Mh Nyalandu. Nilikumbuka wakati ule wa akina Mh Tumtemeke Sanga na lile kundi la G8 namna walivyo kuwa wanaikosoa serekali kupitia chama chao, nikakumbuka namna serekali ilivyokuwa ina kumbushwa kufanya kazi na akina komredi Kinana na Mh Nape wakati ule wa utawala wa Mh Jakaya, na Kufanya mabadiliko serikalini mara kwa mara ili tu kurekebisha dosari zilizokuwa zinaibuliwa na wana ccm wenyewe iwe bungeni au nje ya bunge.
Kwa maana hiyo hoja yake hiyo Mh Nyalandu ya kuwa Serikali inaingilia kazi za chama, ina mashiko tosha kuweka bayana sababu Yy kuondoka na ni hoja nzito kwa serekali, chama cha mapinduzi, na jamii kwa ujumla. Ni hoja isiyo jibika kirahisi hata kama itatumika propaganda nyingi kuijibu.
Ni vyema sasa Ccm kutambua endapo haitochukuliwa kwa uzito hoja hiyo, ni dhahiri ifikapo 2020 wanaccm wengi wapenda demokrasia wataingia mitini na itakuwa ndilo anguko kubwa kuwahi kutokea kwenye vyama vya siasa vikongwe ktk Afrika, na inawezakana ikawa ndiyo mwanzo wa kufutika Ccm kama vile ilivyokuwa kwa KANU ya kenya. Ni vyema wajitafakari sasa kwa hilo. Mengine kama vile katiba mpya, ukandamizaji wa demokrasia, uhuru wa kutoa maoni, uonevu n.k yalishasemwa sana na wengi na yalikuwapo.
Nampongeza Mh Nyalandu kwa uamuzi wake wa kikatiba aliouchukuwa, pia nampongeza zaidi kwa kuimbia serekali ukweli na wana ccm ukweli ya kuwa wameshindwa kuisimamia serikali ya chama chao, kuingoza, na kuiokosoa. Heko zikufikie popote ulipo komredi Nyalando.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,506
2,000
Nchi hii tumeingizwa mkenge, tumepata Rais mbaguzi ambaye Taifa hili hakijawahi kupata tokea tupate Uhuru toka kwa mkoloni!

Inabidi CCM wajitafakari upya ni kwanini wametuingiza kwenye matatizo makubwa kiasi hiki??

Inabidi CCM wachukue hatua kabla mambo hayajazidi kuharibika.....

Halima Mdee aliposema Rais wetu anajiona kila analolisema yeye kuwa ndiyo SHERIA mlimuita mchochezi na mkaagiza vyombo vya dola vimuweke ndani kwa Massa "yenu" 48!

Hivi Leo ndiyo mnarealize kuwa kumbe Halima Mdee alikuwa mkweli by 100%

Nachelea kusema nchi yangu pendwa Tanzania inaelekea shimoni ikiangamia kwa sababi ya mtu mmoja, naye si mwingine bali Baba Jesca!
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Heko zikufikie popote ulipo komredi Nyalando.
.
Ninaamini kabisa hujui hata ulichokiandika. Kauli ya Nyalandu na hata yako kuhusu kupotaza dira kwa CCM iko wapi? Je, ni kazi ya CCM kuisimamia na kuishauri Serikali? (kama kauli ya Nyalandu ulivyonukuu), Katiba ya Jamhuri ndio inasema hivyo?

Halafu MKONGA unazidi kujichanganya wewe pamoja na unaemtetea unaposema kua SERIKALI INAINGILIA SHUGHULI ZA CHAMA. Itawabidi muende shule mjifunze tofauti kati ya chama na serikali, na mahusiono yaliyopo baina ya chama na dola.

Zaidi ya laana na dua zisizo na msingi unazotoa, CCM haijachambuliwa na mtu yeyote hapa, na kwa kifupi tu ni kuwa tangu uchaguzi mkuu uliopita umalizike CCM inazidi kujikusanyia na kujilimbikizia wanachama lukuki.

Kipindi kibaya kabisa katika historia kuwahi kutokea kwa CCM ni mwaka 1995 (bila shaka ulikuwa bado unanyonya, kulingana na fikra zako) ambapo Augustine Mrema aliihama CCM kwa nderemo na matarumbeta, akiambatana na wanachama lukuki. Chama kilibaki uchi, hata hivyo kikafanikuwa kuruka kihunzi cha uchaguzi mkuu.

Mwaka 2015 Chama kilitetereka japo kidogo sana, ambapo Lowassa alikihama chama na kuondoka na wanachama kadhaa, wengine wakiwa ni viongozi. Hata hivyo chama kilipambana na kushinda uchaguzi mkuu na kufanikiwa kujizolea viti vingi vya ubunge na udiwani.

Sasa leo unapojitokeza na kauli za kutetereka kwa CCM inakuwa ni kichekesho. CCM imeanza kujiimarisha toka miaka ya 2013 chini ya uongozi dhabiti. Kuingia uongozini kwa makomredi Kinana, Mangula na Nape kuliibeba CCM na baadhi ya mafisadi wakaanza kujivua magamba wenyewe. Wengine kwa kuogopa kuvuliwa magamba walikikimbia chama. Baada ya uchaguzi mkuu wembe umebaki uleule. Hakuna nafasi kwa fisadi ndani ya CCM.
.
kasi ya Raisi Magufuli imewachanganya mafisadi ndani ya chama. Wengine walijilazimisha kustaafu kabla ya umri, na wengine bado matumbo ni joto. Wapo waliochukuliwa hatua, wengine wakapewa onyo na wengine kuenguliwa kabisa. CCM si ile iliyozoeleka, CCM sasa ni mpya na inaongozwa kwa kanuni na tija.

Propaganda zenu hazima mashiko. Kuliko kukaa mkipayuka bora mkae mfanye kazi kwa manufaa yenu na mjenge chama chenu. Kelele mpigazo haziwasaidee chochote maana ki ukweli CCM inaziti kujijengea mizizi na imani mbele ya jamii. Nyarandu kaondoka kwa sababu maovu yake yamejulikana ndani ya chama, kukimbia kwake ni sababu ya kujihami na uoga tu. Pia Nyarandu alikosa amani ndani ya chama baada ya kuenguliwa katika kinyang'anyiro cha uraisi na hatimae kuenguliwa katika baraza la mawaziri.

Ushauri wangu kwako: Tafakari, na ikilazimu tafuta mwalimu akufundishe mipaka ya madaraka nchini Tanzania kama ilivyoainishwa na katiba. Jifunze kazi za chama, dola na serikali. Zijue tafauti zake na majukumu yake.
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,810

Kenge maji.
 
Milindi

JF-Expert Member
Mar 3, 2009
1,333

Kama sio mukulu kuzuia siasa na kufanya yeye peke yake usingeandika yote… kama sio mnyeti hakuna ambaye angehamia! Jiongeze!

Mwisho hakuna aliyekosoa akabaki salama! Nyalandu be carefully…
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Kama sio mukulu kuzuia siasa na kufanya yeye peke yake usingeandika yote… kama sio mnyeti hakuna ambaye angehamia! Jiongeze!
Mwisho hakuna aliyekosoa akabaki salama! Nyalandu be carefully…
.
Mkuu, siasa hazijakatazwa, kilichopo ni utaratibu wa kuzinatia tu katika kufanya hizo siasa.
Vile vile unamaanisha Nyarandu kahama kwa sababu ya Mnyeti? Tafadhali nyoosha sentensi zako
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
.
Mkuu, siasa hazijakatazwa, kilichopo ni utaratibu wa kuzinatia tu katika kufanya hizo siasa.
Vile vile unamaanisha Nyarandu kahama kwa sababu ya Mnyeti? Tafadhali nyoosha sentensi zako
Kukatazwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni sawa na kukatazwa siasa mkuu, mikutano ile ilikuwa inaimsha serekali pale inapokuwa imelala. Na ilikuwa inaionya pia, iwe ya ccm, iwe ya upinzani. Kwa sasa aliyebakia kufanya siasa ni mkuu peeke yake. Ataweza kuona mapungufu ya serekali yake?
 
KASHOROBAN

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
864
1,000
Mafisadi waondoke tu walitunyonya mno hata kama mtatoa Utetezi gani!
Nyie marofa frm ccm mnashida sana ubońgon kwenu, mtu akitoka ccm kawa fisadi akibaki km akina chenge, mnyeti, ngeleja, mama tibaijuka na ata alouza nyumba za serikal kifisad pia kununua mv dar hao hawana uchafu wowote.

Nadhan endeleen kustawishwa na NEC kwan mnachukiwa sana na watanzania
 
Counsellor Sima

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
480
500
Nyalandu amefanya nini katika Taifa hili la Tanzania, au hamkumbuki alipotolewa uwaziri wa mali asili na utalii, wacha aende pia ni uzalendo kujiuzuru, aache Singida nao wafanye mengine, enzi hizi tutqmpinga muheshimiwa Rais sana kwasababu hataki mambo ya kijinga, anataka watu wafanye kazi, mengine yatakuja tuu na sio unaamka unakuta Tanzania ni tajiri, kumkosoa inafaa hakuna kiongozi hajawah kosolewa, ila Magufuli baba 2020 usifanye hata campaign.
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Mafisadi waondoke tu walitunyonya mno hata kama mtatoa Utetezi gani!
Hivi kwani nn watu wa lumumba; mtu anapo kuwa kwao ni msafi; lakini akihamia chama cha CDM anageuka kuwa fisadi? Kabla ya yy kuhama sikuwahi sikia kashfa yake hata moja. Leo kaondoka mmeanza.
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Nyalandu amefanya nini katika Taifa hili la Tanzania, au hamkumbuki alipotolewa uwaziri wa mali asili na utalii, wacha aende pia ni uzalendo kujiuzuru, aache Singida nao wafanye mengine, enzi hizi tutqmpinga muheshimiwa Rais sana kwasababu hataki mambo ya kijinga, anataka watu wafanye kazi, mengine yatakuja tuu na sio unaamka unakuta Tanzania ni tajiri, kumkosoa inafaa hakuna kiongozi hajawah kosolewa, ila Magufuli baba 2020 usifanye hata campaign.
Yaani ww unaongelea ushabiki; lakini kwa uchambuzi wa sayansi ya siasa, 2020. Hapati kura, na hata kama akitumia polisi kujiweka pale, atashindwa kwa sababu hana watu wanao msapoti.
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Nchi hii tumeingizwa mkenge, tumepata Rais mbaguzi ambaye Taifa hili hakijawahi kupata tokea tupate Uhuru toka kwa mkoloni!

Inabidi CCM wajitafakari upya ni kwanini wametuingiza kwenye matatizo makubwa kiasi hiki??

Inabidi CCM wachukue hatua kabla mambo hayajazidi kuharibika.....

Halima Mdee aliposema Rais wetu anajiona kila analolisema yeye kuwa ndiyo SHERIA mlimuita mchochezi na mkaagiza vyombo vya dola vimuweke ndani kwa Massa "yenu" 48!

Hivi Leo ndiyo mnarealize kuwa kumbe Halima Mdee alikuwa mkweli by 100%

Nachelea kusema nchi yangu pendwa Tanzania inaelekea shimoni ikiangamia kwa sababi ya mtu mmoja, naye si mwingine bali Baba Jesca!
Kweli kabisa mkuu, naunga mkono hoja. Na tukifika 2020 salama bila majeraha makubwa ya kibaguzi na kisiasa, tumshukuru mungu.
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Hivi kwani nn watu wa lumumba; mtu anapo kuwa kwao ni msafi; lakini akihamia chama cha CDM anageuka kuwa fisadi? Kabla ya yy kuhama sikuwahi sikia kashfa yake hata moja. Leo kaondoka mmeanza.
Hahahahaa! ukweli ni kuwa mtu akiwa CCM anaitwa fisadi, akihamia Chadema anaitwa kamanda
 
Milindi

JF-Expert Member
Mar 3, 2009
1,333
2,000
.
Mkuu, siasa hazijakatazwa, kilichopo ni utaratibu wa kuzinatia tu katika kufanya hizo siasa.
Vile vile unamaanisha Nyarandu kahama kwa sababu ya Mnyeti? Tafadhali nyoosha sentensi zako
Dragoon wa kichina au wa Kibongo!!!?????? Nyarandu!!!???? naye Chadema arumeru Jitambue..............
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom