Uchaguzi 2020 CCM inapaswa kukubali hili

Kigongoi kwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
447
440
Kwamba, kwa sasa haiwezi kutawala peke yake, mawazo ya pekee kwa sasa hayana nguvu, Kwamba, upinzani umekua na utaendelea kukua na kwamba kutumia njia za kistaarabu ndio njia pekee ya kuienzi amani ya nchi na kwamba elimu ya wananchi kuhusu upinzani imeongezeka.

Kwamba hoja zinapaswa kujibiwa kwa hoja na wala sio kutumia vyombo vya dola kama alivyowahi kusema kiongozi mmoja wa chama hicho kwamba wanatumia privileges za dola kubaki madarakani.

Na kwamba kuna haja ya kukaa na upinzani na kushauriana njia sahihi za kufanya siasa kwa amani bila kuleta mpasuko wa Kitaifa au kuwa na chuki miongoni mwetu.

Nakumbuka Rais mstaafu Kikwete wakati wa awali wa maandalizi ya katiba ya Jaji Warioba alisema,ni bora kukaa pamoja na kujadili yanayotuhusu tukiwa pamoja, kuliko kutafuta umoja tukiwa tumetofautiana.

Nawasilisha
 
Ok tumekuelewa! Basi basi oktoba 28 itaamua nani anastahili kutawala nchi hi!

Una maono mafupi sana, ndio utaendelea kubaki hapo chini ulipo!! Swala sio kutawala ni kuongoza na ndio point ya mleta mada. Swala ni maelewano, maridhiano, amani, haki na ustawi wa jamii nzima. Kama nchi hatutakiwi kuchagua haki! Haki inapaswa kuwepo bila kujali nani anaisimamia!! Hatutakiwi kuogopa nini kisisemwe! Tunapaswa kushughulika na nini kimesemwa.

Unafahamu zero-sum versus win-win approaches? Nchi hii inamuhitaji kila mmoja wetu kwa nafasi yake katika ustawi wake. Mambo ya kitaifa hatuhitaji kuyabishania, tunapaswa tu kugombea kuyatekeleza!!
 
Upinzani pia ni watanzania, wenye upendo na nchi yao na wana dhamira ya dhati ya kuisogeza mama Tanzania(mbatia) mbele. hakuna chama chenye hatimiliki na nchi hii.
 
Ni sahihi kabisa. Kama wanaipenda nchi tufanye kama US repulican vs democratic. Hakuna njia nyingine mbadala.

Ni kweli walizoea wakiwa wao tu. Lakini sasa they have to accept change is innevitable
 
Tuwafiche Kwa lipi sasa, kwamba mtatutukana tukiwaambia ukweli kwamba, CCM bado ni Chama chenye weledi na mikakati mizuri ya ushindi, na kwamba hata mwaka huu upinzani bado ni wasindikizaji tu na wapiga kelele mitandaoni na Wala hawana Mbinu za ushindi!!!

Nakuhakikishia tena, CCM bado inamiaka mingi ya kuiongoza hii nchi Kwa sababu wapinzani Pindi mnapotaka kuaminika mnaanza kuwatisha wananchi hasa wapiga Kura wazuri walioko vijini wakisikia vitisho Eti kwamba, awekwe kiongozi ambaye hata Mungu mwenyewe awe nyuma Kwanza kwenye maswala ya anmani na kwamba si wa kuachia yeye maswala Yao na kwamba, yeye asubiri hilohilo kwenye Ufalme wake.

Wakati Mungu anatawala duniani na mbinguni,mambo ya vitisho yanasnza kabla hata ya Kampeni zenyewe, basi wanajiamlia kuchagua kilicho Bora na kinachothamini Kwanza Amani na utulivu.

Mwananchi wa kawaida hataki kusikia mandamano yasiyo ya Amani.

Tena hiyo Ndiyo iwe agenda ya kumfurumsha huyo anayemweka Mungu pembeni Ili Hali hata Leo Corona haipo nchini Kwa sababu yeye Mungu Akiwa wa Kwanza kila kitu huwa sawa.
 
Kuna kitu nimeona ndani ya siku kadhaa watu wanaopinga sana humu kuhusu chadema , wamepungua sana . kulikoni au hoja zimeisha , naona watu wakisikiliza tu .

Tundu Antipas Lissu anatumia formula nzuri ya ushawishi , inasema . Watu wasipokuamini wala usighafirike, kwa sababu huitaji watu wakuamini bali unachohitaji kufanya ni kutafuta namna ya kwanini watu waanze kukuamini ..... Yaani kwa hili amelenga mule mule ndani .

Sasa wale wengine wanapata kitu cha wasi wasi , kwani ATTENTION SPAN ya watu imehama na ni lazima wahame . Kwa sababu ya lockdown ya kisiasa kwa wapinzani .

Hebu tujiulize , kwa nini wanaume wanachepuka huku wapo kwenye ndoa? . Huwa wanatafuta kitu cha tofauti . hata katika siasa ni hivyo
 
Kwamba, kwa sasa haiwezi kutawala peke yake, mawazo ya pekee kwa sasa hayana nguvu, Kwamba, upinzani umekua na utaendelea kukua na kwamba kutumia njia za kistaarabu ndio njia pekee ya kuienzi amani ya nchi na kwamba elimu ya wananchi kuhusu upinzani imeongezeka.

Kwamba hoja zinapaswa kujibiwa kwa hoja na wala sio kutumia vyombo vya dola kama alivyowahi kusema kiongozi mmoja wa chama hicho kwamba wanatumia privileges za dola kubaki madarakani.

Na kwamba kuna haja ya kukaa na upinzani na kushauriana njia sahihi za kufanya siasa kwa amani bila kuleta mpasuko wa Kitaifa au kuwa na chuki miongoni mwetu.

Nakumbuka Rais mstaafu Kikwete wakati wa awali wa maandalizi ya katiba ya Jaji Warioba alisema,ni bora kukaa pamoja na kujadili yanayotuhusu tukiwa pamoja, kuliko kutafuta umoja tukiwa tumetofautiana.

Nawasilisha

Point tupu. Nimewahi kusema enzi za ccm kuwa chama pekee zilishapita, maana hiki ni kizazi kingine. Vinginevyo ccm itaendelea kuumiza wasioisujudia
 
Ukimsikia mtu anaongelea kufuta upinzani, ujue ana shida katika akili yake.

Kwa ustaarabu wa Dunia ya leo ni lazima uwe kichaa kufikiria kuwa unaweza kuongoza huku watu wote wakisema NDIYO MZEE. Ukiona mtu ana mawazo hayo, jua huyo hajitambui wala haitambui Dunia.

Wewe ni nani hata kila mmoja akusikilize wewe tu? Kama ni binadamu kama walivyo binadamu wengine ujue utapingwa, utakosolewa na kuna wakati unaweza hata kukejeliwa. Hayo itayapata tu maana hata ungekuwa Rais, Waziri, Mkuu wa majeshi au IGP au hata mkurugenzi wa wasipjulikana, wewe bado ni binadamu tu. Hujabadilika wala kubadilishwa chochote. Uliochopewa ni wajibu tu wa kipindi kifupi.

Kisichobadilika na hakiwezi kubadilika mpaka siku yako ya kwenda kaburini, ni ubinadamu wako tu. Madaraka, uongozi na vyeo, vinakuja na kutoweka.

Usijivunie cheo au madaraka yao bali jivunie ubianadamu wako. Jiulize umekuwa mwanadamu kwa kiwango gani. Ubinadamu wako ndio unaoweza kukufanya uwe kiongozi wa namna gani.

Kiongozi kuwa dikteta, mbaguzi, mbabe au mwerevu, mwenye upendo, mwenye kuthamini utu wa anaowaongoza, hutegemea zaidi kiongozi huyo ubinadamu wake ni wa kiwango gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunahitaji kiongozi bora tu . kwani
Kiongozi bora ni lazima ajue udhaifu wake .... Kila mwanadamu ni working progress..hakuna mwanadamu aliyetimia ... Mungu daima anaendelea kushughulika naye .... Na ndiyo maana ukisoma biblia 2 wakorintho 12:9 ,,, anasema uweza wangu hutimilika katika udhaifu ...
Unaweza ukawa labda hasira inakutesa , wivu, chuki, hofu, sasa ukiwa kiongozi lazima ujue na ukishajua kataa kuishi huko tena.

Kiongozi bora huunganisha watu. Kiongozi bora lazima uwe jasiri. Kiongozi bora lazima uwainue watu , kuonyesha mifano, kusema kweli, kushukuru watu, kujijali afya yako na kuacha urithi (I mean legacy )

Amani ! Amani! Amani! Ndiyo chaguo la Mungu hata yesu akasema ,, amani yangu nawaachieni" .
Tundu lissu namuona hapo , ila tutambue hakuna absolutism katika hii dunia . Tunajitahidi na kubadilishwa na Mungu kila leo .
 
Una maono mafupi sana, ndio utaendelea kubaki hapo chini ulipo!! Swala sio kutawala ni kuongoza na ndio point ya mleta mada. Swala ni maelewano, maridhiano, amani, haki na ustawi wa jamii nzima. Kama nchi hatutakiwi kuchagua haki! Haki inapaswa kuwepo bila kujali nani anaisimamia!! Hatutakiwi kuogopa nini kisisemwe! Tunapaswa kushughulika na nini kimesemwa.

Unafahamu zero-sum versus win-win approaches? Nchi hii inamuhitaji kila mmoja wetu kwa nafasi yake katika ustawi wake. Mambo ya kitaifa hatuhitaji kuyabishania, tunapaswa tu kugombea kuyatekeleza!!
Hili ni changizo bora kabisa katika thread hii na zote za aina hii. Nakubaliana nawe mkuu unaposema HAKI haijarishi nani au chama gani kinaongoza hii nchi yetu na nia ya kweli (spirit of readyness) ya kuikwamua nchi ilipo kusonga mbele katika nyanja zote za maendeleo pasipo ubaguzi wa ukanda bali as Tanzania kwa ujumla wake.
 
Kwamba, kwa sasa haiwezi kutawala peke yake, mawazo ya pekee kwa sasa hayana nguvu, Kwamba, upinzani umekua na utaendelea kukua na kwamba kutumia njia za kistaarabu ndio njia pekee ya kuienzi amani ya nchi na kwamba elimu ya wananchi kuhusu upinzani imeongezeka.

Kwamba hoja zinapaswa kujibiwa kwa hoja na wala sio kutumia vyombo vya dola kama alivyowahi kusema kiongozi mmoja wa chama hicho kwamba wanatumia privileges za dola kubaki madarakani.

Na kwamba kuna haja ya kukaa na upinzani na kushauriana njia sahihi za kufanya siasa kwa amani bila kuleta mpasuko wa Kitaifa au kuwa na chuki miongoni mwetu.

Nakumbuka Rais mstaafu Kikwete wakati wa awali wa maandalizi ya katiba ya Jaji Warioba alisema,ni bora kukaa pamoja na kujadili yanayotuhusu tukiwa pamoja, kuliko kutafuta umoja tukiwa tumetofautiana.

Nawasilisha
Amani yetu imeshikiliwa na wapinzani hichi ni kizazi cha sasa ni dotcom kina exposure. Busara za mbowe na maalimu ndio utulivu wetu
 
Back
Top Bottom