CCM INANUKA! MTAWAELEZA NINI WATANZANIA 2020?

V

VOICE UP

Member
Joined
Oct 13, 2016
Messages
5
Points
20
V

VOICE UP

Member
Joined Oct 13, 2016
5 20
Tundu lissu alishambuliwa kwa risasi 36 na zikampata 16 mchana kweupe eneo linalokaliwa na viongozi wa serikali lenye ulinzi 24/7, akiwa kwenye shughuli za kibunge. Mpaka leo hata mtuhumiwa hatujawahi kumsikia licha ya kuambiwa serikali ina mkono mrefu.

Ben Saanane alitekwa na kutoweshwa, simu yake ilifuatiliwa, baada ya muda vodacom waliuza namba na mpaka sasa inatumiwa na wateja wengine. Serikali haijawahi kutoa majibu mpka leo wala tetesi za washukiwa na ilikataa usaidizi wa kuchunguza matukio hayo kutoka mashirika ya kiupelelezi duniani.

Azory Gwanda alitoweshwa kutoka kwake akiacha watoto wake, wazazi wake na mkewe mjamzito, mpaka leo hii hakuna mshukiwa wala tetesi za watuhumiwa wa uhalifu huo. Huku mawaziri wakiendelea kujichanganya kwa kauli tofauti tofauti, Mara wanaotoweka wanaenda kutafuta maisha mara wanakimbia ugumu wa maisha, mara, alifariki n.k. Kumbuka ni serikali ya awamu ya 5 ya ccm mpya inayojitapa ni serikali ya Kizalendo.

Eng. Lwajabe wa Wizara ya Fedha kitengo cha EU, alitekwa akaachiwa, serikali ipo, akatekwa tena akateswa na kuuawa kikatili. Serikali haijasema chochote.

Unajua ukitokea ujambazi mfululizo huwa kuna makaripio makali kuanzia kwa Mkuu wa polisi mpaka kwa Mkuu wa nchi utasikia tuko imara, na tunawapa taarifa kuwa tutawakamata na tutawamaliza lakini haya mambo naona kimya tu kama vile hakuna kinachoendelea. Mpaka inafikia makada wa chama tawala wanasema haya mambo ni ya kawaida tu.

Roma Mkatoliki alitekwa,akateswa, akaachiwa mpaka leo mtekaji serikali haijambaini.

Abdul Nondo alitekwa akaachiwa, akashtakiwa kuwa alijiteka, akashinda kesi, ikimaanisha kuwa ni kweli alitekwa na mpaka leo serikali haijui alitekwa na nani.

Ney wa Mitego alitekwa na kuachiwa, serikali haijui alitekwa na nani.

Mo alitekwa na kuachiwa, mpaka leo serikali haijui nani alimteka Mo.

Masuala ya kubambikiziwa kesi, masuala ya hojiwa uraia ndio usiseme, yameshamiri kuliko ilivyo kawaida.

Haya yote yanatokea ndani ya Serikali ya CCM MPYA inayojinasibu kuwa ni serikali ya kizalendo, wakati Uzalendo wa kwanza ni kulinda uhai wa raia wako, uhai wa unaowaongoza.

Tuamini lipi kati ya haya mawili?

1. SERIKALI YA CCM MPYA NDIO MUHUSIKA MKUU WA MATUKIO YA UTEKAJI, UTESAJI NA UUAJI? AU

2. SERIKALI YA CCM MPYA HAINA UWEZO WA KIUSALAMA, KIULINZI NA KIUPELELEZI?

HIVI AWAMU YA TANO MTAWAAMBIA NINI WATANZANIA 2020? UTAWASHAWISHI VIPI NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA WATANZANIA WAPENDA HAKI WALIOUMIZWA NA MATUKIO HAYA ILI WAKUPIGIE KURA UENDELEE KUONGOZA NCHI WAKATI UMESHINDWA HATA KUFANYA UCHUNGUZI NA ANGALAU KUWA NA WATUHUMIWA TU WAMATUKIO HAYA?

HAKUNA JIBU BAYA LA SERIKALI KAMA KUSEMA “SIJUI/HATUJUI/NA SISI TUNASHANGAA/ HATA SISI HATUFAHAMU!”
HAIINGII AKILINI! 2020 KAZI SIO NDOGO!

PAMOJA NA HAYO ASANTENI KWA KUILETEA NCHI YA BABA YANGU TAUSI WANNE!

Mungu Ibariki Tanzania ya Mama yangu, Mungu Ibariki Kenya ya Baba Yangu!
 
92Ubuntu

92Ubuntu

Senior Member
Joined
Jan 8, 2014
Messages
179
Points
250
92Ubuntu

92Ubuntu

Senior Member
Joined Jan 8, 2014
179 250
Ni Chung lkn Tam.....
Ngoja wajuaji waje....
Mi ngoja niketi Front line.
 

Forum statistics

Threads 1,326,419
Members 509,499
Posts 32,221,354
Top