Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Kama serikali yetu sikivu ya Rais wetu kipenzi John Pombe Magufuli haitaingilia kati kuzuia "upuuzi" huu unaofanywa na chama cha Mapinduzi chini ya akina Hamfrey Polepole, tutarajie kesho kutatangaziwa kuwa wale wanachama wote wa CCM wanaoumwa na hawana hela ya kutibiwa Muhimbili waende Ofisi za CCM Lumumba dawa na vipimo vya CT Scan vinagawiwa pale bureee.
Tafsiri yake ni kuwa ccm inatengeneza sera zisizotekelezeka ili watu wakose mikopo na kisha itumie tatizo hili kwa vijana wetu kujinufaisha kisiasa, kwamba ili upate mkopo lazima uwe na kadi ya ccm tena uende Lumumba,
Kumbuka ccm hii ndio inayoongoza serikali, yaani ile bodi ya mikopo kwa wanafunzi ipo chini ya serikali ya ccm, iweje ccm hii badala ya kuishauri serikali wanafunzi wapateje mikopo, ati inasema vijana wakapange foleni Lumumba ili kupata mikopo???
Hivi tukisema ccm imekwenda kuchota pesa ya umma kule bodi ya mikopo na kuzihamishia vichochoro vya Lumumba na kisha kutoa mikopo hiyo kwa vijana kwa sharti uwe mwanaccm, Wanaweza kujiteteaje?
Nawahakikishia ccm mnaligawa taifa mchana kweupe, na laana hiii haitawaacha salama... Kama ccm inamsaada huo ipeleke mojakwamoja bodi ya mikopo ili vijana wetu Wakitanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa wakapate mikopo hiyo...
Rais wangu Magufuli ingilia kati hili, ccm wanakuhujumu mchana kweupe!
Na Yericko Nyerere