CCM inajishambulia yenyewe

CCM inajishambulia yenyewe

Joined
Oct 13, 2018
Posts
35
Reaction score
260
Na Thadei Ole Mushi.

Kwa Mara ya Kwanza toka JPM afariki Kiongozi mkubwa wa Upinzani anaenda kuongea. Kwa siku zote hizo wapinzani wamekuwa wakitoa maoni na mawazo binafsi kuhusu mwenendo wa Siasa za nchi. Huenda leo tukapata msimamo wa Chama kikuu Cha upinzani kuhusu Siasa za Sasa na za Mbeleni.

Wakati wote huo wapinzani wakiwa kimya CCM inajishambulia yenyewe.

Niliwahi kusema kuwa CCM haipo sayari nyingine. Magonjwa yaliyoviuua vyama vingine ambayo vina rika sawa nacho yanaweza kukiua CCM pia, narudia tena kama hakitajikinga na magonjwa hayo nacho kitaathirika na hatimaye kufa. Vyama vingi vilivyoanzishwa katika miaka ya 1950 na 60 vilishatimuliwa madarakani Siku nyingine sana, mfano United National Independence Party (UNIP) cha Kaunda, Malawi Congress Party (MCP) na Kenya African National Union, (KANU).

UNIP ya Kenneth Kaunda ilikuwa ya kwanza kuangushwa mwaka 1991 baada ya miaka 27 madarakani, ikafuatiwa na MCP ya Kamuzu Banda mwaka 1994 (miaka 29 madarakani) na kisha mwaka 2002 ikawa zamu ya KANU (miaka 39 madarakani).Baadhi ya vyama vya ukombozi kama Parmehutu cha Rwanda, Mouvement National Congolais (MNC) cha Kongo- Kinshasa vilishafutwa miaka mingi.

Sababu kubwa ilikuwa inaibeba ccm kipindi cha nyuma na haijafa Kama vyama hivyo vingine hapo juu ni heshima aliyokuwa nayo baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere.

Nyerere alikuwa akiheshimika sana na wananchi na hatotokea mtu mwingine akaheshimika kama Nyerere.

Mwalimu Nyerere alikuwa kama baba akisema mustakabali wa jambo fulani uwe hivi hakuna aliyekuwa na uwezo wa kupinga. Hali hii pia ilisaidia chama kutokuonyesha mpasuko. Watu walikuwa wakitofautiana wote wanakimbilia kwa baba wa taifa anawapatanisha au anamkemea mmoja. Mtu wa aina hiyo hayupo tena CCM na hakuna aliyeandaliwa kwa kazi hiyo. Mtu akigombana na mwenzake anakimbilia upinzani kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kuwakalisha na kuwapatanisha. Ni dhahiri familia nyingi husambaratika pindi baba anapofariki kwa malumbano ya watoto.

Nasikiliza mijadala ndani ya Bunge na nje ya Bunge.

Mfano Mh Spika yeye pale Bungeni ni Kama Referee anatakiwa asionyeshe mrengo kwenye Hoja ... Anahotakiwa kukifanya ni ku- Summarize Hoja za wabunge lakini kuanza kutoa mwelekeo wake kabla hata ya Hoja haijaanza kujadiliwa ni kuwa influence wabunge waende kule kule anakotaka. Spika wa Bunge ni Mtu mkubwa Sana nchini atusaidie kuituliza nchi kwa Sasa katika kipindi hiki tulichopigwa na dhoruba. Najua Mzee wangu Spika Ndugai atalifanyia kazi.

Nimemsikiliza pia Mhongo na Prof Assad. Hawa Wana majeraha na UONGOZI uliopita kwa sasa wanataka kurudi ku-justfy kuwa walikuwa sawa. Yes huenda walikuwa sawa lakini hili ni kosa kimkakati kwa Chama ambacho kinatamani kuendelea kuishika Dola na kuiongoza.

Watu Kama Kina Mhongo, Assad na wengineo bado wataibuka wengi Kama Chama hakitachukua hatam ya kuwasimamia viongozi wake. Nilisema Juzi Kati hapa kuwa CCM haijulikani ipo wapi. CCM inatakiwa ikutane mapema sana kwenye kikao cha dharura. Haina Haja ya kufuata kalenda kwa mambo yanayoendelea.

Haya yanayoendelea kwa Sasa ni Hatari Sana kwa CCM yenyewe.

Ole Mushi
0712702602.
 
Wewe na CCM yako wote ni hovyo, shida zote hizi zimeletwa na CCM alafu bado unaleta upuuzi wako hapa, sisi tunaondoa CCM kwnza mengine baadae. Eti hatotokea mtu kama Nyerere wewe una miadi na MUNGU? JINGA kabisa, mawazo ya kizamani sn alifanya nini sasa cha maana ameacha taifa masikini kupita kiasi.
 
Waache kwanza kuweka mwenyekiti na katibu mkuu, maana bado tuna jadiliana huku kambini,kumpa mama,mh panafikirisha sana maana mateke yake ya alfajiri mioyoni yameweka makazi, tuliokuwa wana wa kambo ndani ya nyumba yetu nasi tunataka hewa kidogo na huenda tukawa na mwenyekiti na rais.
 
Ccm habari yake imeisha,walianza na kichwa (jiwe) sasa ni mwendo wa kugawana fito.

Mama leo anatuwakilisha Watanzania Uganda ,kwenye dili la bomba ya mafuta.
 
Ni dhahiri CCM ilishakufa ila ikapata huisho la muda ila kwa bahati mbaya mganga wake hakuwa na maarifa akatumia mabavu, unyang'anyi na mauaji ili CCM isife! Akasahau kwamba kifo ni kanuni ya maumbile, lazima CCM ife, sasa kafa mganga mwenye kifuatacho ni kifo cha kishindo kwa CCM japo ninahisi kama Mama akiuchukua uenyekiti anaweza kuwaongezea uhai hata kama ni miaka 5 au 10 lakini sio 100 tena kama wanavyopenda kujinasibu, la hasha! Vinginevyo, CCM the writing is on the wall!
 
Wakati wote huo wapinzani wakiwa kimya CCM inajishambulia
84806afeb5e20a1dd2374e95b62a5c2b.gif

Hatujakaa kimya tunauangalia mtifuano.
 
Mkuu wewe uko sayari gani.

Kwani CCM kama tunavyoifahamu ipo hai?

Mwendazake alihakikisha CCM imekuwa chombo chake binafsi na iko answerable only to him.

Waliojaribu kureason na Mwendazake walikula sumu, muulize mzee Mangula.

Waliojaribu hata kujitengenezea caucus ndani ya chama, walirekodiwa kijasusi.

Makatibu wakuu wastaafu Kinana na Makamba walichapwa viboko hadharani, sasa wanaviogopa hata vivuli vyao!

Kina nape waliishia kushikiwa bastola.

CCM ya Mwendazake, katibu mkuu alikuwa CUF!

Sasa hivi kuna kasuku anaitwa Pole pole, ndiyo thinker wa chama!

Na sasa hivi CCM haina katibu mkuu wala mwenyekiti, sasa sijuiunaiongelea CCM ipi?
 
Andiko lipo lipo kimhemuko hadi halieleweki! linakigania CCM kisife?

CCM ilipoanza biashara za kuunga mkono juhudi na kuwapa vyeo na kuwaacha wafia chama wakiungua juani, ule ulikuwa mwanzo.

Zikaja business za nileteeni Rashid, in fact na issue za Sukuma gang KM kuwa KMK n.k. wamejiroga wenyewe!

Ngoja tuwaache wafu wazikane!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Ikitokea CCM wanachapana makonde sisi kazi yetu ni kuwanunulia gloves na Mo energy ili wawe na nguvu zaidi za kuchapana kisha tunakaa pembeni kushangilia pambano.

A worthless party this country has ever had
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom