Na Thadei Ole Mushi.
Kwa Mara ya Kwanza toka JPM afariki Kiongozi mkubwa wa Upinzani anaenda kuongea. Kwa siku zote hizo wapinzani wamekuwa wakitoa maoni na mawazo binafsi kuhusu mwenendo wa Siasa za nchi. Huenda leo tukapata msimamo wa Chama kikuu Cha upinzani kuhusu Siasa za Sasa na za Mbeleni.
Wakati wote huo wapinzani wakiwa kimya CCM inajishambulia yenyewe.
Niliwahi kusema kuwa CCM haipo sayari nyingine. Magonjwa yaliyoviuua vyama vingine ambayo vina rika sawa nacho yanaweza kukiua CCM pia, narudia tena kama hakitajikinga na magonjwa hayo nacho kitaathirika na hatimaye kufa. Vyama vingi vilivyoanzishwa katika miaka ya 1950 na 60 vilishatimuliwa madarakani Siku nyingine sana, mfano United National Independence Party (UNIP) cha Kaunda, Malawi Congress Party (MCP) na Kenya African National Union, (KANU). UNIP ya Kenneth Kaunda ilikuwa ya kwanza kuangushwa mwaka 1991 baada ya miaka 27 madarakani, ikafuatiwa na MCP ya Kamuzu Banda mwaka 1994 (miaka 29 madarakani) na kisha mwaka 2002 ikawa zamu ya KANU (miaka 39 madarakani).Baadhi ya vyama vya ukombozi kama Parmehutu cha Rwanda, Mouvement National Congolais (MNC) cha Kongo- Kinshasa vilishafutwa miaka mingi.
Sababu kubwa ilikuwa inaibeba ccm kipindi cha nyuma na haijafa Kama vyama hivyo vingine hapo juu ni heshima aliyokuwa nayo baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere.
Nyerere alikuwa akiheshimika sana na wananchi na hatotokea mtu mwingine akaheshimika kama Nyerere.
Mwalimu Nyerere alikuwa kama baba akisema mustakabali wa jambo fulani uwe hivi hakuna aliyekuwa na uwezo wa kupinga. Hali hii pia ilisaidia chama kutokuonyesha mpasuko. Watu walikuwa wakitofautiana wote wanakimbilia kwa baba wa taifa anawapatanisha au anamkemea mmoja. Mtu wa aina hiyo hayupo tena CCM na hakuna aliyeandaliwa kwa kazi hiyo. Mtu akigombana na mwenzake anakimbilia upinzani kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kuwakalisha na kuwapatanisha. Ni dhahiri familia nyingi husambaratika pindi baba anapofariki kwa malumbano ya watoto.
Nasikiliza mijadala ndani ya Bunge na nje ya Bunge....
Mfano Mh Spika yeye pale Bungeni ni Kama Referee anatakiwa asionyeshe mrengo kwenye Hoja ... Anahotakiwa kukifanya ni ku- Summarize Hoja za wabunge lakini kuanza kutoa mwelekeo wake kabla hata ya Hoja haijaanza kujadiliwa ni kuwa influence wabunge waende kule kule anakotaka. Spika wa Bunge ni Mtu mkubwa Sana nchini atusaidie kuituliza nchi kwa Sasa katika kipindi hiki tulichopigwa na dhoruba. Najua Mzee wangu Spika Ndugai atalifanyia kazi.....
Nimemsikiliza pia Mhongo na Prof Assad.... Hawa Wana majeraha na UONGOZI uliopita kwa Sasa wanataka kurudi ku-justfy kuwa walikuwa sawa. Yes huenda walikuwa sawa lakini hili ni kosa kimkakati kwa Chama ambacho kinatamani kuendelea kuishika Dola na kuiongoza.
Watu Kama Kina Mhongo, Assad na wengineo bado wataibuka wengi Kama Chama hakitachukua hatam ya kuwasimamia viongozi wake. Nilisema Juzi Kati hapa kuwa CCM haijulikani ipo wapi. CCM inatakiwa ikutane mapema Sana kwenye kikao Cha dharura.....Haina Haja ya kufuata kalenda kwa mambo yanayoendelea.
Haya yanayoendelea kwa Sasa ni Hatari Sana kwa CCM yenyewe.
Ole Mushi
0712702602.