Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,330
- 33,954
Kwenye mjadala huu sizungumzii kama CCM "itashinda" tena mwaka 2020 bali najaribu kuona kama chama hcho kina uhalali wa kutuongoza tena kuanzia mwaka 2020 na kuendelea. Nimechagua kuzungumzia chama badala ya watu kwa kuwa inawezekana kabisa baadhi ya watu wasiwepo lakini naamini kwamba CCM itakuwepo mwaka 2020.
CCM ni zao la TANU na ASP na vyama hivyo ndivyo viliasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Muungano uliohitimishwa na Muungano wa vyama hivyo viwili kwa kuundwa kwa CCM mwaka 1977. Na kwa utashi wa vyama hivyo Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 ikaandikwa na kuidhinishwa kutumika.
Wakati mapinduzi ya Zanzibar yanafanyika mwaka 1964, Tanganyika ilikuwa tayari imeshapata Uhuru wake toka kwa wakoloni mwaka 1961 ikifuatiwa na Zanzibar mwaka 1963. Baada ya Mapinduzi kulikuwa hakuna vyama vingine vya siasa vilivyoruhusiwa Zanzibari zaidi ya ASP, na mwaka 1965 TANU ilipiga marufuku vyama vingine vya siasa Tanganyika. Kwa mtiririko huko utaona kwamba kama kuna jambo lolote baya kwenye nchi hii kuanzia mwaka 1965 mpaka leo, ni lazima chanzo chake kiwe ni CCM.
Kama katiba ya Tanzania ni mbaya, basi wa kulaumiwa ni CCM. Kama mfumo wa kuendesha nchi umekaa shaghalabagala basi ni CCM ndiyo wamesababisha. Kwa kuwa hakuna mahali chama kingine cha siasa kimewahi kuongoza nchi hii zaidi ya CCM. Kwa ivo maovu na mabaya yote yanatokana na CCM.Lakini ni kwa nini kila wakati wa uchaguzi CCM huomba nafasi ya kurekebisha maovu yaliyosababishwa na chama hicho siku za nyuma.
Kama Mwalimu alilea uzembe hadi aliyemfuatia Ali Hassan Mwinyi aje na kauli mbiu ya "fagio la chuma" ni kwa nini tena Mkapa akaja na kaulimbiu ya "Uwazi na Ukweli' iliyopigwa kumbo na kauli mbiu ya Kikwete ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu mpya" ambayo imefutwa na kaulimbiu ya Magufuli ya "Hapa kazi tu"?
Kwa nini kila Rais anayetokana na CCM huonesha kwamba Rais aliyetangulia amemwachia nchi "chafu ama dhaifu" wakati wao wote wanatoka kwenye chama kimoja cha CCM? Mwinyi alikuwa waziri kwenye serikali ya Mwalimu, Mkapa alikuwa waziri kwenye serikali ya Mwinyi, Kikwete alikuwa waziri kwenye serikali ya Mkapa na Magufuli naye alikuwa waziri kwenye serikali ya Kikwete. Kwa nini wakiwa mawaziri hawaoneshi kwamba hali ni mbaya kiasi hicho mpaka wawe marais?
Nadhani CCM hakuna mtu anayeweza kutatua matatizo yaliyosababishwa na chama hicho kuwa madarakani. CCM inapata wapi uhalali wa kuongoza tena Tanzania kutokea mwaka 2020 na kuendelea?