CCM ina wenyewe..

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,354
Reaction score
829,591
Ccm ni ile ileee... Ohhh ni ile ileee
Kitengo ni kile kileeee ooh ni kilekileee
Fikra ni zi zilee zileee ooh ni zilee zileee
Chawa ni walee walee ooh ni walee walee
Fitina ni zilee zileee ooh ni zilee zileee
Majungu ni yalee yaeee ooh ni yalee yalee
Kubutua ni kulee kuleee ooh ni kulee kulee..
Sura ni zilee zilee ooh ni zilee zileee
Mbinu ni zilee zileee ooh ni zileezileee

Mapandikizi hayajastawi ukame umeyauwa
Wakuja wamefurushwa..hawana chao tena
Washamba wametawanywa hawasikiki tena
Wajuaji jua linawawakia wengine wamekuwa ndezi, wengine wako jehanum hata kabla ya kifo
Wakubebwa mbeleko imechanika
Wakulialia hamuna leso tena
Waunga juhudi wakakate tu pua waunge wajihi

Kumkoma nyani jiladi.. Kuna baadhi wanaogopa hata vivuli vyao
... wahuni sio watu japo wana roho.. wanakuchinjia baharini huku wanakutupia boya la kujiokoa...!

Chama kimerudisha hatamu... ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKIGODA!

ITIKA! ZINGUMU....!!!!
 
hizo beti za mwanzo na vina vyake nimecheka sana🤣🤣🤣
 
Kazi ipo....!! Marungu yanashuka kwa spidi ya radi..!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…