MMASSY
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 290
- 196
Mnamo wiki jana dunia naTanzania imeshuhudia tukio la kihistoria la kuinyima misaada Tanzania inayofikia dola billioni moja za marekani ambazo ni sawa na Trillioni moja za Tanzania.Mara baada ya shirika moja la marekani linalotoa fedha hizo kutoa uamuzi huo kupitia kwa bodi yake huko Marekani, makada kadhaa wa CCM wakiongozwa na ndugu Humphrey Polepole kutaka kuiaminisha dunia kwa fedha hizo hazikuwa na maana yoyote katika maendeleo ya Tanzania.Makada hawa walijaribu kutupumbaza kama ilivyo kawaida yao kuendelea kuamini kusadiki kuwa mwananchi mzalendo ni yule anayeipenda serikali yake.Nasema hivyo kwa sababu siku kadhaa zilizotangulia uamuzi huo wa MILLENIUM CHALLENGE CORPORATION viongozi wa Ukawa walishatoa tamko kutaka fedha hizo zisitolewe kwa serikali kwa kuwa uchaguzi wa ZANZIBAR uligubikwa na utata(kubakwa).Viongozi waandamizi wa serikali na wanachama wa CCM waliamua kushinikiza tume ya uchaguzi Zanzibar kupitia kwa kibaraka wao Jecha S.Jecha kufuta matokeo ya mwezi october mwaka 2015 kinyume cha sheria.Tanzania ina maajabu kadhaa katika duniahii,ukiachilia yale ya sili kama Ngorongoro na Kilimanjaro, pia ndio nchi ambayo wanafunzi wanaofeli kidato cha nne huenda kusomea ualimu na kuwafundisha wanafunzi ili wafaulu vyema.Lakini pia suala la kufutwa kwa matokeo halali ya uchaguzi Zanzibar mwaka 2015 ni maajabu mengine yanayong’arisha Tanzania katika medani za kimataifa.Kwa bahati mbaya wakati uchaguzi wa Tanzania unafanyika jamii ya kimataifa na taasisi za kiserikali na za kiraina zilikuwa ZANZIBAR na ziliridhishwa na uchaguzi ule kuwa ulikuwa huru na haki.Sio CCM waka CUF waliolalamika kuwa uchaguzi uligubkwa na utata.Sio Shein wala Maalim waliolalamika.Wote waliridhika, lakini kibaraka Jecha S.Jecha alipoona Bwana wake “CCM” na mgombea wao anaanguka kaamua kuyafuta.Kwanini haya yasiwe maajabu?
Duru kutoka ndani ya CCM zinaeleza kuwa hata Dr.Shein mwenyewe alishakubali kushindwa, lakini ubabe wa viongozi wachache hasa kutoka bara wakashinikiza yafutwe.Kuna vijisababu vinatolewa havina msingi wowote.Viongozi wa nchi hii wanafahamu fika kuwa kila anayepewa ruhusa na tume ya uchaguzi kupeperusha bendera ya chama kugombea ni mtanzania.Lakini viongozi hawa hawa wakati wanaadhimisha sherehe za mapinduzi kule Zanzibar waliwaona na pengine waliwatuma viongozi wa UVCCM kubeba mabango yanayowaga wazanzibar kwa misingi ya upemba na uunguja,kwa misingi ya Uarabu na Uafrika.Hoja ya kuogopa kuwapa watu fulani nchi kwa kuwa sio Wazanzibar ni hoja ya kuogopa kivuli chako mwenyewe.
Marekani imeamua kusitisha fedha zote katika mradi wa MCC, Maana yake ni kuwa, ule umeme wa vijijini tuliokuwa tunaahidiwa na serikali ya CCM ndio umeota mbawa hivyo, zile dawa za kifua kikuu na matibabu ya bure tuliyokuwa tunapata bure tuanze kujipanga kulipia, zile dawa za Arv ambazo waathirika wa ukimwi walikuwa wanapewa ndio ziko mashakani na zikija na bei ghali mno.zile barabara kadhaa zilizokuwa zinajengwa nchini kwa fedha za MCC ndio zinaota mbawa.Tutarudi kwenye zile barabara zetu za asili ambazo mvua ikinyesha wote hatuwezi kufika majumbani mwetu.Vyandarua vinavyogawiwa bure leo vinapatikana na msaada kutoka marekani,Kuna tangazo moja ambalo huwa silipendi na nashkuru siku hizi halichezwi redioni.Lenyewe linatangaza umuhimu wa kunawa mikono nalo ni kwa hisani ya Marekani.CCM na Humphrey Polepole wanataka leo hii tuwapuuze wamarekani.Tutawapuuzaje wakati nyie ndio mliosainiana nao mkataba wa kutunawisha mikono?Leo hii bajeti ya nchi tunaambiwa inategemea wahisani kwa 40% lakini kwa wataalamu wa kiuchumi watakubaliana nami kuwa tunategemea wahisani kwa zaidi ya asilimia 50%.Waliotufikisha huku ni CCM ambao leo wanataka eti uzalendo wetu upimwe kwa kipimio cha kuwatukana wamarekani.Haiwezekani chini ya jua wala juu mbinguni.Ni hivi, mbwa anamweshimu zaidi yule anayempatia chakula kuliko yule aliyemnunua na kumweka kwenye banda.Serikali ya CCM ambayo Polepole amejipa kazi ya kuiteteta kwenye upuuzi wameongoza nchi hii kwa miaka ya kutosha wamesaini mikataba kadhaa na mmojawapo ni wa MCC mradi ambao awamu ya kwanza ya iliyoshia mwaka 2013 ulikuwa na dola millioni 698.1.CCM kwa uroho wao wa madaraka ya kisiwa cha Zanzibar na kutunga sheria kandamzi ya mitandao ili kisikosolewe.Yaani Watanzania mamilioni wanateseka kwa sababu ya upuuzi wa CCM.
MCC inafanya kazi maeneo tanzu matano ambayo ni Elimu, Afya,Nishati,maji na umwagiliaji na masuala ya ardhi.Wakati wa kampeni mkwaja 2015 CCM waliitumika vyema misaada ya wamarekani kujipatia kura vijijini.Waliahidi umeme na wakionyesha namna umeme ulivyorahisishwa upatikanaji wake, walionyesha na maeneo ambayo yanasubiria fedha za MCC kuyakamilisha.Mfano kule Hai mkoani Kilimanjaro kuna baadhi ya vijiji kama Ngosero na Mbatakero ambako zilikuwa zinasubiriwa fedha za MCC ili kukamilisha ufungwaji wa umeme.Sasa ndio zimeyeyuka na CCM wanataka kutumia kete ya sizitaki mbichi hizi.
Humphrey Polepole anataka kutuaminisha yeye na CCM yake kuwa Wamarekani wanataka kuingilia masuala yetu ya ndani(Sovereignty).Fikra hizi ni potovu kwa sababu kadhaa, moja, suala la serikali ya CCM kusaini mkataba na MCC wenye kuingilia uhuru wa nchi yetu maana yake ni kuwa CCM walikubali kuuza nchi yetu bla sisi kujua kwa maana hiyo Kikwete atuombe radhi kama Mwenyekiti wa CCM na chama kiwajibike.Pili, kama miaka yote tangia 2012 MCC walifanya kazi ya kutoa huduma za kifua kikuu bure Tanzania,Wakachunguza na kutibu saratani ya kizazi bure,walitupatia vitabu mashuleni lakini pia walitupatia umeme wa uhakika vijijini.Hizo zingine ni propaganda za CCM.Kama vile hawakumbuki, ccm wanatuaminisha sasa kuwa eti fedha hizo sio dili kwetu na kwamba sasa ndio muda mwafaka wa kuchukua hotuba za mwalimu Nyerere na kutuaminisha kuwa hata serikali ya CCM haipendi misaada ya masharti magumu.Huu ni uchuro.Serikali ya CCM haijawahi kubuni vyanzo vipya vya mavavi kwa sababu ya kutegemea wahisani.Kikwete amesafiri zaidi ya safari 4092 kwa muda wa miaka kumi.Kila safari ilitumia kiasi cha angalau siku nne.Kote huko alikuwa akisaka fedha za wahisani zikiwemo za MCC. Suala la Zanzibar tu na sheria ya mitandao ndio limeigharimu serikali ya CCM.Tunachotakiwa kujua sisi kama Watnzania ni kuwa ni kweli kunyimwa fedha hizi hakuna athari kwa viongozi na watu kama akina Humphrey Polepole kwa kuwa wao tayari wanamiliki majumba mjini na tayari yana umeme wa kutosha.Wao wakuimwa tatatibiwa ulaya na India iwe mafua au kfua kikuu ama ukimwi.Wao watoto wao watasoma kwenye shule zenye mahitaji yote na wanayo fedha za kuwasomesha HAVARD UNIVERSITY.Kwa viongozi wa Ccm kila kitu kwao ni siasa tu.
Tukumbuke katika suala zima la uhusiano kati ya nchi moja na nyingie kutokana na shria za kimataifa ni la hiari.Sasa kama CCM wenye serikali wanaona uhusiano wetu na marekani hauana afya kwa kuwa unaingilia uhuru wetu wa ndani basi wauvunje.Rais anajua kuwa yeye anayo mamlaka hayo wala aitaji ushauri wetu wananchi.Polepole anaelewa kidogo sana masuala ya diplomasia.Angekuwa anaelewa vizuri angejua kuwa uhusiano kati ya nchi moja na nyingine ni zaidi ya siasa.Angeelewa kuwa, siku hizi Tanzania haitekelezi kwa kiasi kikubwa sera yake ya mambo ya nje ya mwaka 1964.Inatekeleza sera mpya ambayo imejikita katika masuala ya kiuchumi zaidi zaidi ya harakati.
Pole pole na makada wengine wa CCM wanatakiwa kuelewa kuwa Mwalimu Nyerere hakutaka kabisa kuwa na ubalozi wa Israel hapa nchini Tanzania kwa sababu ISRAEL Ilikuwa inauwa na inaendelea kuuwa Wapalestina wasio na makosa na wanakalia ardhi yao kimabavu.Angeelewa pia kuwa Rais JPM amesharuhusu ubalozi wa marekani ukafunguliwa hapa Tanzania.Hii inaitwa evolution ya Foreign policy and Diplomacy.Je Polepole na makada hawa wa CCM ni kwamba hawajua hayo?hawajui kuwa CCM ilisaini kupata fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi? Imekuweje leo hii makosa ya CCM yanaigharimu Tanzania?
Sera ya mambo ya nje ya marekani inajulikana wazi; wao ni Cpitalists wanaamini katika soko huria,utawala wa kidemokrasia na haki za binadamu.Iweje leo hii wakubali ubakajiwa demokrasia uliotokea Zanzibar? Yaani hata mimi ningewaona wa ajabu kama wangefumbia mamcho uchaguzi huu wa maigizo.Uchaguzi ambao uliandaliwa na serikali ya CCM,Ukasimamiwa na serikali ya ccm na matokeo yakatangazwa na serikali ya CCM.Ni uchaguzi wa ajabu kuwahi kutokea.Ulikuwa na wasimamizi wa ndani tu ambao ni JWTZ,Jeshi la polisi,Makada wa CCM kama Kificho na wenzake.Ulikuwa ni uchaguzi ambao vikosi vya ulinzi na usalama vilijazwa Zanzibar kuliko idadi ya wananchi wa huko na ulikuwa ni uchaguzi ambao watu walikuwa hawaonekani vituoni lakini maboksi yalijaa kura mapema asubuhi.Hivi CCM na polepole wanadhani kuwa Wamarekani wanaumwa macho? Na kama ndio je hata kusikia hawasikii?
Kuna msemo wa kiswahili unasema kuwa debe tupu ndilo linapiga kelele.Kama fedha hizi sio muhimu kama baadhi ya makada wa CCM wanavyodai,basi watafute fedha waziweke kwenye gap iliyoachwa na fedha za MCC kama wana ubavu.Yaani huduma za kifua kikuu zitolewe bure,kina mama waendelee kufanyiwa utafiti na matibabu ya saratani ya kizazi,fistula, tuone umeme unaedenelea kufungwa kwa kasi vijijini na kwa bei rahisi kama ilivyokuwa, tuone pia miradi ya barabara na huduma zingine zinatolewa kamailivyokuwa.Kutuletea maigizo kwenye keyboard za Kompyuta hakutatoa shida wala kutibu makovu yaliyoachwa na fedha za MCC.
Polepole na wenzake amejaribu kutuvika joho la watu wasio WAZALENDO kwa kuwa tunaikosoa serikali kutokana na kosa walilolifanya hadi kupelekea kunyimwa fedha hizi.Mimi naelezaulimwengu kuwa, kati ya raia safi wa nchi hii naamini namimi nimo kwa sababu kuwa mzalendo hakutokanai na kutetea serikali bali kutetea na kuipenda na kuilinda nchi yangu. Yani kwa wale wasioelewa maana ya uzalendoakiwemo Humphrey Polepole ni kwamba kuwa mzalendo ni kuipenda,kuitetea na kuitumikia nchi yako kwa gharama yoyote na sio kuitii,kuitetea serikali na chama chako kwa sababu moja tu rahisi.Katika mazingira yoyote yale, Serikali zinapita kama itakavyopita ya CCM,Chama kama CCM kitapita tena kwa mwendo kasi lakini nchi ya Tanzania itabaki milele.Na ndio sababu nimeamua kuwa upande huu.Napenda vijiji na miji yote Tanzania iwake umeme wa bei rahisi, napenda Watanzania wote watibiwe bure tena kwa fedha za nchi yangu na hata za nje,nataka barabara zijengwe hadi kule usaki,uri,mang’ola na kwingineko ziwe za lami kabisa.Napenda sana kuona Tanzania ikibaki stable hata baada ya kuwa hatuna serikali ya CCM kuliko kuiona CCM ikibaki salama na nchi ikiteketea.Na hiyo ndiyo tofauti ya uzalendo ninaoujua mimi na ule wa makada wa CCM wakiongozwa na Humphrey Polepole.
TAFAKARI