MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
CCM bado inakabiliwa na kazi ngumu sana ya kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo linaongozwa na Mbunge kutoka CHADEMA, Joseph Osmund Mbilinyi maarufu Sugu pamoja na kupata ushindi wa Udiwani katika kata 3 kwenye uchaguzi mdogo uliomalizika jana katika Jimbo la Mbeya Mjini.
Ukichunguza utagundua kuwa matokeo ya kura za Madiwani yanaonyesha ni jinsi gani CCM bado ina safari ndefu sana katika kurudisha Jimbo la Mbeya Mjini. Matokeo ya Kata tatu ni angalizo linalojitoshereza kwa kiwango kikubwa kuchambua kwa undani mwonekano wa siasa katika Mkoa wa Mbeya hasa Jimbo la Mbeya Mjini.
Katika Kata 3, wagombea wa CCM walipata jumla ya kura 7,851 wakati wagombea wa CHADEMA walipata kura 6,115. Tofauti ya kura ni 1.736.
Kata ya Maanga, Newton Mwatujobe (CCM) alipata kura 1897 na kumshinda, Steven Mwashilindi (CHADEMA) ambaye alipata kura 1703.
Katika Kata ya Iwambi, Humphrey Ngalawa (CCM) alipata kura 2107 huku Elisha Mwandele (CHADEMA) akipata kura 1906.
Aidha katika Kata ya Nsalaga, Kasusura, David Ngogo (CCM) alipata kura 3847 wakati Reward Mshanga (CHADEMA) akipata kura 2506.
Matokeo haya yanaweza kuwafurahisha wanaCCM lakini ukichunguza kwa undani zaidi kwa kutumia sayansi ya siasa utagundua kuwa safari ya CCM kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini bado ni ndefu sana hasa ukichukulia kuwa ni mkoa ambao unaongoza kwa kuwa na vijana wengi wajasiliamali wasio na mitaji mikubwa.
Sijui ni nani atasimama kama mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu 2020, lakini kama CCM itaendekeza siasa za ‘’kubebana’’ katika mchakato wa kumpata mgombea wa kupambana na Mbunge Mbilinyi, sitashangaa kuona Jimbo likibaki mkononi mwa Mbunge wa sasa.
Nimemuona Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dr. Tulia Ackson Mwansasu akipita huku na kule Jijini Mbeya lakini ukichunguza zaidi utagundua anatafuta fursa ya kuchaguliwa na wanaCCM kuwa mgombea Ubunge. Ninaweza kuwa siko sahihi lakini historia inaonyesha kuwa ukiona mwanasiasa anafanya jambo fulani kwa jamii lazima atakuwa anatafuta maslahi zaidi ya kisiasa!
Baada ya kumsikia Dr. Tulia kwenye majukwaa ya kisiasa akijieleza, Sina uhakika kama huyu anaweza kupambana na kushinda ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini. Ninaweza pia kuwa siko sahihi kama ambavyo Waziri Mkuu wa Uingereza, Harold Wilson aliwahi kusema, ‘’a week is a long time in politics!’’
Kwa matokeo haya ya jana, CCM wanatakiwa wazichange vizuri karata zao za kisiasa kama kweli wanataka kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini.