CCM ina kazi kubwa sana ili kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini!

Naishauri Tume ya Uchaguzi igawe jimbo la mbeya mara mbili, idadi ya wapiga kura ni kubwa.

Hii itaodoa huo msuguano (CCM watapata na Chadema watapata)
 
Niliona Monduli ndio jimbo lenye vikwazo hasa kuliko hata Mbeya Mjini!

Ila kilichofanyika Monduli katika uchaguzi wa Marudio ya Jumamosi nimebaki kinywa wazi!


Yani CHADEMA na LOWASSA nyumbani kwao, tena katika kabila lenye msimamo na mshikamano kama Masai eti anazawadiwa asilumia 3% ya kura zote zaidi ya elfu sitini?

Kama Monduli CCM wameweza sioni mahali ambapi watashindwa!

Huu ni uchaguzi uliokuwa na maajabu kuliko maajabu yale saba ya dunia!

Ww baki na idadi ya wapiga kura ya kupikwa. Kwa taarifa yako huko monduli waliojitokeza kupiga kura hawafiki 20,000. Watu wametangaza idadi kubwa kuficha aibu. Tumeona kwa macho yetu na ndio maana huoni wanaccm wakishangilia sio monduli tu wala ukonga maana wanaona soni.
 
Ninapenda sana watu wanaodadavua masuala ya kisiasa kama ulivyofanya.

Tatizo linalokumba kwa sasa hili jukwaa la siasa hapa Jamiiforums ni kuwa na wachangiaji wa sentesi moja yenye kutafuta LIKES za wajinga!

Kwa sasa watu wenye uelewa mpana wanasoma heading na thread tu halafu wanaenda kwenye thread nyingine kwa sababu ni kupoteza muda kusoma michango ya wachangiaji wa thread kutokana na michango ya kitoto au kijinga.

Usichoke kutoa elimu kwa faida yetu tunaopenda kusoma michango yenye kufikirisha zaidi.

Unaweza ukaandika ukaona umeandika hoja za maana na ukapata nguvu ya kutoa kejeli kwa wengine kwa kuamini una hoja za msingi. Ila ukweli uko hivi hoja yako/zako hazina maana kama utafumbia macho ukweli. Kwa sasa ukweli uko wazi, mkuu wetu hawezi siasa za ushindani, hivyo anatumia nafasi yake kuagiza tume kumtangaza mgombea wa chama chake bila kujali box la kura linasemaje. Hivyo huo uchambuzi wako tunauona ni kama furahisha genge. Tusubiri huko mbeleni iwapo tutapata kiongozi anayemudu ushindani ulete uchambuzi wako na sio sasa. Ni wendawazimu kujadili ubora wa Yanga au Simba iwapo wananunua mechi na kuingia na matokeo uwanjani.
 
Kwa maoni yangu, kwa uchaguzi wa mwaka 2020, jimbo pekee ambalo CCM itapata taabu sana kulikomboa ni jimbo moja tuu la Zitto, kwa sababu determinant ya ushindi sio sera, sio chama wala sio wapigakura bali ni mtu wao.
P
Sikuingi maana kweli yaweza kuwa umefanya tafiti. Ila kwangu Mimi majimbo "magumu" sana kwa ccm kuweza kushinda ni pamoja na Kaliua lililo chini ya Sakaya Magdalena wa CUF. Yule mama ni "jasiri" sana
 
Ww baki na idadi ya wapiga kura ya kupikwa. Kwa taarifa yako huko monduli waliojitokeza kupiga kura hawafiki 20,000. Watu wametangaza idadi kubwa kuficha aibu. Tumeona kwa macho yetu na ndio maana huoni wanaccm wakishangilia sio monduli tu wala ukonga maana wanaona soni.
Mkuu tindo

Ukinisoma kwa upole na utulivu utaona masikitiko yangu.

Hakuna Mwana CCM mwenye akili timamu anayeweza kuchekelea aina hii ya uchaguzi!
 
Sikuingi maana kweli yaweza kuwa umefanya tafiti. Ila kwangu Mimi majimbo "magumu" sana kwa ccm kuweza kushinda ni pamoja na Kaliua lililo chini ya Sakaya Magdalena wa CUF. Yule mama ni "jasiri" sana
Mkuu Chakaza

Hakuna narudia tena, hakuna jimbo mpinzani atashinda bila ridhaa ya raia namba moja nchini.

Yeye ndiye atakayeamua nani awe mpinzani wapi, kwa kura kiasi gani na kwa muda gani wa utumishi wake Bungeni kama raia huyo namba moja ataendelea kuwa Mkuu mpaka wakati wa uchaguzi!

Chaguzi hizi ndogo zimetoa picha ya jumla ya nini kitafanyika katika chaguzi zijazo!
 
Back
Top Bottom