Kijibabu
JF-Expert Member
- Apr 3, 2016
- 462
- 586
Umeongea point kubwa sana. Kwa wasio zijua siasa za Mbeya hawawezi kukuelewa. Ukitazama hata ushindi wa Sugu 2010 ni kwa sababu CCM Mbeya waliziba masikio na kuendelea na ujinga wao . CCM Mbeya sio wasikivu na hawajifunzi kutokana na makosa. Sugu anatumia sana advantage ya udhaifu wa CCM kuwateka wana Mbeya.Uchambuzi wako uko sahihi. Siasa za Mbeya mjini ni upinzani wa kukomoana baina ya Wanyakyusa (wakuja wenye majidai na dharau dhidi ya wenyeji) na Wasafwa pamoja na wageni wengine (wanaodharauliwa kwa ufukara wao). Nimeishi na kufanya tafiti za kisiasa na kijamii Mbeya. Siasa za hapo ninazijua na ni za siku nyingi (historical). Msigano huo wa kijamii ndio mtaji wa Sugu (siyo Mnyakyusa). CCM wakitaka kulirudisha jimbo la Mbeya mjini waachane na Tulia (pengine wamtafutie jimbo jingine mkoani humo, kama hapana budi). Atafutwe Msafwa au mgeni mwingine apambane na Sugu. Chadema ni coincidental beneficiary wa Siasa za kikabila na kudharauliana za Mbeya.
Kumsimamisha Shitambala 2015 ilikua ni kosa kubwa sana na hata zile kura 60k walizipata kwa wanaCCM kindakindaki tu. Na kosa kubwa sana ni kumfunga sugu bila kujua wanamuongezea Kiki kwa wananchi.
Katika majimbo yanayopata tabu kwa hizi siasa za CHADEMA/CCM basi Mbeya ni ya kwanza. Limekua Jimbo yatima kwa sababu serikali haitaki kufanya chochote kwa kuwa wakifanya Kitu credit atapata sugu na CHADEMA. Hizi siasa zimetuletea madiwani wadhaifu sana kwa sababu raia waliamua kuikomoa CCM kwa kuchagua CHADEMA hata kama wengi wa wagombea wao hawakua na sifa. Mfano mzuri ni kata ya Isanga ilikua inapiga hatua kimaendeleo ila hizi chuki za CCM/CHADEMA zimeirudisha sana nyuma baada ya kumpiga chini diwani wao mzuri wa CCM.
Kati ya NSSF au NHC walikua tayari kujenga Mall kubwa pale lilipokua Soko la uhindini lakini hizi siasa za majitaka zimepelekea mpaka leo lile eneo lipolipo tu. Sasa wakienda kujenga mkoa mwingine tutaanza kulalamika kuwa watu/mashirika hawataki kuwekeza Mbeya Kumbe hatuna Sera nzuri tu.
Hata timu ya Mbeya city imekumbwa na huu msukosuko. Inakwepa kushuka daraja kabla hata msimu haujaanza. Ikifika 2020 utaona wanasiasa watakavojipendekeza kuipa msaada wakati saizi ina ukata utafikiri ni timu ya walalahoi kama majimaji.
Kama 2020 Sugu (CHADEMA haina ubavu wa kusimamisha mgombea tofauti na yeye ) atapita na CHADEMA ikashika tena halimashauri basi maendeleo Mbeya yatabaki kuwa ndoto za mchana. Japo tunaichukia CCM lakini CHADEMA Mbeya sio mbadala sahihi wa CCM. Yaani wave of change iliwabeba sana CDM na athari tunaiona saizi.
Japo hatupendi ila hii ndio hali halisi ya Mbeya