CCM ina gundu gani?

Nani aliye wa chomoa fuse kichwani ninyi vijana wa Lumumba mtu mwenye akili timamu hawezi jifurahisha kwa picha ya uwongo jinga kabisa wewe!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aliyefanya hivyo kafa
 
Naomba kuona picha zenu za jana mlizopiga kwa drones
Tune nyomi?
 
👊👊
 
Naomba kuona picha zenu za jana mlizopiga kwa drones
Tune nyomi?
Unataka picha au unataka sera?

Yaani watu wànajadili fainali murua ya Asernal na Liverpool kuliko uzinduzi uliogharimu zaidi ya mil.700?
Watu wanadili hotuba yenye matumaini kwa;
Watumishi
Wakulima
Wanafunzi
Wavuvi
Vijana
Wanawake
Wazee na
Taifa
Iliyotolewa viwanja vya Tanganyika Packers Jana.
Tena wanoijadili wengi ni wale walioshiriki kuandaa "Green Fiester" pale uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wengine wanasema angalau kasema ya maana kuliko juzi Mbagala, hawajui wanayemjadili NI YEYE.
Wengine wanasema ametoa wapi hayo wakati Ilani yao haijazinduliwa, hawajui wanayemjadili NI YEYE.
Wengine wanasema atatoa wapi hela ya Bima ya Afya kwa wote, Machinga kutotoa 20k baada ya kuboreshewa mazingira ya biashara, Watumishi wanaodaiwa na HESLB kukatwa 3% badala ya 15% na itakuwa kwa wale wenye ajira zinazoeleweka tu, wamesahau hapa wanayemjadili NI YEYE.
Wanasema kwa nini juzi kaongea mengine na Jana kaongeza mengine, wamezoea kusikia yule mtu mwenye wimbo mmoja wa Flaiova, Mandege, Standaji Geji kila siku, wanasahau maneno haya yanayempaisha NI YEYE.

Credit kwa Bila bila
 
Naomba kuona picha zenu za jana mlizopiga kwa drones
Tune nyomi?
SISI SIO WAJINGA

Ulipochukua tu madaraka ukaanza na kubomoa nyumba zetu ktk bonde la Msimbazi. Bila huruma ukatuacha tumelala nje na watoto wetu. Ulidhani tutahama mjini lkn sisi bado tupo.

SISI SIO WAJINGA
Ulipokuwa unapanua barabara ya Ubungo - Kibaha ukabomoa nyumba zetu. Mbunge wetu Mnyika aliomba utulipe fidia ukampinga mbele yetu. Lengo lako tufe masikini lkn kwetu sisi maisha yanaendelea.

SISI SIO WAJINGA
Baada ya kuwa tumefanya kazi kwa miaka 40 na tumebakiza miezi 3 tustaafu ukatufukuza kazi kwa kisingizio cha vyeti feki. Ulidhani tutakufa kwa njaa lkn Mungu anatupigani bado tunaishi.

SISI SIO WAJINGA
Tulipopata tetemeko la ardhi Watanzania wenzetu walituchangia pesa nyingi lkn wajanja wakatafuna. Ulipokuja Bukoba tulidhani utatutetea wanyonge badala yake ukatusimanga na kutukumbusha majanga ya Ukimwi, MV Bukoba kwamba yote yanatupiga sisi. Sasa nasikia unakuja kuomba kura kwetu! Je, ni kweli ww utakanyaga Bukoba?

SISI SIO WAJINGA
Tukaenda Mtwara kulima korosho. Ukatuma askari wako wakatunyang'anya korosho halafu wakadai tuwaonyeshe mashamba yetu. Mbona wanaolima mahindi, pamba, mpunga, n.k.hamuwaulizi mashamba yao? Ukasema hao askari watabangua korosho kwa meno ili kila Mtanzania atapata 2kg, lkn hatujapata mgao. Sasa nasikia unakuja kuomba kura! Landa uishie Nangurukuru kwa sababu SISI SIO WAJINGA.

Credit kwa Goheki
 
wewe nawe acha kusumbua watu, hamia CCM
 
Unataka picha au unataka sera?
Kwani sera hizo za lisu ni ngeni hapa duniani?
Hata obamaalisema akipewa nchi ndani ya siku mia moja atafunga gerza la gwantanamo, lakini mpaka sasa lipo.
Akasema atawashugulikia wapalestina wapate ardhi yao iliyoporwa na waisraeli na wapalestina wakalipuka kwa shangwe,
Lakini mpaka sasa wanasubili utekelezaji wa obama, sasa itakuwa lisu ambaye ahjui hata huko serikalini kuna nini, hata ilani yenu tu haipo.
 
Halafu hii umeileta kimasihara lakini ndio ukweli.. nyota imefifia sana..tunatumia nguvu kubwa kuirudisha! Na hata wao wanajua hilo.. nafsi zao zinasononeka,usihadaike na sura zao moyoni wamejaa maumivu!

HAKI HUINUA TAIFA.
 
Vipi mbona unatoka tena nje ya mada? Na kuzungumzia past tense? Kwanini mnapenda kuishi nyuma ya wakati!?
 
Gundu ni pale unapozindua kampeni halafu unakumbuka mifuko mitupu pesa zote ulinywea bia😱 "unaanza hay bonyeza *150*0....."
 
Vipi mbona unatoka tena nje ya mada? Na kuzungumzia past tense? Kwanini mnapenda kuishi nyuma ya wakati!?
Haya sera gani unadhani kasema ina ukweli?
Atowe bajeti yake na mchanganuo wa kwa vipi ataweza kutekeleza hayo na mapato yatatokana na nini
Maana kuna kodi zitapunguzwa ila matumizi yataongezeka?
Sasa hiyo pesa ya ku cover hayo atatoa wapi?
Hili ndo jambo la msingi atwambie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…