CCM imeshindwa tuisaidie kuondoka salama

Basil Lema

Member
Jan 20, 2013
86
277
Leo ninaanza na hoja ya upinzani katika siasa Tanzania.

Sitaweza asilani kuzungumzia somo lote la historia ya upinzani wala kina cha ukombozi wa Afrika. Lakini katika kuhawilisha somo nitawapeleka kwa matukio na wawezeshaji wa baadhi wa matukio hayo.

Wanajukwaa wenzangu.

Upinzani katika siasa unaonekana leo kama kazi inayofanywa na vyama vya siasa peke yake. Kimsingi hii ni kazi ifanywayo na hivi vyama kwa niaba ya makundi mengi. Labda nitangulie mapema kabisa kusema kwamba vyama vya siasa vinanyamazisha makundi hayo ili viyasemee mahitaji yao kwa utaratibu bila vurugu.

Makundi makubwa katika kudai HAKI na USTAWI wa jamii ni pamoja na:-
1. Wafanyakazi (kupitia vyama vyao)
2. Wakulima (kupitia vyama vyao)
3. Wanafunzi na wanazuoni (kiholela na kwa kupitia vyama vyao)
4. Waandishi wa habari (kwa kazi zao)
5. Mashirika ya dini...
6. Walipa kodi wasiowakilishwa na vyama vyovyote kimfumo.
7. Wafanyabiashara (kwa kupitia vyama vyao)
8. Tabaka la watu wasio na usajili rasmi na hasa WAHUNI. (Lumpen proletariat class) Tabaka hili lina [wazururaji, wasio na kazi, makahaba, wachuuzi wadogo, wehu na makundi yote ya wahitaji maalum]
9. Mashirika yasiyo ya kiserikali
NA
10. viongozi wa kimila na kijamii.

Katika uongozi wa siasa ni lazima SERIKALI za dunia zitunze kwa umakini, usahihi na UTIIFU haki na maslahi ya makundi yote haya. Hii ni pamoja na haki za watoto na wazee.

Serikali zinawajibika kuwatumikia kwa sababu wanawezeshwa kwa kutumia kodi zinazotokana na jasho lao jingi. Serikali zinawajibika kuwatumikia ili waishi vizuri na waendelee kiuchumi ili watakapoinua ununuzi na kiwango cha huduma wataweza kulipa kodi kubwa zaidi kwa malengo ya kuiwezesha aerikali kutajirika na kutekeleza mipango yake mingi ya maendeleo.

Katika zama za mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi mwishoni mwa miaka ya 1980 nchi nyingi zilijikuta zikilazimika kurekebisha mifumo yake ili kuboresha njia zake za kukusanya kodi na kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa kila mwanachi. Ilionekana kuwa vema zaidi kwa kuondoa ulipaji kodi ya kichwa uliokuwa wa kudhalilisha na kutweza utu wa raia na kupeleka kodi hizo kwenye bidhaa.

Kutekeleza haya serikali zililazimika pia kupanua mawanda ya kisiasa na kidemokrasia. Hii haikuwa haki ya baadhi ya watu bali kwa wote.

Enzi hizo kelele hatari zaidi zilikuwa za WAFANYAKAZI. Vyama vyao vilitoa sauti kubwa zaidi kwa kila kundi. Walimu walipiga kelele sana kuhusu maslahi yao, wafanyakazi wa viwandani, wafanyakazi wa majumbani, wafanyakazi wa mashambani, nk. Kila chama kimoja kimoja kilipofanya mkutano basi waliishia kupiga kelele nyingi dhidi ya mifumo ya uendesha na kutetea haki zao. Migomo ya wafanyakazi ilikuwa tishio kubwa dhidi ya serikali na hivyo ikawa lazima kwa serikali kutoa suluhisho la kimfumo ili haki za wote zilindwe kiuhakika.

Ili serikaki zitende shughuli zake kwa ukweli, uwazi na ushirikishwaji wa umma wote, ilibidi sheria zitungwe za kupambana na ufichwaji wa taarifa za utendaji na matumizi yake kwa umma.

Leo tusizungumzie makundi ya:
DINI
LUMPEN PLORETARIET
NGOs
WAHITAJI MAALUM
WAFANYAKAZI na
WAFANYA BIASHARA

Tuweke mawazo yetu kwa washiriki katika utawala wa nchi peke yake. Nimetumia term hiyo ili neno wanasiasa lisitumike kama hatarisho kama watawala wanavyojitahidi kufanya katika nyakati za sasa.

Makundi yote kabisa yanaweza kutetewa na vyama rasmi vya siasa. Hata wanaotawala wanafanya hivyo kwa kutumia vyama vyao vya siasa.

KWA MANENO MENGINE MARAHISI ZAIDI ni KWAMBA VYAMA VYA SIASA VINATUMIKA KAMA MDOMO WA MAKUNDI YOTE YALIYO RASMI NA YASIYO RASMI NCHINI.

Vyama vya siasa vinatumia kutengeneza na kutekeleza sera zinazotetea MASLAHI na HAKI za makundi hayo.

CCM kwa upande wake ilipata ahueni kwa kuwezeshwa kwa vyama vya siasa rasmi kuzungumza kwa niaba ya makundi mengine ya kijamii (ambayo yangeongea kiholela na kila moja kivyake) Sasa badala ya kusikiliza makundi zaidi ya 20 wanasikiliza makundi yasiyozidi 5.

Hii ni kusema kuwa kwa kutumia usajili wa vyama vya siasa, serikali ya CCM wakati ule ilinyamazisha kelele za makundi yaliyokuwa yakililia maslahi yake kwa hadi kufikia kutekeleza migomo hatarishi kwa serikaki na jamii nzima ya Tanzania.

Leo: baada ya kunyamazisha kelele za makundi hayo mengi na kuweka haki ya utetezi wa maslahi ya umma kwa vyama vya siasa, CCM inafanya bidii nyingi kunyamazisha kelele za utetezi zinazopigwa na vyama vya siasa. Katika kutekeleza lengo hili CCM itafurahia sana kuwepo kwa vyama vya siasa visivyo na lengo wala sauti ya kutosha kuikosoa na hadi kufikia kuiondoa madarakani.

Vyama makini na vinavyoonekana kuimarika hadi kuhatarisha uwepo wa CCM madarakani ni hasimu wa CCM kwa kuwa tu wanawanyima usingizi na pengine wanaweza hatimaye kuwaondoa kabisa.

Hawa CCM waliweza kuvizima vyama kama NCCR Mageuzi, CUF na TLP vilipokuwa na nguvu kwa kuingiza migogori ndani yake wakitumia mawakala wao wa kuua upinzani. Kila wanapoua chama chenye nguvu wanastawisha kingine watakachokiendesha kisifikie kuwadhuru. Huu ni mradi wa kudumu wa CCM na serikaki yake wenye lengo la kuibakiza madarakani kwa kisingizio "visible" kwamba upinzani haujaimarika kiasi cha kupewa nchi na eti wao wanakubalika kwa kuwa "wanashindaga kila uchaguzi kwa kishindo"

Mahitaji ya wananchi yamewekwa mikononi mwa vyama vya siasa. Juhudi zozote za kunyamazisha vyama vya siasa na wanasiasa ni bidii za kunyamazisha sauti za wananchi walipa kodi ili MITUPORA iendelee kunyonya wananchi.

Ingawaje leo sitazungumzia "vita kuu baina ya watawala na upinzani", lakini ni vema ifahamike kwa sasa hoja si tu kuogopa kwa CCM kuondoka madarakani bali ni kwa MITUPORA kuvunjiwa mnyororo wao wa kuendelea milele kuelea katika ulevi wa madaraka, ulaji na utapanyaji wa mali za pamoja za umma na uhakika na matarajio ya mbeleni ya kuendeleza uporaji huo wao.

Ndugu wanajamvi:
CCM iko katika vita ya sasa ambamo wanafanya matendo mengi ya kinyama kwa wapinzani wao kisiasa kwa sababu MBILI kuu.
1. Ni kuchelewa kwao kuuzimisha upinzani hasa ule utokanao na CHADEMA.
2. Uvivu wao wa muda mrefu katika kufikiri, kupanga mipango na kuitekeleza hadi kufikia kujenga jamii ya raia wenye maisha bora, furaha na usawa katika kila jambo.

Kwa kuwa wao wanafikiria uchaguzi tu na kubaki madarakani milele, hawaoni hata siku moja sababu ya kujibidiisha kubadili maisha ya wananchi. Wameishia kuimarisha idara yao ya kudhoofisha na kuua upinzani tu.
Walifanikiwa kuua vyama vingine huko nyuma.
Kwa bahati mbaya wakaisahau CHADEMA. Wamekuja kushtuka liCHADEMA limekuwa likubwa sana. Haiwezekani kupambana nayo kwa hoja wala umaarufu. Haiwezekani kuishinda katika uchaguzi huru. Wamebakia kutumia maguvu kuinyamazisha na kuidhoofisha kwa lengo la kuiua.

Wanawatesa sana wale wanaosimama kama nguzo imara za CHADEMA. Hiki ndiyo chanzo cha vita na madhila mengi anayopitia MBOWE. Wanampiga ili waisambaratishe CHADEMA. "Nitampiga mchungaji na kondoo wake watatawanyika". Ukweli unabaki kuwa, CCM na serikali yake inatupitisha katika uchafu na ushetani huu si kwa kupenda kwake. Bali hawana njia nyingine ya kujinusuru na makali ya CHADEMA. Wakijisahau tukafanya uchaguzi huru na wa haki, sioni namna watakavyopata hata 20% ya kura za wananchi. Watapata ushindi tu kwa kutumia wizi wa kura, kupora kibabe na kuwalaghai wananchi.

Lile la PILI kuhusu uvivu wao wa kufikiri, kupanga na kutekeleza shughuli zenye kuboresha maisha ya wananchi ndilo linalotangaza heshima na hadhi ya CCM. Hiki ni chama kisichoweza kuwa na kikosi cha wazalendo wenye kuifikiria na kujitolea kwa uaminifu kuwapigania wananchi. Hakina nafasi hata moja ya watu wazalendo wa kweki na waaminifu kwa taifa. Akitokea mmoja watapambana naye kama joka lililoingia nyumbani vile. Hata pale wanapoapa mbele za MUNGU wanafanya hivyo wakijua wazi hiyo ni hatua tu ya kusonga mbele ili wakapore kwa masilahi yao pamoja na ndugu na jamaa zao tu. CCM kimekuwa chama cha kujiimarisha kwa kutoa propaganda tu! Wanajisifia kutenda mema na kupambana na kila sauti ya wale wanaowaonesha makosa yao.

Kwa bahati mbaya sana leo hii CCM hawana macho ya kuona nguvu ya upinzani ikiyoko mbele yao. Wanaiangalia CHADEMA ya mikutano mikubwa ya hadhara. Lakini hawajui kwa sasa teknolojia imetengeneza upinzani mkubwa zaidi ambao siku utakapolipuka hakuna namna watakavyoweza kupambana nao. CHADEMA ilifakuwa ikifanya si zaidi ya mikutano mikubwa MITANO kwa mwezi. Leo kila siku kuna mikutano mikubwa si pungufu ya MIWILI kila siku. Mikutano hii inaleta wachambuzi, wanazuoni na wataalamu pamoja. Hawa ni aghalabu kuwapata katika mikutano ya hadhara ya kufanyika kwenye maeneo ya hadhara.

Wandugu nimeleta mambo mchanganyiko kidogo lakini kimtiririko. Ni mengi kwa tabia zetu za kutopenda kusoma.

Naomba sana tuone umuhimu wa kufuatilia haya na kusambaza kwa wengine ili tuiokoe nchi yetu na watu wake.

CCM imeshindwa: twendeni tuwasaidie kutoka salama.

Na
Mwl. Basil Lema
Kwa taifa langu na MUNGU wangu
 
Keyboard nyepesi sana bwana basil.

Siasa ya kuandika sio siasa ya field.

Ushauri tu unga juhudi mkono kama wenzio
 
Keyboard nyepesi sana bwana basil.

Siasa ya kuandika sio siasa ya field.

Ushauri tu unga juhudi mkono kama wenzio
Walioonfoka walikuwa wagumu kuliko hawa. CCM haijaifikia USSR brother.
CCM haijaifikia Ujerumani na Berlin Wall yake.
Wanaoota ndoto kwamba CCM ni unbeatable endeleeni hivyo hivyo.
Hofu yangu ni kuwa hamtapata muda wa kujadiliana "imeondokaje* kwa sababu hata yenyewe haijui "itaondokaje".
 
Walioonfoka walikuwa wagumu kuliko hawa. CCM haijaifikia USSR brother.
CCM haijaifikia Ujerumani na Berlin Wall yake.
Wanaoota ndoto kwamba CCM ni unbeatable endeleeni hivyo hivyo.
Hofu yangu ni kuwa hamtapata muda wa kujadiliana "imeondokaje* kwa sababu hata yenyewe haijui "itaondokaje".
CCM ipo kwenye mwamvuli wa NEC, polisi na TISS
 
Unajisumbua Tu.

Na labda ni uchanga wako kwenye siasa , watafute akina Mabere Marando, Akina Mbatia waulize uhalisia
 
Na mwambie Ccm imejaza hao watu wao huko Upinzani 90%

Hivi Mtu anidanganye Eti Salimu Mwal ni Cdm😆😆

Ovaa!
 
Pamoja na kuandika makala ndefu... Naomba tu nikwambie kwa nchini Tanzania makundi yote uliyotaja yapo ila hayapo serious make yapo chini ya umiliki wa ccm!
 
Umeandika kweli kabisa, kadiri ccm inavyozidi kupoteza ushawishi kwa umma, ndivyo inavyozidi kufanya siasa chafu kwa kushirikiana na vyombo vya dola. Na kwa bahati mbaya wanashindwa kuukubali ukweli kuwa kizazi hiki sio cha ccm, hivyo ni vyema wakubali kushindana kihalali wapate ushindi watakaopata kihalali, kuliko kulazimisha kukaa madarakani kwa shuruti, kwani inaweza hata kupelekea machafuko.
a walikuwa wagumu kuliko hawa. CCM haijaifikia USSR brother.
CCM haijaifikia Ujerumani na Berlin Wall yake.
Wanaoota ndoto kwamba CCM ni unbeatable endeleeni hivyo hivyo.
Hofu yangu ni kuwa hamtapata muda wa kujadiliana "imeondokaje* kwa sababu hata yenyewe haijui "itaondokaje".
 
Back
Top Bottom