CCM imeshashinda Zanzibar hata kabla ya Uchaguzi 2010!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Kwa vile Uchaguzi wa 2010 bado, kuandika kuwa CCM imeishashinda, Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, itaonekana kama ni utabiri, huu sio utabiri bali ni mwelekeo halisi wa kitakachotokea kutokana na kinachoendelea sasa kwa mujibu wa historia ya siasa za Zanzibar.

Nikiwa Sekondari ya Tambaza miaka ile, hakuna cha kuchagua masomo ya sayansi wala arts, ni kusoma yote mumo kwa mumo. Nlipomaliza nikajikuta combi zote zimekubali, kuanzia PCM, PCB, PGM,EGM, ECA, CBG, HGE, HGK, NA HGL, mimi nilichagua HGL kwa sababu tuu ya kulipenda somo la Historia na kijiunga Ilboru.

History is the study of the past in relation to the present to determine the future. Yaani Historia ni somo la kuangalia mambo ya zamani na kuyahusianisha na mambo ya sasa ili kujua mambo yajayo. Kwa kifupi ni kuangalia tulikotoka tukilinganisha na tulipo ili tujue tunapokwenda.

Historia ya siasa za Zanzibar inaonyesha hakuna ushindi uso hila, tangu ule wa 1963 ulioleta uhuru uliodumu kwa mwezi mmoja, ukafuatiwa na Mapinduzi ambayo yameendesha siasa za kibabe mpaka uliporudi mfumo wa vyama vingi, yanajirudia yale yale ya kabla ya uhuru.

Uchaguzi wa 1995, nilibahatika kuwako Zanzibar, nikayashuhudia niliyoyashuhudia, mwaka 2000 nikawa tena Zanzibar na kuona nilichoona, 2005 nilifanya kusikia nilichosikia, na 2010 ndio nawaelezeni kinachofuatia.

Ili chama chochote kishinde Zanzibar, hakuna ushindi safi wa kwenye kisahani cha chai, ushindi kule ni mbinu ziwe safi au chafu almuradi akeshatangazwa mshindi, mshindwa ni kugojelea miaka mitano mengine.

CCM wana jua mbinu walizotumia 1995, za 2000 na za 2005 zisingeweza kufua dafu kwa 2010, hivyo wana historia wenye kuona mbali, wakalitumia Baraza la Wawakilishi kuwaingiza mkenge CUF kwa kupitisha sheria ya ukaazi ambayo sasa ndio mpini wa ushindi wa CCM Zanzibar na kinachotokea Pemba sasa, ni juhudi za kunyanganyana kisu huku CCM ameshika mpini. CUF kwenye makali, matokeo yake ni CUF kujikata, au kukatwa kwa risasi, vifaru, mabomu ya machozi, maji ya upupu na wengi kuishia magerezani na mshindi ni CCM.

Hivi hao wawakilishi wa CUF walipokubali haki ya msingi ya kikatiba ya kuruhusu Wazanzibari kushiriki uchaguzi, itiwe mfukoni na sheria ya ukaazi, hawakuliona hilo?. Hivi hawakujiuliza "What was the motive behind? Habari ndio hiyo!.

CCM walijua kwa njia ya kawaida hawashindi, wanaitumia sheria ya ukaazi kuhakikisha CUF hawaandikishwi ili hata wapigakura jimbo zima wakibaki wawili, au mbunge amechaguliwa kwa kura moja, huyo huyo mwenye kura moja ndio mshindi , tena mbunge halali wa CCM!.

CUF nadhani somo hilo limeeleweka, ukweli umeanza kujulikana, naona mnachotaka kukifanya Pemba ni kupafanya pawe hapaliki wala hapalaliki, ama hapakaliki wala hapatawaliki. Ingekuwa ni enzi za Zambibar huru, CUF nanyi mgefanya mapinduzi yenu ya kisiwa cha Pemba na kujitangazia uhuru, lakini sasa Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, mutaletewa majamaa wa UWT, jeshi na Polisi na kudhibitiwa mpaka mtu kwa mtu mkose pa kupumulia ali murad CCM iendelee kutawala.

Kwa maoni yangu, kama hamtaweza kutumia njia halali kukifuta kipengele cha sheria kandamizi ya ukaazi, hesabuni uchaguzi 2010 umeisha, jikusanyeni, mjipange upya kwa 2015 tena ziwe enzi za kina Juma Duni sasa maana Wazee waacheni wapumzike.
 
Last edited by a moderator:
Wakiwa Tanganyika (Mafia au Ukerewe) hakuna kuonyesha cheti cha ukaazi. Dhambi ya ubaguzi ndio inayowamaliza.
 
Yaani we umesema kweli kabisa,CUF ni dhofri hali hawana wa kuwasemea.
 
Thanx, umesema kweli, CCM kwa utaratibu wa kawaida zanzibar na pemba hawawezi kushinda. Ndio maana kutumia dola ni muhali. Walishasema tangu zamani kwamba CUF hawatakujatawala visiwani, ati wao kazi yao ni kutizama tu na kulialia. CCM wamepewa majina kibao lakini wao huchekelea tu, maana hakuna awezaye kuwatoa, wnajua sana kuongea lakini hawawezi kutenda ila kwa kebehi. Bahati mbaya wananchi wa kawaida ndio wanaoumia.

Sio Visiwani tu, hata bara ni vivyo. Angalia wanavyojibadili majina kila kukicha na kujitungia sheria. Ndani yao CCM wapo wakweli ambao sasa wanapigwa vita sana. Subiri bunge lijalo. Maji ya kujisuza yamekauka. Kumwondoa spika anayewawekea kiwingu wameshindwa, sasa wanamtishia nyau kila mccm mbunge atakayesema anauchukia ufisadi. Bahati mbaya anti-ufisadi wako ngangari mno wala hawaogopi nyau.
 
Ubaguzi ni kitu kibaya sana I respect Nyerere alielezea kwa undani zaidi.

Hao wazenj huku Tanganyika wanaishi kwa hivo vitambulisho vyao?
 
Ni kweli. Napenda hiyo hoja kwamba Zanzibar walipata uhuru uliodumu kwa mwezi mmoja, ukafuatiwa na Mapinduzi ambayo yameendesha siasa za kibabe hadi leo..
 
Wakiwa Tanganyika (Mafia au Ukerewe) hakuna kuonyesha cheti cha ukaazi. Dhambi ya ubaguzi ndio inayowamaliza.
.
Kitambulisho cha ukaazi ni kazi ya wanasiasa wanahistoria waliopina tulikotoka, tulipo na kuona mwelekeo wa tunakokwenda, CUF wamepigwa bao la kisigino, wameamua Pemba kusikalike.
 
Hicho kitambulisho kitatumika hata huko Tanganyika ,eleweni tu kinachofanywa na CCM Zanzibar basi pia kitafanyika Tanganyika.Kwani kifo cha CCM kimeenea Tz nzima ,ili kuwepo madarakani kwa CCM ni lazima watumie ubabe ,jiandaeni kama WaPemba.
 
Wakiwa Tanganyika (Mafia au Ukerewe) hakuna kuonyesha cheti cha ukaazi. Dhambi ya ubaguzi ndio inayowamaliza.
Dhambi ya ubaguzi haitawaacha salama. Nafikiri kwa sasa waache siasa. Waanze kuongelea issue ya mafuta maana ndio inayowapa umoja. Mambo mengine ni kizungumkuti kwao
 
Back
Top Bottom