CCM imeruka maji ikakanyaga tope. Sophia na Shaka ni "light materials" majukwaani!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Inawezekana laana za "wabaya"sasa zimeanza kufanya kazi yake ndani ya CCM hii.kama mmefikia kujiita Chawa wa Taifa!

Halafu mnaamini Kwamba Sophia atakuwa bora majukwaani,katika kipindi ambacho Siasa za majukwaani zinaenda kuanza rasmi.

Na kwamba atamzidi Shaka aliyekuwepo? Ambaye hata yeye alikuwa ni mwepesi kama cream ya uso! Muda utaongea soon!

Tatizo ni kwamba CCM mnaishi kwa kukariri! Juzi sio jana, na jana sio leo. Na pia leo haitakuwa hivi mpaka 2025 au 2030!

Watu sasa hawaangalii majina ya wanasiasa. Bali watu wanamsikiliza mtoa hoja na sera makini, na inayogusa kile wanachokiishi huku site!

Maana tumejua rasmi kwamba,wengi wa wanasiasa ndani ya CCM. Mpo hapo kwa maslahi yenu na makundi yenu ya kimfumo.

Msidhani ni wakati ule wananchi walipokuwa wakishabikia vyama kama timu za mpira!

Kwamba yeyote atakayewekwa,ilimradi amesajiliwa na timu,basi atashangiliwa pia na wananchi, La hasha!

Mambo yamebadilika sana,tumejifunza mengi sana! Mnapobadilishana vyeo kama magari, mnapobadilishana bila kutafakari ni nani anaweza nini?

Na anaweza kwa kiasi gani kulisimamia jukwaa na kuongea na wananchi kwa kujua nini hasa wanakihitaji!

Mnapobadili viongozi, kwa kuangalia wanaowafaa nyinyi, kwa maslahi yenu.
Badala ya kuchagua kwa kuangalia wanaowafaa wananchi, kwa maslahi yao na maendeleo ya taifa letu!

Inaweza kuwa ndio anguko lenu linaanza kujitokeza.

Sio kwa hali hii,ambapo tunaona ufisadi ukirudi na kuitafuna CCM, kama ilivyokuwa kabla ya 2015.

Kama hamuamini,tumieni mfano wa kilichotokea juzi huko Mwanza,kati ya Mkurugenzi wa jiji, na kamati ya ulinzi na usalama mkoa.

Tangu siasa za 2015 huko upinzani na pia CCM,hadi 2020! Na kuja mpaka tulipo sasa!

Wananchi wamejifunza mengi sana kutoka matendo ya nyinyi viongozi wa kisiasa nchi hii.

Wameujua ukweli na uhalisia wenu kimatendo na nafsi zenu!

Tumewajua wauaji, tumewajua wezi,tumewajua wanasiasa CCM wanafiki na pia tumewajua wanasiasa wazuri,ambao wanabaniwa na vyama vyao.

Kwa sababu ya ukweli na uzalendo wao.

Kwa hiyo msitarajie wananchi kukurupukia mikutano,ambayo itakosa sera madhubuti ili kugusa utatuzi wa kero zao za kimaisha ya kila siku.

"Wananchi wanalia na mfumuko wa bei,pamoja na Tozo lukuki zinazowafilisi kila uchao huko mitaani."

"Wananchi wanalia na huduma mbovu za kijamii, kuanzia hospitalini mpaka Polisi na ofisi zote nyeti za Umma"

Wakati nyinyi mnagawiana magari ya kifahari ya milioni 500 kwa milioni 600. maofisini,mikoani hadi wilayani.

Wananchi nao wanataabika kuanzia mikoani hadi vijijini. Kwa mfumuko wa bei,ambao hauhusiani hata na vita ya Ukraine na Russia.

Nyama ya Ng'ombe,Mchele,Unga wa Mahindi ni mifano tosha wa hilo.

Tunawasubiri majukwaani na tutawapimia huko. Na pia majibu mtayapata huko huko.

Ilimradi msikae kwa kutegemea maguvu ya Dola mlioishikilia kwa sasa!
Kuweni fair na muache wananchi wawe huru kuamua mbichi na mbivu.
Jumapili njema!

Alamsikhi.
10101.
View attachment 2481544
 
Siasa za majukwaani zinaenda kuanza lakini haitarajiwi ziwe za kuvuka mstari mwekundu, na kuvunjiana heshima, adabu na yote ya aina hii, Dr. Samia is a very polite woman, endapo tutakuwa na hoja zenye staha zisizovuka mstari mwekundu, endapo zitavuka ndipo watamtambua kwa rangi zake!
 
Siasa za majukwaani zinaanza lakini sio za kuvuka mstari mwekundu, na kuvunjiana heshima, adabu na yote ya aina hii, Dr. Samia is a very polite woman, ukitaka mstari mwekundu usio na staha, ndipo watamtambua kwa rangi zake!
Hakunaga siasa za staha wewe , mnajidanganya tuuu , kutukanwa kupo tuu ... Huyo katibu mwenezi wa kike sjui ataongea nn wanaume waache kazi wamsikilize
 
Inawezekana laana za "wabaya"sasa zimeanza kufanya kazi yake ndani ya CCM hii.kama mmefikia kujiita Chawa wa Taifa!

Halafu mnaamini Kwamba Sophia atakuwa bora majukwaani,katika kipindi ambacho Siasa za majukwaani zinaenda kuanza rasmi.
Na kwamba atamzidi Shaka aliyekuwepo?
Ambaye hata yeye alikuwa ni mwepesi kama cream ya uso!
....muda utaongea soon!

Tatizo ni kwamba CCM mnaishi kwa kukariri!
Juzi sio jana,na jana sio leo.Na pia leo haitakuwa hivi mpaka 2025 au 2030!

Watu sasa hawaangalii majina ya wanasiasa.
Bali watu wanamsikiliza mtoa hoja na sera makini,na inayogusa kile wanachokiishi huku site!

Maana tumejua rasmi kwamba,wengi wa wanasiasa ndani ya CCM. Mpo hapo kwa maslahi yenu na makundi yenu ya kimfumo.

Msidhani ni wakati ule wananchi walipokuwa wakishabikia vyama kama timu za mpira!

Kwamba yeyote atakayewekwa,ilimradi amesajiliwa na timu,basi atashangiliwa pia na wananchi,
La hasha!

Mambo yamebadilika sana,tumejifunza mengi sana!
Mnapobadilishana vyeo kama magari,mnapobadilishana bila kutafakari ni nani anaweza nini?
Na anaweza kwa kiasi gani kulisimamia jukwaa na kuongea na wananchi kwa kujua nini hasa wanakihitaji!

Mnapobadili viongozi,kwa kuangalia wanaowafaa nyinyi,kwa maslahi yenu.
Badala ya kuchagua kwa kuangalia wanaowafaa wananchi,kwa maslahi yao na maendeleo ya taifa letu!

Inaweza kuwa ndio anguko lenu linaanza kujitokeza.

Sio kwa hali hii,ambapo tunaona ufisadi ukirudi na kuitafuna CCM, kama ilivyokuwa kabla ya 2015.

Kama hamuamini,tumieni mfano wa kilichotokea juzi huko Mwanza,kati ya Mkurugenzi wa jiji,na kamati ya ulinzi na usalama mkoa.

Tangu siasa za 2015 huko upinzani na pia CCM,hadi 2020!
Na kuja mpaka tulipo sasa!

Wananchi wamejifunza mengi sana kutoka matendo ya nyinyi viongozi wa kisiasa nchi hii.

Wameujua ukweli na uhalisia wenu kimatendo na nafsi zenu!

Tumewajua wauaji,tumewajua wezi,tumewajua wanasiasa CCM wanafiki na pia tumewajua wanasiasa wazuri,ambao wanabaniwa na vyama vyao.
Kwa sababu ya ukweli na uzalendo wao.

Kwa hiyo msitarajie wananchi kukurupukia mikutano,ambayo itakosa sera madhubuti ili kugusa utatuzi wa kero zao za kimaisha ya kila siku.

"Wananchi wanalia na mfumuko wa bei,pamoja na Tozo lukuki zinazowafilisi kila uchao huko mitaani."

"Wananchi wanalia na huduma mbovu za kijamii,kuanzia hospitalini mpaka Polisi na ofisi zote nyeti za Umma"

Wakati nyinyi mnagawiana magari ya kifahari ya milioni 500 kwa milioni 600. maofisini,mikoani hadi wilayani.

Wananchi nao wanataabika kuanzia mikoani hadi vijijini.kwa mfumuko wa bei,ambao hauhusiani hata na vita ya Ukraine na Russia.

Nyama ya Ng'ombe ni mfano tosha wa hilo.

Tunawasubiri majukwaani na tutawapimia huko.
Na pia majibu mtayapata huko huko.

Ilimradi msikae kwa kutegemea maguvu ya Dola mlioishikilia kwa sasa!
Kuweni fair na muache wananchi wawe huru kuamua mbichi na mbivu.
Jumapili njema!

Alamsikhi.
10101.
In CCM there is nobody who is heavy in game
 
Hakunaga siasa za staha wewe , mnajidanganya tuuu , kutukanwa kupo tuu ... Huyo katibu mwenezi wa kike sjui ataongea nn wanaume waache kazi wamsikilize
Hapo sasa,inafikia mahali unashindwa kuelewa akili ya mwenyekiti inashauriwa na akili ya nani mwingine?
 
Acha kujichanganya na kujidanganya mwenyewe,ach kuota ndoto ukiwa umekaa kwenye daladala.

Napenda kukuambia kuwa CCM bado Ni chama imara Sana,madhubuti,shupavu , chenye mvuto wa kipekee na chama kiongozi hapa nchini na mfano wa kuigwa Barani Afrika,CCM ndio chama pekee chenye Sera na ajenda za kugusa wananchi ,Ni chama chenye dira na muelekeo unaoeleweka,Ni chama chenye misingi imara, Ni chama chenye mizizi mpaka mashinani iliyo imara na imara,

Hakuna chama chenye uwezo wa kuitikisa CCM kisera ,kiajenda,kiitikadi na kihoja,CCM imesheni na kuwa na vitu vyote hivyo,uchapa kazi wa CCm na serikali Yake umeifanya CCM kukaa katika mioyo ya watanzania,kuungwa mkono na kutetewa na watanzania, CCM ndio Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo,Ndio chama kilicho na uchungu na maisha yao, ndio chama kinachojuwa Mahitaji ya watanzania,ndio chama kinachoongoza mapambano ya kumtetea mnyonge bila kuchoka,Ni sauti kwa wasio na sauti na nguvu kwa wasio na nguvu kwa wasio na nguvu, ni mdomo wa watanzania na ulimi wa wenye shida.

Mama Sophia Mjema Ni mama Wa shoka na imara,Ni shupavu na madhubuti,Ni Hodari na Jasiri Sana,Atawasha Moto majukwaani mpaka upinzani utakimbia kimvuli chake,Atayatetemesha majukwaa mpaka upinzani utakimbia kishindo chake,atateka anga la Siasa za Tanzania mpaka upinzani utapotelea gizani hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa upinzani wa nchi hii Ni wa usaka tonge na mkusanyiko wa watu wasio na muelekeo Wala dira inayoeleweka
 
Hakunaga siasa za staha wewe , mnajidanganya tuuu , kutukanwa kupo tuu ... Huyo katibu mwenezi wa kike sjui ataongea nn wanaume waache kazi wamsikilize
Kwani wewe huna mzazi wa kike nyumbani kwenu? Hujawahi kukaa kumsikiliza? Hajawahi kukulea? Kukuzaa? Kukukuza? Kukuelekeza? Kukufundisha? Kwani jukwaani watu wanasikiliza hoja au wanaangalia jinsia? Watu wanasikiliza Sera na ajenda au wanaangalia sura? Watu Wana fuata na kusikiliza ajenda zinazowagusa au wanaangalia jinsia? Ndio maana upinzani mnadharaulika na kupuuzwa Sana na watanzania,ndio maana hamna ushawishi wowote ule kwa watanzania
 
Acha kujichanganya na kujidanganya mwenyewe,ach kuota ndoto ukiwa umekaa kwenye daladala.

Napenda kukuambia kuwa CCM bado Ni chama imara Sana,madhubuti,shupavu , chenye mvuto wa kipekee na chama kiongozi hapa nchini na mfano wa kuogwa Barani Afrika,CCM ndio chama pekee chenye Sera na ajenda za kugusa wananchi ,Ni chama chenye dira na muelekeo unaoeleweka,Ni chama chenye misingi imara, Ni chama chenye mizizi mpaka mashinani iliyo imara na imara,

Hakuna chama chenye uwezo wa kuitikisa CCM kisera ,kiajenda,kiitikadi na kihoja,CCM imesheni na kuwa na vitu vyote hivyo,uchapa kazi wa CCm na serikali Yake umeifanya CCM kukaa katika mioyo ya watanzania,kuungwa mkono na kutetewa na watanzania, CCM ndio Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo,Ndio chama kilicho na uchungu na maisha yao, ndio chama kinachokuwa Mahitaji ya watanzania,ndio chama kinachoongozwa mapambano ya kumtetea mnyonge bila kuchoka,Ni sauti kwa wasio na sauti na nguvu kwa walio na nguvu kwa wasio na nguvu, ni mdomo wa watanzania na ulima wa wenye shida.

Mama Sophia Mjema Ni mama Wa shoka na imara,Ni shupavu na madhubuti,Ni Hodari na Jasiri Sana,Atawasha Moto majukwaani mpaka upinzani utakimbia kimvuli chake,Atayatetemesha majukwaa mpaka upinzani utakimbia kishindo chake,atateka anga la Siasa za Tanzania mpaka upinzani utapotelea gizani hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa upinzani wa nchi hii Ni wa usaka tonge na mkusanyiko wa watu wasio na muelekeo Wala dira inayoeleweka
Kwanza nikwambie ukweli kwamba mimi sio chawa kama wewe!
Mimi siweki namba ya simu kutafuta uteuzi.
Mimi ninaandika kulingana na uhalisia bila kutaka kumfurahisha mteuzi.Ninaandika kile ambacho tuna kiishi kama CommonWananchi huko site.

CCM imara ni ile ambayo inakuwa ndani ya mioyo ya wananchi na wanachama wake.

Na si hii inayokuwa ndani ya mioyo ya walamba asali na Machawa wa chama kama wewe Lucas mwashambwa !

Huenda unatarajia kupitia njia aliyopitia Kafulira,lakini tatizo Ma-Chawa mmekuwa wengi kuliko hata mahitaji ya mnaemsifia na kumpamba kwa unafiki.

Labda siku akitoa ule mtandio na akaweza kuona pembeni vizuri,ndio atagundua mlipokuwa mnampeleka sio sahihi.
Lakini inawezekana ikawa too late.
FB_IMG_1673119654191.jpg
 
Kwani wewe huna mzazi wa kike nyumbani kwenu? Hujawahi kukaa kumsikiliza? Hajawahi kukulea? Kukuzaa? Kukukuza? Kukuelekeza? Kukufundisha? Kwani jukwaani watu wanasikiliza hoja au wanaangalia jinsia? Watu wanasikiliza Sera na ajenda au wanaangalia sura? Watu Wana fuata na kusikiliza ajenda zinazowagusa au wanaangalia jinsia? Ndio maana upinzani mnadharaulika na kupuuzwa Sana na watanzania,ndio maana hamna ushawishi wowote ule kwa watanzania
Mambo ya mzazi wa kike yanakujaje , mwanaume mzima unauza akili Kwa uchawa si Bora ukalime matikiti
 
Kwanza nikwambie ukweli kwamba mimi sio chawa kama wewe!
Mimi siweki namba ya simu kutafuta uteuzi.
Mimi ninaandika kulingana na uhalisia bila kutaka kumfurahisha mteuzi.Ninaandika kile ambacho tuna kiishi kama CommonWananchi huko site.

CCM imara ni ile ambayo inakuwa ndani ya mioyo ya wananchi na wanachama wake.

Na si hii inayokuwa ndani ya mioyo ya walamba asali na Machawa wa chama kama wewe Lucas mwashambwa !

Huenda unatarajia kupitia njia aliyopitia Kafulira,lakini tatizo Ma-Chawa mmekuwa wengi kuliko hata mahitaji ya mnaemsifia na kumpamba kwa unafiki.

Labda siku akitoa ule mtandio na akaweza kuona pembeni vizuri,ndio atagundua mlipokuwa mnampeleka sio sahihi.
Lakini inawezekana ikawa too late.View attachment 2481550
Nani akupe uteuzi mtu Kama wewe ambae kila Siku huoni juhudi kubwa zinazofanywa na serikali hii,upate uteuzi ili ukabomoe miradi? Ili ukaharibu huduma? Ili ukatukane wananchi? Ili ukavunje mipango mizuri ya serikali yetu? Huna sofa za kuwa katika serikali yetu Hii tunayoiamini na inayoaminika na watanzania na kuungwa mkono
 
Mambo ya mzazi wa kike yanakujaje , mwanaume mzima unauza akili Kwa uchawa si Bora ukalime matikiti
Wewe kwa akili yako hiyo si umeeleta habari za jinsia ? Kwa hiyo kwa akili yako ulitaka upewe majibu gani? Au unataka wanaofanana akilinna wewe waje wakupongeze
 
Lucas kama lucas mwashambwa!

Wakati Mwingine tumia akili mkuu!!

Sasa mjema ana mzidi Nape au pole pole kwa ushawishi!?

Nina nadharia Mbili;-

1.Mama anataka kuiua ccm kwa kuipunguzia umaarufu Baada ya kuona hana nafasi ya kugombea urais 2025!!!hivyo UPINZANI wachukue kijiti!!

2.Mama ameamua kuwakomesha wapinzanit ndani ya chama kwa kukataa pendekezo lao Ili amuweke incompetent asimfunike JUKWAANI kisiasa!!

3.Amechoka sasa amebutua kopp la kombolela mwenye kupata apate mwenye kukosoa akose!

4.kaamua kumlinda shaka Ili upepo wa mikutano ya hadhara usi m expose kijana wake kateua wa Bara Ili tuaibike kisiasa NDANI ya CHAMA!!!

"Mawazo huru haya toka KWA mlipa kodi makini na mwanaccm mwenye itikadi za nyerere,Butiku,kawawa,Warioba na vijana wa TANU!
 
Back
Top Bottom