CCM imepotea kwenye ramani na masikio vimebaki vyombo vya dola kutekeleza ilani na maslahi yao

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Najiuliza CCM imepotelea wapi? Chama dola kimepotea kwenye ramani ya siasa nakuviachia vyombo vya dola vimefanye kazi kwa niaba yao.
Chama dola ambacho hata viongozi wake wa mkoa na hata Taifa hawafahamiki kwa wananchi, kwanini mmefikia hapa?

Chama dola ambacho kimepwaya kujibu hoja badala yake kimeruhusu hoja kujibiwa kwa ukamataji wa watoa hoja na kuwafunga midomo

Chama dola ambacho hata kushawishi watu kujiunga nao ni watu hao wapewe nafasi za uongozi au wapewe madaraka ndio wajiunge.

Chama dola ambacho kinashuhudia spika akivunja sheria iliyowazi na iliyokinyume na misingi ya chama lakini akisemi.

Chama dola ambacho kimehalalisha rushwa ya madaraka na kufungua milango ya uonevu kwa kila mwenye mawazo mbadala. Chama hiki kwanini kimeamua kufa kifo Cha fikra na kubaki na fikra zakushikiliwa na kundi flani la watu?

Chama ambacho hakina vijana wajenga hoja kina vijana watukanaji, chama ambacho kila Jambo la maendeleo linalotoka nje ya mfumo wa linaitwa ubeberu.....

Naitafuta ccm ya mwalimu na vijana wake imepotea imebaki ccm ya dola ambayo siyo ccm iliyozaliwa mwaka 1977 Bali hii ni ccm isiyokuwa na itikadi wala dira.
 
We umekurupuka kutoka Igabiro mjini Kagera?

Ccm inatumia vyombo vya dola kufanya kazi zake kwa namna gani? Maana kama serikali ya Ccm inatumia polisi kudhibiti na kukamata wahalifu, inatumia Pccb kudhibiti rushwa na ubadhirifu, Inatumia askari magereza kufundisha wahalifu ili wajirekebishe hapo tatizo lipo wapi? Au hujui maana ya chama dola?

Unasema viongozi wa mikoa na taifa hawajulikani. Yaani ina maana watu wa Mwanza hawamjui mwenyekiti wa Ccm mkoani mwanza? Hawamjui Dk Bashiru kama katibu mkuu. Hawamjui JPM kama mwenyekiti taifa?

Unadai kuna watu wanatoa hoja alafu wanakatwa bila hata kuwataja. Ni hoja gani hizo walizitoa?

Unadai Ccm haina ushawishi wa kujiunga na chama chao. Na hao wabunge na madiwani waliohamia Ccm toka Chadema haujawaona?

Unadai kuna rushwa matumizi ya madaraka ni kiongozi gani wa Ccm? Ambae alishatumia hayo madaraka vibaya kujinufaisha ambae wewe unaushahidi?

Unamtuhumu spika kukiuka taratibu. Je, ni ofisi gani ya serikali ambayo inafanya kazi bila kufuata formalities?

Hao ndugu zako wanakesha humu Jf wanatukana matusi huwaoni. Au unaleta mada ili kujifurahisha.
 
Naitafuta ccm ya mwalimu na vijana wake imepotea imebaki ccm ya dola ambayo siyo ccm iliyozaliwa mwaka 1977 Bali hii ni ccm isiyokuwa na itikadi wala dira.
Muwahi Mzee Mang'ula ...... hao ndio waliobaki lakini hawatakiwi kwani ni wakweli na wa haki, wanavuruga 'kasi' ya kazi za akina Bashite.
 
1589467681960.png
 
Nimeamini kuwa,Siasa ni Jambo moja gumu saaana,

Kwa nini!

Ni pale unapolazimika kuidhurumu nafsi Kwa kulazimisha ukweli wa nafsi ufunikwe na uwongo, na uwongo kuwa faraja ya nafsi isyotaka uwongo, tukisema watu huwa wanajitafutia vidonda vya tumbo, ndio kama hivi,

Mnakazi kwelikweli wanasiasa, Okey, yetu macho
 
Uroho wa madaraka umepelekekea kutamani mfumo wa China, wenzao China wana tech, wana akili, wanadespline
 
October kuna mtanange ambao utaleta jibu nani anafaa. Kwani hujamuelewa jamaa?
Nimetoka huko kwenye wizi mimi nakumbuka wakati niko Segese tulikuwa tunampigia kampeni lakini hafai

Tokea nihamie upinzani nimegundua mengi ccm kinaliangamiza taifa na wamechagua muhamiaji haramu kuwa mwenyekiti
 
Nimetoka huko kwenye wizi mimi nakumbuka wakati niko Segese tulikuwa tunampigia kampeni lakini hafai

Tokea nihamie upinzani nimegundua mengi ccm kinaliangamiza taifa na wamechagua muhamiaji haramu kuwa mwenyekiti
Kwa hiyo ulikuwa unakula mpunga wa Maige?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom