Tuwasaidie CCM, wapo katika vita ya ndani (CCM kwa CCM) na vita ya nje (CCM na Watanzania)

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Ni dhahibi kwamba Ccm chama cha siasa kikongwe kuliko vyote vilivyopo Tanzania, sasa kiko katika vita ya ndani (ccm kwa ccm) na vita ya nje (Ccm na Watanzania).

Kwa ndani wana ccm wanashambuliana mercilessly wakipigania itikadi kinzani. Wako wachache wenye nguvu wanaotetea ufisadi na kuupamba, kuuhalalisha na wapo wanaopigania uadilifu kwa maslahi ya Watanzania walio wengi. Wakati wengine wakipambania kambi za godfathers ili waendelee kuwa ndani ya mifumo, wengine wanaingia vitani kupigania dini, huku wengine wakipingania uzanzibar na utanzania.

Upande wa vita vya nje, Watanzania wanaishambulia CCM kwa kung'ang'ania uongozi wakati imeishiwa pumzi, inawasaliti watanzania, inawafanya watumwa katika nchi yao, inawahadaa na kuwatumia na kuwatumikisha kwa maslahi ya ustawi wa CCM

Hapa tunachotaka, tuwasaidie ccm kwa kuwapa mbinvu za vita na kupigana vita vyao bila ku commit war crimes. Mimi naanza kama ifuatavyo:-

1. Waache kutumia vyombo vya ulinzi na mihimili mingine kama shield kwa kuwa hivyo si property ya CCM bali ni vyombo vya waTanzania wote bila kubagua. Kuendelea kuvitumia ni kuingiza mihimili mingine kwenye uhalifu wa kiutendaji, kuvidhoofisha, na kuvitenga na Watanzania na sote tuna jua nini maana ya kukosekana thamani ya vyombo hivyo machoni pa umma.

2. Waache kuwatishia watu kwamba atakayewakosoa watamtesa kwa sababu huo ni ugaidi.

3. Waondoe mentality ya kuona kila mwenye hoja tofauti na mwingine ni adui kwa sababu ni kugandamiza fikra za watu na kujinfaya kwamba CCM tu ndio kuna mawazo bora kitu ambacho ufisadi wa kutisha na hatua duni za maendeleo kwa miaka 60 zinathibitisha sivyo.

4. Tabia ya kupinga kelele kila mwenye malalamiko dhidi ya utendaji wa ccm, ama serikali ama dola kwamba "wanaichafua nchi, wananajisi nchi, wauawe, wakamatwe, wapotezwe n.k", ni uvunjaji wa katiba na ni kutangaza vita ya ndani ambayo mshindi wake si ccm wala wa Tanzania.

5. Wajifunze kuelewa kwamba ccm imeharibu mifumo ya elimu nchini makusudi ili kujenga taifa la watu wengi wasiokuwa na ufahamu viwango vya kujenga na kusimamia mstakabari wa taifa kitaifa na kimataifa, na hao ndio watakao imaliza ccm kwa sababu they can not think rationally. Hao ndio hao wanapiga makofi kila kinachosemwa na kambi zao bila kufikiri, wanasema "asurubiwe, asuribiwe, asuribiwe", kila mwenye mawazo mbadala, na wanakuja kushtuka kwenye athari za matokeo ya makofi yao, na hawana uelewa wala uwezo wa kurekeisha wanabaki kulalama.

6. Wajue kwamba Watanzania walikwisha wachoka siku nyingi na hivyo hawatakiwi tena kuongoza nchi kwa sababu hawan uwezo, unless, warudi kwenye drawing table wajipambanue walipochochora, badala ya janja janja.

7. Waelewe Tanzanai ni ya Watanzania wote, hiyov wanapokuwa katika uongozi, wasijimilikishe nchi, bali wajenge mifumo itakayosimamia ustawi wa taifa vizazi vyote vijavyo katika maeneo yote. Ukimbizini hata ukiwa nyapala, wewe ni mbwa koko.

8. Waache woga wa mabadiliko katiak nchi kwa kuwa hiyo itakuwa njia sahihi kwa maisha ya kila mtu including vizazi vyao. Tunaona hii ya ugaidi wa mbowe, mara wabunge wasio na chama bungeni kinyume cha katiba, mara, kudhikisha viongozi na wenye itikadi tofauti n.k. ni hofu ya mabadiliko ndani ya ccm ambayo hayana budi kuja. Kama sileo kesho yaja. Ni afadhali kujipanga na kuyaongoza ipasavyo ili yafanyike katika hali sahili kulilko yaje kuwaburuza bila mpangilio.

9. CCM inaonyesha uroho wa madaraka usio na kipimo, kwa sababu imezoea ku override mifumo na kufanya watakalo bila kujali sheria wala katiba ya nchi. Uhuru huo ni zaidi ya ukoloni. Lakini pia ni kutaka kulinda uvundo ambao serikali nyingine ikja itausafisha, na pia kwa sababu ya kukosa weledi, makada wengi wa chama hivyo hawajui namna nyingine ya kuishi nje ya kuwa mpiga debes wa chama tawala. Lakini haya yote huwa si endelevu.

10. Acheni kuwadhikisha wapinzani kwa kusema wana uroho wa madaraka wakati ninyi ndio mnathibitisha zaidi ya uroho wa hayo madaraka. Ruhusini watalaam watengeneze mifumo sahihi ya maisha sahihi kwa kila Mtanzania hata akiwa nje ya utawala ama ccm.

11. Kumbukeni Watanzania ni wengi kuliko ninyi na nguvu minazozitegemea, ha hivyo mafanikio yenu katika vita vyenu yako katika msingi wa "Kuwaheshimu Watanzania", na si "Kuwalaghai ama kuwadhikisha".

Mwenye lingine, ndugu zangu, tuwasaidie.
 
Back
Top Bottom