CHADEMA kuweni makini, mnademka sana na ngoma za CCM

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
396
717
Assalam wanajamvi! poleni na majukumu ya kila siku ya kujikwamua kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni!

Niende moja kwa moja kwenye hoja, neno kudemka lilipata umaarufu miezi kadhaa likiwa na maana ya kucheza sana ngoma inayopigwa, ndugu zangu CHADEMA mnademka sana et sasa mpo huru sasa mnafanya mtakavyo, mmeachiwa. Huku ni kudemka kwenyewe.

Chochote kinachofanywa na chama cha mapinduzi kinapangwa, ukiona sabaya amekamatwa kimepangwa, na wanajua kwanini wamefanya hivyo. Kamati zao za usiku ndo zimekuja na hio ripoti, mkamateni sabaya kwa mikwara yote mmtie ndani, huko alipo hamjui anaendeleaje.

Tembeeni na agenda zenu vifuani, niwapeni mfano, Nelson Mandela baada ya kutoka kifungoni na kuwa rais aliweza kwa mamlaka aliyonayo kulipa visasi na kuacha agenda zingine, lakni kifuani alijua amebeba nini.

Nchi hii bado ina katiba ya chama kimoja, nchi hii bado haina tume huru ya uchaguzi, ndugu zangu acheni kudemka, wao wanakesha usiku kwenye kamati zao hawalali wanatafuta mbinu zozote kuwapumbaza, nyinyi mpo na kususa kumpigia Diamond kura za BET, huku ni kudemka, nyie mpo busy na wabunge 19 ambao kiuhalisia bado haijawekwa clear.

CCM ya kina Nzee Nyerere iliwaandaa viongozi wake kijasusi, mnavyowaona kina JK, kina Kinana kina Membe kina Makamba na wengine, wale ni majasusi wa madaraka, wanajua wafanye nini na wapige ngoma kwa style gani, msiamini maneno yao na kusahau kwenu mnakula mlenda kisa bakuli la sahani ya biriani uliopewa usiku mmoja.

Kaeni umizeni vichwa, wabaneni kipindi hiki kwa kutafuta katiba na tume huru, tengenezeni hoja, pingeni kwa hoja acheni porojo, vijana wengi kwa sasa mnaweza kuwakamata wote wakawa wenu, wamechoka na sera tawala, wamechoka na kukosa ajira baada ya kuhitimu, hili ni bomu kubwa sana, ni nyie kulitega tuu na kulitumia, mna mitandao ya kijamiii hii ni ramani tosha ya kutafuta mbinu na kukusanya watu.

Achaneni na Fatma na Maria, hawa wanajua kwanini wanapinga, na hawakamatwi, waulizeni kwa dhati Je, wao ni CHADEMA? acheni kudemka tembeeni na sera zenu, tembeeni na shabaha zenu, mkikomaa sana miaka kumi ni mingi sana kuiongoza nchi hii, lakini mmejiandaa kushika dola?

Niwakumbushe kampeni za lowasa 2015, lowasa ni Jasusi aliepata mafunzo ndani na nje ya nchi hii, mnakumbuka aliyoyafanya? mnakumbuka nusura aue watu kwa presha, watu wakawa mpaka wanatukana lakni jukwaani mzee hata haongei sana, halipi visasi hatukani lakini kishindo chake, hata fedha si kwamba wote walipewa, lakini kishindo chake hadi kijijini kilisikika.

Chongeni plan zenu tumieni hata fedha nyingi kuja na mikakati, watumieni hata majasusi wao kisiri siri, mtatoboa.

Asanteni, narudia tena acheni kudemka, wakati ni ukuta na hua hauna tabia ya kuacha ufa!
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
27,680
31,212
CHADEMA ni CCM tusiyoitaka ambayo haiko madarakani.

wanarukia hayo wakijua kabisa ndiyo yatafanya wandelee kusikika kwa wananchi,maana story za katiba,tume huru,na uhuru wa kujieleza ni blah blah kwa wananchi. Baada ya kudemshwa kwenye kifo cha magufuli na wananchi sasa hawajui washike tete lipi kujiokoa.
kilichobaki ni kudandia kila jambo

jana boss PCCB anatamka bayana hana sababu za kumkamata makonda,bado kuku zinaamini sabaya anafungwa,na zinaimba mapambio ya kusifu kwa mungu wao.

hao mashangazi wana ajenda zao na tawala hizi mbili,nashangaa hawa jamaa zetu wanadanganywa eti ni wanaharakati!!!!
nikikaaga peke yangu huwa najisemea,upinzani tanzania upo,ila sio wa kuitoa ccm madarakani.
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom