CCM imeishiwa pumzi, upinzani upo ICU, nani atuongoze kwenye mapambano ya ukombozi?

Kuna mengi nakubaliana na ww sana kwenye post yako. Na pia nashukuru hili jukwaa limekurudisha kwenye mstari kwa ile tabia yako ya kuisifia ccm eti kwa madhaifu ya cdm. Ninavyoamini mimi cdm ilikuwa kwenye mstari mzuri hata walikuwa wakisema serekali inasikia hata kama haitekekezi. Mahali walipokuja kuchemsha ni kumpokea EL na kumpa nafasi ya juu kabisa ya uongozi. Mwanzoni Mbowe alitaka kutuaminisha kacheza karata yake vizuri, lakini toka mwanzo nilijua na kuonya kwamba ile ni kete mbovu kabisa kuicheza. Hapa tulipo tuko na cdm iliyochemsha kwa kumkumbatia EL chini ya mtazamo wa Mbowe, na ccm inayolazimisha kupendwa na kukubalika chini ya Magufuli.
Mkuu unajua sisi wengine ni wana majeruhi katika siasa za kinafiki ambao mwisho wake tuliona 2015 uchafu uliofanyika CDM! Ila yote ni yote MBOWE amechoka amwachie mwingine atuongoze kwenye mapambano mapya sasa hivi tunamtaka mtu mwenye damu ya ukombozi siyo mwenye tamaa ya kuongoza!

Imetosha imetosha! Tunamtaka mwingine atuongoze kwenye battle field jasiri na mwenye ushwawishi kwa wananchi, mwenye kutuunganisha kiitikadi zetu
 
Nimesoma makala yako nzuri kuhusu maisha ya Raila Odinga kisiasa. Ila umesahau kuelezea mchango mkubwa wa wananchi wa kawaida waliokuwa wanajitokeza kuunga mkono harakati za Raila Odinga na wenzie.

Sisi vijana Tanzania badala ya kuendelea kuwaunga mkono Mbowe na wenzie kudai mabadiliko, tunatumia keyboard za computer zetu kuwashambulia viongozi wanaotaka mabadiliko. Wakina Raila Odinga kama uzi/makala yako walipata nguvu ya kisiasa toka kwa umma bila kukoma. Inaonekana sisi vijana ndiyo tumeishiwa pumzi tunakuwa watazamaji "bubu" walioketi bila kusimama na kushiriki ktk kudai mabadilko ya kisiasa tukisubiri mtego wa "katiba mpya" ipatikane kwa "hisani" ya CCM ndiyo tuingie katika vuguvugu la mabadiliko.
Mkuu unajua kazi ya mpambanaji mkuu! Kazi yake ni kuwa kwenye front time kupinga kila aina ya uharamia lakini kwetu huku yeye ndo kageuka anakumbatia uharamia ujue kuna watu wanafanya kazi upinzani kumzidi ata MBOWE mara elfu! Imetosha imetosha tunamtaka mwingine
 
nafikiri ni vizuri tukitofautisha ilani na sera na wanaozitekeleza, CCM ina ilani na sera imara!muhimu ni kupata viongozi waadilifu kutuongoza na kutumbua walafi bila kuwaonea aibu!
Sio mlafi lakini anabana ajira, uhuru wa kujieleza, sheria za ajabuajabu kibao, huyu hatufai tumuondoe hata kwa damu
 
Tukubali kwanza watu kufa, bila vifo usitarajie kwa sababu yanayodaiwa ni maslahi ya watawala wa sasa (ccm). Inahitaji mtu jasiri na asiogope jela
 
Nimesoma makala yako nzuri kuhusu maisha ya Raila Odinga kisiasa. Ila umesahau kuelezea mchango mkubwa wa wananchi wa kawaida waliokuwa wanajitokeza kuunga mkono harakati za Raila Odinga na wenzie.

Sisi vijana Tanzania badala ya kuendelea kuwaunga mkono Mbowe na wenzie kudai mabadiliko, tunatumia keyboard za computer zetu kuwashambulia viongozi wanaotaka mabadiliko. Wakina Raila Odinga kama uzi/makala yako walipata nguvu ya kisiasa toka kwa umma bila kukoma. Inaonekana sisi vijana ndiyo tumeishiwa pumzi tunakuwa watazamaji "bubu" walioketi bila kusimama na kushiriki ktk kudai mabadilko ya kisiasa tukisubiri mtego wa "katiba mpya" ipatikane kwa "hisani" ya CCM ndiyo tuingie katika vuguvugu la mabadiliko.
Hivi John Heche hawezi kakazi haka mwanawane
 
Tukubali kwanza watu kufa, bila vifo usitarajie kwa sababu yanayodaiwa ni maslahi ya watawala wa sasa (ccm). Inahitaji mtu jasiri na asiogope jela
Tunamuitaji mtu jasiri mwenye uthubutu wa kuhoji na kutegua kila aina ya mbinu chafu! Ambaye hana malsahi ya kibiashara kwenye siasa. Atuongoze kwenye mapambano ya kweli
 
Upinzani Bongo bado sana Ni sawa na mtu anayetamani kwenda mbinguni lakin kufa anaogopa je,huko mbinguni utafika vp Bila kufa
kwanza nikueleweshe kenya ni rahisi kupitisha reforms maana hakuna chama dola kule toka KANU iangushwe hakuna chama kilichojizatiti ndani ya dola na taasisi za serikali hivyo hakuna sana uchama kama huku na ndio maana ni rahisi mapendekezo kukubaliwa shida huku tanzania tuna chama ambacho kina mizizi kwenye kila taasisi imejaza makada ambao hawako tayati kuona chama kikitolewa madarakani na hawa ndio hudhoofisha kila mipango ya upinzani. hilp moja

Nani kaogopa kufa?? mara ngapi mbowe kaongoza maandamano au umesahau yale ya arusha hadi watu kupigwa risasi.... umesahau maandamano ya zenji hadi mkaua watu kibao na mamia kujeruhiwa na kutupwa jela???

shida nyie ni wanafki tulipoitisha UKUTA mlianza kumlaunu mbowe kuwa atasababisha vijana wafe na kuwekwa jela.... then akiacha mnasema MUOGA. Ssa kwa mfano angelazimisha maandamano hta kma mmeyapiga marufuku then watu wengi wangekufa mngemsifia mbowe ni mpinzani wa kweli au mngemuita MUUAJI asiyejali maisha ya wanachadema????

Mbowe licha ya mapungufu aliyonayo kma mwanadam maana akuna aliyemkamilifu kafanya nafasi yake kwa ufanisi propaganda nyingi sana na nguvu kubwa sana ilitumika na dola kukimaliza chama rejea migogoro, propaganda za udini,ukanda,ukabila na ugaidi lakini chama kimeweza kuvuka vihunzi vyote hivo na kuwa imara kuliko wakayi wowote.

Hayo ya katiba sijui uhuru wa vyombo vya habari nafkiri wote mliona mbowe na upinzani kwa ujumla walivyofight kuiteea rasimu ya warioba na walifanya mikutano nchi nzima kuwahamasisha wananchi kuhusu uhuni uliofanywa na ccm kuipora katiba yenye maoni ya wananchi. Ssa ulitaka afanye nni zaidi??? aingi msituni ndo mumuite gaidi na mkifute chama??? Hta siku ya kupitisha sheria ya cybercrime wote tuliona jinsi mkosamali,lissu na mnyika walivyopambana kuwabana ccm kifungu kwa kifungu hadi mwishoni kwa hoja nzito ingawa kwa wingi wao walipitisha kwa mabavu ila watanzania tulio wengi tuliona nia njema walionayo kwa sisi wananchi.
 
Nimesoma makala yako nzuri kuhusu maisha ya Raila Odinga kisiasa. Ila umesahau kuelezea mchango mkubwa wa wananchi wa kawaida waliokuwa wanajitokeza kuunga mkono harakati za Raila Odinga na wenzie.

Sisi vijana Tanzania badala ya kuendelea kuwaunga mkono Mbowe na wenzie kudai mabadiliko, tunatumia keyboard za computer zetu kuwashambulia viongozi wanaotaka mabadiliko. Wakina Raila Odinga kama uzi/makala yako walipata nguvu ya kisiasa toka kwa umma bila kukoma. Inaonekana sisi vijana ndiyo tumeishiwa pumzi tunakuwa watazamaji "bubu" walioketi bila kusimama na kushiriki ktk kudai mabadilko ya kisiasa tukisubiri mtego wa "katiba mpya" ipatikane kwa "hisani" ya CCM ndiyo tuingie katika vuguvugu la mabadiliko.
Yaani kaka unathubutu kumlinganidha Mbowe na raila
Tofauti mmoja ni mpigania mabadiliko mwingine ni mchumia tumbo. Kazi kuanzisha kampeni zisizo kuwa na mwisho mambo ya kushabikia mtu na vyama badala ya uwezo wa mtu na nia yake nzuri hatutafika popote.
 
Kuna mengi nakubaliana na ww sana kwenye post yako. Na pia nashukuru hili jukwaa limekurudisha kwenye mstari kwa ile tabia yako ya kuisifia ccm eti kwa madhaifu ya cdm. Ninavyoamini mimi cdm ilikuwa kwenye mstari mzuri hata walikuwa wakisema serekali inasikia hata kama haitekekezi. Mahali walipokuja kuchemsha ni kumpokea EL na kumpa nafasi ya juu kabisa ya uongozi. Mwanzoni Mbowe alitaka kutuaminisha kacheza karata yake vizuri, lakini toka mwanzo nilijua na kuonya kwamba ile ni kete mbovu kabisa kuicheza. Hapa tulipo tuko na cdm iliyochemsha kwa kumkumbatia EL chini ya mtazamo wa Mbowe, na ccm inayolazimisha kupendwa na kukubalika chini ya Magufuli.
Sina la kuongeza umepoint mada muhimu muhimu.
 
Raila Odinga hakuwahi kuwa tishio kwa Moi miaka ya 80 na tisini mwanzoni.Muda wote huo mpaka anafungwa mwaka 1982 alikuwa chini ya mpinzani wa wakati huo Jaramogi Oginga Odinga, baba yake.

Hivyo kusema Raila Odinga aliongoza kuleta vyama vingi Kenya ni kutoijua historia ya Kenya.Raila alianza kuwika na kuwa kiongozi mwenye ushawishi baada ya kifo cha Baba yake, Jaramogi Oginga Odinga.Kabla ya hapo alikuwa mfuasi wa Baba yake.
 
Back
Top Bottom