CCM imechoka ona hii sasa

CCM imechoka ona hii sasa

Invinsible

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
314
Reaction score
382
TAFAKARI JADIDIFU:-

CCM imechoka, tuitoe! Ikapumzike wajipange upya!!
Just imagine👇👇👇

Tanzania ina ukubwa wa eneo la ardhi (total land area) mita za mraba milioni 364,915. Kenya ina ukubwa wa mita za mraba milioni 224,962, Uganda mita za mraba milioni 91,136, Rwanda mita za mraba milioni 10,169 na Burundi mita za mraba 10,745.

Tanzania peke yake ni kubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zikijikusanya kwa pamoja zinakuwa na jumla ya eneo la mita za mraba milioni 337,012. Wakati Tanzania peke yake ina mita za mraba milioni 364,915.

Kwa hiyo ukiigawa Tanzania utapata nchi 4 zenye ukubwa sawa na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na litabaki eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba milioni 27,903 ambalo linaweza kutengeneza nchi nyingine yenye ukubwa sawa na Togo.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Tanzania ni sawa na nchi tano. Yani Tanzania ni nchi moja yenye nchi tano ndani yake.-

Hivyo basi Rais anayeweza kuongoza taifa hili na kuleta maendeleo lazima awe Rais mmoja lakini mwenye akili za Marais watano. Yani awazidi akili mara tano akina Kenyatta, Museveni, Nkurunzinza na Kagame.

Marais wote wa Afrika Mashariki wanapaswa wakija Tanzania wajione ni kama wakuu wa mikoa. Na ili wajione hivyo lazima kuwe na hatua kubwa za kimaendeleo kuliko kwao.

Yani Kagame akija hapa akikuta treni za umeme (kwake hana), akikuta Hospitali za kisasa watu wanatoka Asia kuja kutibiwa hapa (kwake hakuna), akikuta Barabara za juu ktk miji mikubwa (fly overs), akikuta maslahi mazuri kwa watumishi, akikuta umeme wa uhakika na tunalipa TZS 3000 kwa mwezi, akikuta elimu ni bure kuanzia Shule ya msingi hadi chuo kikuu, lazima ajione Mkuu wa mkoa.

Lakini kama Kagame kwake ana fly overs (sisi hatuna), wanafunzi wa Rwanda wana loptop kuanzia shule ya msingi (sisi hatuna), Elimu ya sekondari bure (sisi tumeshindwa), halafu akituangalia tuna Bandari, madini, gesi, mlima K.njaro, Mbuga za wanyama etc lazima amuone Rais wetu kama "Diwani".-

Jiulize Tanzania yenye rasilimali lukuki ndiyo inayoongoza kwa kukata kodi kubwa (PAYE) kwa watumishi wake kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Serikali kila mwisho wa mwezi inajikusanyia 18% ya mishahara ya watumishi kana kwamba haina chanzo kingine cha mapato zaidi ya kunyonya watumishi.

Rwanda isiyo na rasilimali nyingi kama sisi, watumishi wanalipa 6% kama kodi kwenye mishahara yao.

Yani mtumishi anayelipwa TZS 700,000/= nchini Tanzania anakatwa TZS 108,000/= kama kodi. Wakati mtumishi anayelipwa mshahara kama huo nchini Rwanda anakatwa TZS 36,000/= tu kama kodi.

Rwanda ambayo haina gesi, haina bandari, haina madini inawajali watumishi wake. Tanzania yenye gesi, mlima, madini, bandari haitaki kutoza kodi huko kote badala yake inamnyonya mtumishi kama vile serikali haina chanzo kingine cha mapato zaidi kodi za watumishi.

Hivi "logic" ya kumtoza mtumishi 18% ya kodi ni ipi wakati kuna vyanzo vingi sana vya mapato nchini? Unatoa msamaha wa kodi kwa wawekezaji wa madini, na wachimbaji wa gesi, halafu unakazana kumnyonya mtumishi. Hii ni kukosa akili.

Mwaka huu Tanzania imepoteza jumla ya TZS 4.7 Trilioni kutokana na misamaha ya kodi. Yani karibu robo ya bajeti. Makadirio ya gharama za kusomesha watoto wetu kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu kwa mwaka ni TZS 1.6 Trilioni (kwa mujibu wa Mbatia).-

Maana yake ni kwamba tukipunguza misamaha ya kodi kwa mwaka mmoja tu, tunapata hela za kutosha kusomesha wanafunzi wote wa shule za msingi hadi chuo kikuu kwa miaka miwili. Lakini serikali ya CCM haiwezi kuliona hili kwa sababu ya akili ndogo.

Mtumishi yoyote anayeiunga mkono CCM yafaa akapimwe akili. Imagine wewe ni mwalimu unalipwa 700,000/=. Kodi tu ni 108,000/=, Pensheni 70,000/= (10%), CWT 21,000/= (03%), mwisho wa siku unapokea 498,000/=. Serikali ya CCM inakunyonya bila huruma na wewe unakenua meno kusema "ccm mbele kwa mbele".

Bado hujalipa kodi ya pango, ulipe maji, umeme, ada ya wanao shule, nauli, chakula, mavazi, etc. Hivi kwanini usiwe maskini?? Kwanini usikope kabla ya tar.05?? Hivi unadhani waalimu wanapenda kuwa na "vidaftari" vya mkopo kwenye maduka ya kina mangi? Serikali ya CCM ndio inawalazimisha kudhalilika.

Sasa mwaka huu iwe mwisho. Uwezo wa kufanya mabadiliko uko mikononi mwako. Mchague Lowassa kuwa Rais wako uone mabadiliko. CCM imetutesa miaka 50 sasa yatosha. Let them rest in peace.

Magufuli hana uwezo wowote wa kufanya mabadiliko yoyote ndani ya CCM. Haiwezekani CCM hii iliyowatesa watanzania zaidi ya miaka 50 leo ilete neema kwa sababu ya Magufuli.-

Hakuna "theory" yoyote ya kisayansi duniani inayoweza kudhibitisha kuwa Gari bovu lililoshindwa kutembea kwa miaka 50, linaweza kukimbia speed 120 likipata dereva mpya.-

SAY NO TO CCM. Tunataka Rais mwenye akili za marais watano, ili marais wengine wa Afrika Mashariki wakimuona wamuogope na wamheshimu kwa kasi ya maendeleo atakayotuletea. Na Rais huyo ni Edward Ngoyai Lowassa peke yake. CCM Imechoka, tuitoe.!

MABADILIKO YANAANZA NA WEWE; CHUKUA HATUA SASA!!
 
Hizi siasa zinachosha sasa, kila tunavyozikwepa tunakutana nazo pande tofauti ambazo wala hutegemei kukutana nazo
 
Duuuh! Nna hasiraaaa!!! (weee letaaaa kikatio chaanguuu!) wanakalia kugawawana tuu mipesa yetuu mfyuuuuuu!!! hahah mkuu una hasira huku ni mahabati tyetyetye!!!
 
Lowasa atosha . siasa ni kama usipoyanywa utayaoga. siasa ni maishaaaa.
 
richard77

Dawa imeanza kuniingia! Ila magufuli ataya change haya
 
Last edited by a moderator:
ccm ni ile ile magufuli ni yule yule sera ni zile zile....chagua liwassaaaaa mabadiliko ya kweli.
 
Mzee Mtei,Mzee Ndesamburo,Mbowe,Lowassa wote wametusua chini ya hiyo hiyo CCM,kwanini sio baba zenu?
Hasira zenu anzieni kwanza kwa BABA ZENU!
 
Kuna mdau hapa JF aitwaye Malisa Godlisten alileta thread kama hii.Umekopy
kutoka kwake au yeye alikopi kutoka kwako? Mimi nachukia sana plagiarism!
https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania/936113-ccm-imechoka-tuitoe.html

Mkuu sioni tatizo la yeye kucopy. Kwangu mimi nashukuru kuisoma topic hii kwani hiyo unayosema amei copy mimi sikuwahi kuisoma. Cha muhimu ni ujumbe utufikie hata kama ujumbe huo utatumwa mara mia mbili. Tusiwakatishe tamaa watu wenye kutumia muda wao katika kutushirikisha kwenye vitu vya msingi. Heshima yako.
 
ccm ni ile ile magufuli ni yule yule sera ni zile zile....chagua liwassaaaaa mabadiliko ya kweli.

huu wimbo ccm wanauimba kila leo, lakini hawaoni maana yake kiundani! ni kweli ni ile ile, ni wale wale! kama ni waelewa umewasaidia kifasihi.
 
Nchi kubwa maana yake more mouths to feed! Kijana unakula kiroba na kumtegemea raisi aondoe umaskini hata ndani ya nyumba yako! Sasa kwa raisi anayefikiri kuwa lengo lake la kuingia ikulu ni kuondoa umaskini hata ktk nyumba za wavivu wewe ndiye unayemuona ana visions za kuliongoza taifi hili kweli!

Uchumi wa mataifa haujengwi na rais! Ni matunda ya wananchi wanaojituma kwa nguvu zao kuleta manufaa kwao na taifa lao!
Ona vijana wa kiasia kina mo, manji wamekulia hapahapa Bongo tena singida lkn wanaona fursa na kufanya vitu!

Kesi zote za wizi zilizobayana na zilizojificha ikiwemo ya raisi wako unayempalilia, pesa zao ziliishia kuhongwa na watoto wao au wao mwenyewe! Rejea- kina Liyumba, maranda et al!

Fanya kazi acha kuota ndoto za alinacha! Taifa hili litajengwa na vijana wenye visions sio hao wazee wenu wa propaganda, za kufuta umaskini bila kueleza how!
 
Halafu huyu Richard sio Yule wa Monduli? Richmond????? Imekaaje hii! Unajipigia debe bwana mdogo?

Kuwa mtafiti kidogo kuhusu Richmond.

Richmond City in Virginia

Richmond, the capital of Virginia, is among America’s oldest cities. Patrick Henry, a U.S. Founding Father, famously declared “Give me liberty or give me death” at its St. John's Church, leading to the Revolutionary War. The White House of the Confederacy, the Confederate States Army headquarters during the Civil War, is now a museum in Court End, a neighborhood known for Federal-style mansions.

Area: 161.9 km² Weather: 12°C, Wind N at 8 km/h, 87% Humidity Population: 214,114 (2013) Local time: Tuesday 12:12 AM Area codes: Area code 804 Cities: Warsaw, Robley, Sharps, Virginia
 
Nchi kubwa maana yake more mouth to feed!
Kijana unakula kiroba na kumtegemea raisi aondoe umaskini hata ndani ya nyumba yako!
Sasa kwa raisi anayefikiri kuwa lengo lake la kuingia ikulu ni kuondoa umaskini hata ktk nyumba za wavivu wewe ndiye unayemuona ana visions za kuliongoza taifi hili kweli!
Uchumi wa mataifa haujengwi na raisi!
Ni matunda ya wananchi wanaojituma kwa nguvu zao kuleta manufaa kwao na taifa lao!
Ona vijana wa kiasia kina mo, manji wamekulia hapahapa Bongo tena singida lkn wanaona fursa na kufanya vitu!
Kesi zote za wizi zilizobayana na zilizojificha ikiwemo ya raisi wako unayempalilia, pesa zao ziliishia kuhongwa na watoto wao au wao mwenyewe! Rejea- kina Liyumba, maranda et al!
Fanya kazi acha kuota ndoto za alinacha!
Taifa hili litajengwa na vijana wenye visions sio hao wazee wenu wa propaganda, za kufuta umaskini bila kueleza how!

vijana wanafanya kazi sana na wanajituma sana ila mazingira si rafiki,unaposema vijana hawafanyi kazi ww unahisi wanaishije????vijana wanakopesheka??vijana wametengenezewa mazingira???umeshawah kuona vijana wakikamatwa na mgambo kariakoo???acheni kuwabeza vijana wenzenu wasio na ajira mkahisi ni wavivu.......vijana na wanawake ni makundi yanayopambana na kurisk sana maisha yao hapa Nchini,si mijini si vijijini.Lets us be serious
 
Mzee Mtei,Mzee Ndesamburo,Mbowe,Lowassa wote wametusua chini ya hiyo hiyo CCM,kwanini sio baba zenu?
Hasira zenu anzieni kwanza kwa BABA ZENU!

Tatizo ni ccm imewalea hao wachache watusue ili sisi tuteseke kwa hiyo bora tuwaondoe walio sababisha wachache watusue na wengine wateseke
 
2kimo nilidhani kwa elimu yako ungeelewa kuwa Rais anamchango mkubwa kubuni mbinu za kuinua uchumi!!
Mfano Rwanda, Kenya, Ethiopia,Korea, Malesia, ziko nyingi ambazo sera nzuri za kiuchumi nchi zimeinuka!!
Hasa ukianza na elimu mengine yanafuata!!
Usikurupuke bila kufikiri, ukijenga viwanda vingi watu wako watakuwa vibarua, wataalamu wote watatoka nje ya nchi, Rwanda IT, Kenya Management, Uganda engineers !!
Maandalizi muhimu hata kwenye kilimo, madini, gessi, mafuta nyukria e t c!!
Elimu first priority, mengine yatapangika kuondoa umasikini!!
Urais sio pushups ni brains ili tukwamuke!!
Chagua UKAWA CHAGUA LOWASA KUONDOA UMASIKINI TANZANIA!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom