CCM imechoka ona hii sasa

CCM imechoka ona hii sasa

jamii yetu ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,amlofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!













 
Dogo richard77 na mwezako dogo KILIVITE naona umri unawasumbua
kwanini msisubiri Oktoba 2015 ukatumia Kura yako kuliko kuhutubia habari za laptop za Rwanda au kusubiri mikate ya kudondoshewa?
Hakuna Rais atakayekuja kuwawekea chakula mdomoni ingieni maporini mkafyeke mfungue mashamba ya vitunguu kma Sharif Hamad alivyowaasa hakuna serikali ya Nchi hapa duniani leo inayowapa kazi vijana direct ila mkajiajiri
01.JPG
 
2kimo nilidhani kwa elimu yako ungeelewa kuwa Rais anamchango mkubwa kubuni mbinu za kuinua uchumi!!
Mfano Rwanda, Kenya, Ethiopia,Korea, Malesia, ziko nyingi ambazo sera nzuri za kiuchumi nchi zimeinuka!!
Hasa ukianza na elimu mengine yanafuata!!
Usikurupuke bila kufikiri, ukijenga viwanda vingi watu wako watakuwa vibarua, wataalamu wote watatoka nje ya nchi, Rwanda IT, Kenya Management, Uganda engineers !!
Maandalizi muhimu hata kwenye kilimo, madini, gessi, mafuta nyukria e t c!!
Elimu first priority, mengine yatapangika kuondoa umasikini!!
Urais sio pushups ni brains ili tukwamuke!!
Chagua UKAWA CHAGUA LOWASA KUONDOA UMASIKINI TANZANIA!!

Bwana mtumishi sidhani kama tunaweza kumpata raisi mtaalamu wa yote hayo!
Wakati wa kampeni tunamtaka raisi mwenye vision na aliyekuja na package (sera) yenye viashiria kuwa maeneo kadhaa ya maendeleo yatafanyiwa kazi!
Kubuni ajira, kuboresha huduma, michezo na kadhalika hizo ni kazi za wataalam husika watakachohitaji wataalam ni mazingira rafiki tu ktk kutekeleza hayo!
Kama unazungumzia Sera hadi sasa sijasikia Sera anazosimamia Lowasa ni zipi, hakuna anapotoa ufafanuzi wa kitu chochote. Yeye anaheadings zake, elimu, umaskini na Mama lishe hakuna anayejua details labda Mama Regina!
Hataki mdahalo labda angefunguka zaidi!
Lakini nini nafasi ya vijana ktk kuhakikisha maendeleo kwa umma! Wapo vijana wachache wa kitanzania waliopewa fursa tena kubwa kulikomwanazopata vijana wa kenya na mataifa mengine ya jirani! Ona wasomi wetu wa vyuo vikuu wanaipa nafasi gani taaluma! Waulize wengi wao how many hours wanaspend ktk elimu? Wengi wanapoteza muda ktk issues ambazo sio academic! Ukikutana na Kijana wa kihindi shuleni atakuwa anajali zaidi elimu kuliko huyu wa kibantu! Tuna shida somewhere namkama hatutaki kuwa wakweli na kuliangalia hili tutalia kila siku!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom