CCM imechanganyikiwa?

CCM imechanganyikiwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,096
Reaction score
828,926
Huu ni zaidi ya utoto na ulemavu wa kukosa tafakuri... Haya yanayoendelea nchini nikiri wazi kuwa pamoja na kwamba kuna matukio ya kutisha ya kuwashambulia wapinzani kwa silaha za moto na silaha nyingine zenye kujeruhi na kusababisha ulemavu....

Lakini hili la kutumia ushawishi wa ahadi za mali pesa vyeo na ulinzi kwenye bishana ili watu warejee ccm ni uhuni na michezo ya kitoto kabisa

Tusijaribu kuwaiga Rwanda.... Ukubwa wa ile nchi ni sawa na mkoa mmoja wa Tanzania... Tusiige zile siasa kuna kuna mvutano wa makabila mawili... Siasa za pale zinahusika sana na ukabila
Tumeshashuhudia yaliyotokea kwenye uchaguzi wa madiwani hivi karibuni, watu wameumizwa sana.. Watu wamejeruhiwa sana, watu wamebambikiwa kesi sana... Hii ni ishara gani kwenye uchaguzi 2020?(kama utakuwepo lakini) tofauti ya hoja ndio tuumizane kiasi hiki? Vyombo vyetu vya usalama na tume ya uchaguzi vimevaa miwani ya mbao

Kama hii haitoshi pamoja na kufanya yale yote kwenye uchaguzi ule sasa ni mwendo wa kununua wapinzani... Naamini kuna kundi kubwa sana ndani ya ccm wanashangazwa na haya lakini hawana pa kusemea.. Hawa wanaonunuliwa wanaenda kutupwa huko... Ni uchoyo na ulafi wa aina yake... Ni sawa na kuwa na makabati ya nguo lakini bado unataka na za jirani....

Hawa wanaonunuliwa hawaendi kuonyesha vipawa vyao huko, wanaenda kuminywa na kufichwa ili mradi tu kukomoa kaliba fulani ya watu...

Hivi kipaumbele ni kuua upinzani? Ingekuwa mashindano yako hivyo kusingekuwa na kushindana basi... Tunapoteza muda mwingi kwenye siasa za kipuuzi kabisa.. Mwisho wa siku morali wa kujenga taifa unashuka kabisa.... ccm halisi wanabaki na kinyongo, ccm makinikia wanakuwa na hofu na kutojiamini.... Mwendo mpya wa kuwindana kusimangana na kuchomeana unaaza.... Ni aina gani hii ya siasa mnafanya?

Mtanunua wangapi? Mtawabana wangapi ili waombe Po na kujiunga nanyi? Kumbukeni kuna kura million 6 +, tena hizi mmezitamka nyie... Uhalisia ni kwamba zipo zaidi ya hapo tena kwa mbali sana....

Tunawakemea kwa sauti ya uzalendo hamjengi bali mnabomoa, hamtengenezi bali mnaharibu.. Hamuunganishi bali mnatenaganisha.... Huu ni uwendawazimu na kukosa tafakuri... Hivi mmesahau kuwa WAKATI SI MILELE?!?!??
 
Naomba wale wote wananchi ambao itikadi yetu ya upinzani ni IMANI au tunaopenda demokrasia tusife moyo na tusiwaamini hawa wanasiasa vigeugeu,yaan mtu anaongea mpaka unaemsikiliza unaona aibu
 
mshana jr

Tungepata waonyaji na wakemeaji wa huu uhuni ingependeza haiwezekani mtu mmoja apeleke nchi jinsi anavyotaka Hata Kama kakosea asikosolewe hii sio fair. Ila akumbuke atawadanganya Watu Wote ila sio Siku zote. Ajifunze Kwa Mugabe Ipo Siku udhalimu utafika mwisho. Kila mtu anaogopa yy ni Nani???

Tz haijawa kilaza Namna hii au ni kizazi cha zilipendwa haki yanane I wish I could be meja General.
Mungu tusaidie!!!
 
Kama kuna ushahidi wa ccm kuhusika ni kweli inapaswa kukemewa kwa nguvu zote, lkn wasi wasi wangu makamanda jahazi linatoboka baada ya kujadili nini tatizo mnakuja na visingizio lukuki. Wanachama wanakimbia eti oohh wanahongwa sababu nyepesi kweli kweli.

Kwa sasa mmekosa mtu kama slaa mnabaki kulia lia tu mitandaoni. Ukweli ni kuwa mmewaangusha wananchí hata kabla ya kupewa dola, mlichobakisha kwa sasa kila anaekuambieni ukweli eti ccm. Edo na wengine kadhaa wapo njiani nyie katafteni flash mseme wanahongwa.
 
Hivi ukiwa CCM ujinga unahusika? Upofu na uziwi je?!! Huoni kinacho endelea wala husikii...?!! Hata kuwaza kweli huwezi?! ....mkuu wa wilaya wakati ananunua watu Arumeru wewe ulikuwa wapi? uko dunia gn?!! .Naamini wapo CCM welevu hasa na IPO siku watapata pa kusemea.@Mshana
 
Back
Top Bottom