CCM ilifanyia tathmini matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita lakini haikufanyia kazi mapendekezo ya tathmini hiyo!

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
CCM kama chama inaweza kusumbuka kwenye uchaguzi wa 2020.

Hata bila kuwa ndani ya chama hicho, ukiangalia kwa nje kuna picha unaweza kuona!

Wakati Nape anafungia bunge live na baadhi ya magazeti nadhani ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotokana na tathmini ya uchaguzi mkuu 2015.

Kwa bahati mbaya timu ya utendaji ndani ya chama na kwenye serikali ambayo rais Magufulia alianza nayo kazi, ilimtia wasiwasi na hofu mapema sana, hivyo akaamua kuishughulikia!

Nadhani kosa la kwanza kabisa kwa rais Magufuli kama mwenyekiti wa chama kisiasa lilianzia hapa!

Mfano, wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu 2015 kulikuwa na malalamiko mengi ya wagombea wa ubunge na udiwani waliopitishwa bila kufuata michakato inayokubalika kichama. Hii ilikuwa moja ya sababu ya wao kuanguka mapema kabla hata kura hazijapigwa.
Jambo hili lilipaswa kuwa limefanyiwa kazi na wahusika kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Well, halijafanyiwa kazi na ni kama hiyo michakato ndani ya chama imekufa kifo cha jumla jumla- chaguzi ndogo zilizofanyika zitakuwa shahidi wangu!

Sasa kuna mseto wa sura, harufu, sera, mawazo na malengo ndani ya CCM wa kutosha. Watu wamenunuliwa kutoka karibu vyama vyote vya siasa na wakawa wana CCM na viongozi on short notice. Hawa sijui watablend vipi na ile CCM ya asili kwenye mchakato wa kutafuta wagombea.

Polisi kwa uzoefu wangu kwenye uchaguzi mkuu wanakuwaga wachache kutokana na wingi wa watu na matukio.
Haitakuwa rahisi kupitisha wagombea wote kwa nguvu ya polisi hasa ukizingatia mpasuko utakaokuwepo ndani ya chama.

Kutakuwa na wagombea wa mfukoni kuanzia ngazi ya urais mpaka udiwani!
Na wakati huu wa kugombea ugali na kuonyesha unazi katika chama sioni wanaCCM wakikubali kunyamazishwa kirahisi.

Upinzani ujipange tu, hii game inaweza kuwa rahisi mno maana badala ya kupambana na chama na wanachama, tutakuwa tunapambana na mtu mmoja ambaye nae atakuwa anapigania ugali wake!

Ila usalama wa wagombea uhakikishwe maana uchaguzi huu una harufu ya damu!
 
Umeandika ukweli mtupu
 
Kuna picha ambayo wanaCCM hawaioni, chama sasa kinamtegemea mwenyekiti na polisi kusurvive!

Kama picha ikibadilika akapitishwa mgombea mwingine ambaye ni 'non-violent'
Na akasimamia sera zenye tija kwenye kampeni na sio ubabe, hao wagombea wa ubunge na udiwani watakaokuwa wametokea mfukoni watapukutika kama majani.
Umeandika ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom