CCM Ilala yapinga uchaguzi wa Meya

CCM Ilala yapinga uchaguzi wa Meya

Mkurugenzi wa Manispaa sio mbumbumbu. Kabla ya kufanya hivyo amechambua kwa makini hoja za pande zote kwenye suala hili la ushiriki wa wajumbe kwenye uchaguzi huu.
Hapa unampa sifa mkurugenzi za buleeee! Huhitaji hata kufungua kifungu cha sheria/katiba inayowakataza wabunge/madiwani wa Z'bar kushiriki uchaguzi huo. Ila unahitaji gharama ya ujinga wa kutupwa ili kuhalalisha uwepo wa wabunge wa Z'bar katika uchaguzi wa bara hususani kipindi hiki cha sito fahamu ya uchaguzi wa Z'bar. Hakuna madiwani/Wabunge madhalani wa Kigoma, Iringa n.k wanaoishi Dar? Kwanini na wao wasishiriki?
 
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wake wa Wilaya hiyo Asaa Simba aliponukuliwa na gazeti la mwananchi.

Amesema wapo kwenye mchakato wa kumburuza mahakamani Mkurugenzi wa manispaa hiyo Isaya Mngurumi.

Akiendelea kufunguka zaidi Simba alisema mojawapo ya sababu zilizosababisha wakagomea uchaguzi huo ni kuzuiliwa wabunge wanane wa viti maalum wakiwemo waliotoka mikoa ya Zanzibar.
Sasa Wabunge kutoka Zanzibar wanapiga vipi kura ya kumchagua Meya wa Ilala. Hapo ndipo ninapowaomba wataalamu wa mambo ya sheria wanisaidie. Mbunge wa Zanzibar anahusika vipi na udiwani wa Ilala. Waende tu mahakamani ili mahakama ikatoe tafsiri sahihi. Lakini swala lenyewe lilivokaa ni kichekesho kitupu.
 
Tunakuomba Mh Asaa Simba uje ujibu hii .
Hiki chama kinaumwa ugonjwa mbaya kabisa na kiko taabani icu

Mi nilishajua CCM isipoanza upya ni tatizo tu. Ukitaka kujua ubovu wa CCM angalia wajumbe wa CC na mkutano mkuu. Wanachoweza kufanya kwa ufasaha kabisa ni kunengua. Hawana msaada wowote wa kukijenga chama.
 
Sasa Wabunge kutoka Zanzibar wanapiga vipi kura ya kumchagua Meya wa Ilala. Hapo ndipo ninapowaomba wataalamu wa mambo ya sheria wanisaidie. Mbunge wa Zanzibar anahusika vipi na udiwani wa Ilala. Waende tu mahakamani ili mahakama ikatoe tafsiri sahihi. Lakini swala lenyewe lilivokaa ni kichekesho kitupu.
Mkuu lisilowezekana kwa mwana chama wa chama cha siasa tofauti na ccm,kwa mwana ccm linawezekana
 
Mi nilishajua CCM isipoanza upya ni tatizo tu. Ukitaka kujua ubovu wa CCM angalia wajumbe wa CC na mkutano mkuu. Wanachoweza kufanya kwa ufasaha kabisa ni kunengua. Hawana msaada wowote wa kukijenga chama.
Duuuuu nimefurahisana na kupiga vigeregere
 
ni kweli lakini safari hii kuna mabadiliko makubwa sana .
Mwambie aende tandahimba,aende newala , aende ndanda aende kilwa huko ndio ccm walikuwa wanajizolea kura bila wasiwasi lkn akaulize nini ccm kimewapata mwaka huu
 
Hatujazoea kushindwa. Tukiahindwa tunarudia Uchaguzi.
 
Huyo asaa simba gajui hata hesabu za kujumlisha wao walikua 19 na hao nane waliozuiliwa unapata 27 ukawa wamepata kura 31 .sasa kesi ya nn hapo si anajitafutia deni la garama ya kesi!
 
Mi nilishajua CCM isipoanza upya ni tatizo tu. Ukitaka kujua ubovu wa CCM angalia wajumbe wa CC na mkutano mkuu. Wanachoweza kufanya kwa ufasaha kabisa ni kunengua. Hawana msaada wowote wa kukijenga chama.
umeandika ukweli lakini wenye kufedhehesha sana ! nimejikuta naangalia chini kwa aibu .
 
Nitashangaa hata wakili atakayepokea kesi hiyo kama ni kupiga pesa sawa lakini kitaaluma aibu
 
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wake wa Wilaya hiyo Asaa Simba aliponukuliwa na gazeti la mwananchi.

Amesema wapo kwenye mchakato wa kumburuza mahakamani Mkurugenzi wa manispaa hiyo Isaya Mngurumi.

Akiendelea kufunguka zaidi Simba alisema mojawapo ya sababu zilizosababisha wakagomea uchaguzi huo ni kuzuiliwa wabunge wanane wa viti maalum wakiwemo waliotoka mikoa ya Zanzibar.
Naomba kuuliza, miaka yote ya uchaguzi kama huo uwa wanafanya hivyo walivyotaka kufanya??
 
Kw jiyo walitaka hao wabunge wao 8 nao waoige kura?
Haya basi na tufanye matkeo ni ,31 kwa 28 badala ya 31 - 0.
 
Hivi hichi chama kinajua kunamushindwa maana wao wakishindwa wanasema palikua na fitna. Waache hizo wakubali matokeo kazi ianze
 
Wabunge wa viti maalum kutoka Zanzibar wanahusika vipi na Jimbo la Ilala.

Huu utetezi hauna mashiko kinachotakiwa sasa hivi ni kushirikiana na hao Mameya wa Ukawa kuwatumikia watanzania.

Ahsanta!
 
Back
Top Bottom